Thursday, August 28, 2008

AGOSTI 28, 2008 WIMBO WA TAIFA

Usiku mzima leo sijalala kisa nilikuwa nimekumbuka sana wakati nasoma shule na msingi na kuimba wimbo huu:-


Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.


Tanzania Tanzania,
Ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu,
Biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi,
Mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote


Tanzania Tanzania,
Watu wako ni wema sana,
Nchi ngingi zakuota,
Nuru yako hakuna tena,
N wageni wakukimbilia,
Ngome yako imara kweli wee,
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa.



Nchi nzuri Tanzania,
Karibu wasio kwao,
Wenye shida na taabu,
Kukimbizwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha,
Mpigane kiume chema wee,
Tanzania Tanzania
Mola awe nawe daima.

2 comments:

Anonymous said...

Hivi Tanzania tuna nyimbo Mbili za taifa?
Nilikuwa sijui na bado sijaelewa.

Yasinta Ngonyani said...

Ni wimbo wa taifa sasa unajua na ni kibwagizo pia. je unataka kuniambia wewe hujawahi kuimba?