Saturday, August 23, 2008

AGOSTI 23,2008 MIMI NDIVYO NILIVYO

Udadisi;- Watu wengi wamechoka na mimi kutokana na udadisi wangu, maswali yangu pia. Wanasema huwa hawapati jibu waulizapo swali/maswali. Badala ya kupata jibu, wanapata swali pia. kama vilw KWA NINI? Ni kweli huwa nafanya hivi, sio kwamba nataka kuwatesa wao hapana ila ndivyo nilivyo au niseme ndivyo nilivyozaliwa. Na nimekwisha zoea ila sasa wengi wanaona kero sana. Je ni tabia mbaya kufanya hivyo? Nisaidieni wasomaji.

3 comments:

Unknown said...

Si kero bali hii ni kudhihirisha kwamba wewe ni Mtanzania halisi, maana hata ukiulizwa swali badala ya kujibu na wewe unauliza!
Nahisi kwa mtu ambaye hajui watanzania wapoje likija suala la maswali na majibu hii inaweza kuwa kero ila kwa sisi wengine tunajua ni kawaida tu, na hapo tutaulizana maswali bila majibu hadi kila mmoja mimi na wewe turidhike, maana ndivyo tulivyo.

Naamini sijakusumbua

Anonymous said...

Moja ya matokeo yanayochangia katika tabia ya kuuliza maswali/kutojibu maswali ni matumizi ya lugha/kuogopa kujibu swali maana wabongo tuna tabia ya kudhani ukiulizwa basi umetegewa/kuwekewa mtego.Ukweli ni kwamba watu wengi wamekuwa wakishindwa ua kutoelewa maana ya kuulizwa maswali shauri wamezoea maisha ya kutojiuliza yaani wanaishi kwa mazoea hasa sisi wabongo.Suala la kutojibu/kujibu linaathiri sana mawasiliano kati yetu sisi wanadamu.Mfano mtu anauliza swali halafu unajibu swali hilo lakini kwakuwa matumizi ya lugha hayajulikani kwake/kwako kunazuka swali ambalo linajijibu iwapo unyumbulishaji wa lugha iliyotumika.Matumizi ya lugha yamewafanya watu wengi wasielewe uhalisia wake,pia unaweza kutumia lugha mfano kiswahili chetu halafu ukaona mtu anauliza kitu/jambo ambalo pengine tayari lina jibu lake bila hata kuuliza.Makosa yanayofanyika katika matumizi ya lugha yanaathiri sana mawasiliano na kuonekana usumbufu/kero.Kuuliza swali siyo maana yake mtu anateseka bali inawezekana wengine wanaona kuulizwa kwao ni mwiko lakini hili si jambo la kawaida.Kwanini? mara nyingi nimekuwa nikipata taabu ninapofanya mazungumzo na watu/katika mawasialiano hii inatokana na kile nilichokigundua kwamba uwezo duni wa matumizi ya lugha ya kiswahili/kuelewa.Iwapo mtu anatumia kiswahili fasaha hakika unaweza kujikuta unawasiliana na watu wawili au mmoja tu.mimi naitwa msumbufu/ninakera sabau tu huwa napenda kuuliza na kupata uhakika wa jambo/kitu.
Inawezekana wengine wanakuchoka dadangu pengine kwa kutoelewa umuhimu wa urafiki/kuwasialiana/kuulizana shauri wamezoea kutouliza hasa wabongo na pia wakati mwingine matumizi ya lugha yanaashiria uwezo wa lugha yenyewe.USHAURI usikate tamaa kwani duniani tupo kwa ajili ya wengine hivyo tunahitaji wengine ili tushamirishe uwepo katika dunia hii.Aghalabu sisi wabongo twajiita watulivu na wenye amani lakini ukweli wabongo kuulizwa hatutaki sijui kwanini na ukizidi kuwauuliza utasikia huyu jamaa anapenda mambo ya udaku eti sababu tu umeuliza.Mfano mimi siachi kuuliza lakini pia napata taabu iwapo lugha inayotumika ni duni au pengine ukijibu lugha haifafanuliwi na mhitaji jawabu hapo ndipo panapozuka kile unachodhani dadangu kwamba wamekuchoka.Je matumizi yako ya lugha unajua kufafanua/kunyumbulisha/kuitafsiri lugha ili ushamirishe kupunguza maswali? maana wakati mwingine huhitaji kuuliza iwapo unaona mnyumbuliko/fasiri ya lugha/matumizi ya lugha yako wazi. Sijui usije ukanihesabu na mimi bure,mie simo mtajiju karibuni nyasa

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni sana kwa maoni yenu mazuri kaka zangu. Lakini hii kwa mimi imekuwa ni mazoea sio lugha kwani siwezi kabisa kujibu swali moja kwa moja bili kuuliza kwa nini hata kama ni baba yangu mzazi ananiuliza hii sio kwa mtu mmoja tu hapana. Ila nitajitahidi kuacha kuuliza.