Sunday, August 31, 2008

AGOSTI 31, 2008 NYUMBANI(KUNYUMBA)

Peramiho kwa mbali






Kanisa la Peramiho




Angalien jinsi kunavyopendeza au mnasemaje. msione aibu jamani ni kuzuri. Karibuni sana Ruvuma Peramiho.

6 comments:

Anonymous said...

mmm jamani hakika umenikumbusha sana Abate Lambert kwani nilipomaliza kidato cha sita 2005 aliwahi kunihoji iwapo naweza kujiunga na seminari ili nifaute nyayo za baba yangu mkubwa padre chiwangu kongocha. mwenzenu nilimwambia haraka sana kwamba ndoto hizo zimekufa naogopa kuharibu kanuni za mwenyezi mungu

Egidio Ndabagoye said...

Duh Markus yahitajika wito.Zamani nilikuwa napenda sana kuwa "faza" nilivyokuwa naona magari mazuri mazuri wanayoendesha enzi hizo,lakini baadae nilikata tamaa na hilo la kuishi konventini peke yangu.

Katika mikoa ambayo sijakanyaga ni kusini.Siku moja nitakuja huko.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

nina mengi sana ya kuandika kuhusu huu mtundiko.

Nimekumbuka mengi sana.

Naomba nichukue nafasi hii kuomba ruksa ya kutumia pichayako ili niweze kuandika niliyoyaona na kukumbuka nilipofika Ruvuma.

Yasinta Ngonyani said...

Haya kaka edwin unaruhusiwa kutumia picha lakini sijui ipi. Kwani natamani sana kusoma hiyo habari unayotaka kuiandika. Na kaka egidio KARIBU SANA RUVUMA

Kibunango said...

MMhm... Hapo Peramiho miaka ile ya themanini ilikuwa kama kwenda ulaya. Siku za Jumamosi walikuwa wanauza nguo nzuri sana na viatu vizuri

Wale wapenzi wa Mkuu wa Meza waliweza kununua kila watakazo....

Anyway huu utaratibu bado upo hapo Peramiho?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka kibunango kusema kweli sijui ila nadhani bado. Ila ni kweli nakumbuka wakati ule miaka ya 80-90 ukifika peramiho mmh