Thursday, March 9, 2017

MNAKUMBUKA HII?

Mimi nakumbuka sana.....wazazi wanaondoka kwenda shamba nawe unaachiwa wadogo zako uwatunze na papo hapo labda kuchochea maharege. Nakumbuka siku moja niliunguza maharage, ila hata hivi niliachiwa mdogo wangu mmoja...ila sasa kucheza nako. Ila kusema kweli binafsi ninapenda sana utamaduni huu ingeendelea. Maana hapa ndipo mtoto/watoto wanapojifunza kazi  za nyumbani... Kwa hiyo naweza nikasema nayapenda zaidi maisha ya kale/enzi zangu.

2 comments:

Salehe Msanda said...

Habari!
Makuzi hayo yalikuwa muhimu na yalikuwa yanaakisi uhalisi wa maisha yetu na hasa utamaduni na mila
Ikiwa ni pamoja na kujenga umoja kupenda na kuwa watu wenye ushirikiano.
Kumbuka huko kucheza kulikosababisha maharage yaungue ulikiwa unacheza na watoto wa jirani na kufanya ule ujamaa wa kiasili kushamiri baina yetu. sasa hivii tunakoelekea siko tunakazi ya ziada kuyaenzi mazurii ya enzi hizo

Kila la kheri

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salehe za masiku?
Samahani kwa kuchelewa kujibu majukumu. Nafurahi sana kuwa hujanisahau /hujasahau kunitia moyo katika kublog...AHSANTE SANA