Nimekumbuka leo nilipokuwa mtoto nilikuwa nikipata taabu sana kuhusu mwaka mpya ufikapo.
Katija akili yangu nilifikiri MWAKA MPYA ni kila kitu hubadilika na kuwa kipya hususan rangi ya Mbingu. Kumbe hapana, nilipoendelea kupata akili mambo hayakubadilika. Hapo sasa udadisi ukazidi nikawa namuuliza kila mtu aliye nizidi umri MWAKA MPYA ina maana gani?
Nikawa napata majibu tofauti tofauti:- kama vile...
1. Mwaka ni jumla ya miezi kumi na mbili.
2. Mwaka ni siku nyingi.
3. Mwaka ni siku inayoadhimishwa baada ya kibunzi.
Na kibunzi ikiwa na maana siku kuaga mwaka, mkesha wa kuaga mwaka mwisho wa mwaka au pia ni aina ya ubao unaotiwa mchanga utumiwao na waganga wa asili kupigia ramli.
Mh!...nikawa najiuliza kwanini isiitwe tu NAMBA MPYA maana ni namba tu 2016?
Upya wake ni nini kwa wale walioishi miaka 80, 50 au 30? Na je kwa nini tunapotimiza miaka isiitwe KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KUZALIWA? Badala yake tunasema BIRTHDAY.
Bado natafakari.
No comments:
Post a Comment