Thursday, January 28, 2016

AMA KWELI...LEO NIMEYAKUMBUKA SANA HAYA MATUNDA ....

Nilipokuwa msichana mdogo wakati tukiishi kijiji cha LUNDO huko nyasa, nyumbani kwetu tulikuwa na miti miwili ya matunda haya. Nasi tulikuwa tukiyaita "farafaraji" (Red mulberry).....ni matamu sana. Pia kitu kimoja nilikuwa najivuna ni kwamba nilikuwa sikosi marafiki  tulikuwa tukila pamoja...Nimeyakumbuka sanaaa:-)

3 comments:

Nicky Mwangoka said...

WAAAW matunda damu, sie tulikuwa tunayaita 'madalaa'

Anonymous said...

Na mashaka kaka Nicky Mwangoka kuwa hayo SI matunda damu! Naona kama yana vimwiba mwiba kwa nje ukiangalia sana na matunda damu hayana halafu haya ni madogo zaidi, matunda damu makubwa kuzidi hayo. Ila si mtaalamu ngoja dada Yasinta atujuze kama ni matunda damu au la? Na wengine pia. Asante dada yasinta nimeyala kwa macho tu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Nick! haya matunda nina uhakika ni "farafaraji" kama nilivyosema. Ila inawezekana kwa vile ukiyashika yanaacha rangi nyekundu.

Usiye na jina...kwa nijuavyo mimi ni kwamba matunda damu ni makubwa kwa mfano wa yai. kama hayapo ya Aina nyingi. nitaweka picha yake wiki ijayo.