Tuesday, January 5, 2016

LEO NI TAREHE ALIYOZALIWA KAPULYA .. :-) AMETIMIZA MIAKA KADHAAA

Aama kweli miaka inakwenda ...kuna wakati natamani kuwa mdogo tena ....Hapa ni Njombe 2014/15
HAPA NI MSOSI TU...KARIBUNI

Leo ni tarehe/siku kama ile  familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa na furaha kumpata binti yao ambaye alizaliwa kama tarehe hii ya leo 5/1. Na leo ameongeza mwaka tena na kuzidi kuzeeka:-). Lakini hata hivyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...Pia salamu na HONGERA nyingi kwa wale wote wanaotimiza miaka mwezi huu wa kwanza/Januari pia.   Nachukua nafasi hii  kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama  na namwomba azidi kunilinda/kutulinda salama. 
Naona tumalizia na mwimba huu ni kwa Neema na Rehema...na Edson Mwasabwite...

9 comments:

Manka said...

Heri ya kuzaliwa Dada Yasinta, Mwenyenzi Mungu akupe maisha marefu na yenye Baraka Tele, heri ya mwaka mpya

Anonymous said...

Happy birthday da Yasinta. mwenyezi Mungu akubariki na akupe mafanikio yote unayoyataka. By Salumu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Heri ya kuzaliwa na inshallah Mwenyezi Mungu akuongezee makumi mengine mengi ya miaka uwaona wajukuu vitukuu vilembwe na vilembwekezi.

Mbele said...

Nakutakia kila la heri.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu Manka..Kwanza habari za siku nyingi na Kheri sana ya mwaka mpya. Ahsante sana kwa kuwa nami katika siku yangu ya kutimiza miaka.

Kaka Salumu! Ahsante sana kwa kutonitenga...na pia kwa baraka ulizonitakia nimezipokea kwa mikono miwili.

Kaka Mhango! Umeifanya siku inoge zaidi. Ila du kweli nitaweza kutembea nikiishi hadi vitukuu vlembwe na vilembwekezi itabidi wawe wananitoa njekuliona jua na kuniingiza tena ndani:-)

Pro. Mbele Ahsanti nga maha!

Anonymous said...

Happy birthday Yasinta. Mungu akubariki sana katika maisha yako yote.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 5:27AM..Ahsante sana.

Penina Simon said...

HAPPY BIRTDAY YASINTA.
I can imagine lazima ulipika chakula cha nyumbani

Yasinta Ngonyani said...

Dada P...Ahsante sana ..ni kwelnilipika pilau kidogo