kati ya nyimbo zake huwa sichoki kuusikiliza 'Karola'
kipande cha kwanza kinaenda hivi:
"Ukiwa mtenda mabaya wewe mwenyewe haujijui Ukiwa mtenda mabaya kila siku unasema unaonewa Ukiwa mtenda mabaya huko unakokwenda ni pabaya Ukiwa na roho mbaya eeh kweli tutakuogopa Ukiwa na pesa nyingi usahau hata ndugu zako kweli walimwengu hawana wema Mola awape nini"
katika wimbo huu tumba, saxaphone na solo guitar la yeye mwenyewe huwa vinanikuna. hasa tumba.
Remmy Ongala katutangulia lakini nyuma kaacha kielelezo cha muziki wa dansi iliyo hai. Kifo chake kinathibitisha kutokomea muziki wa dansi na kushamiri huu wa "ubongo wa fleva"
12 comments:
R.I.P!
Wimbo wa kifo aloimba ni kweli na sasa kifo kimemchukua mola aweke roho yake mahala pema amin.
Sad, very sad......Mungu ameumba na Mungu amechukua, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
Mungu ailaze riho yake mahala pema peponi.
Sisi tulimpenda, lakini bwana amempenda zaidi. Pumzika kwa amani Mzee Ongala... ni msiba mkubwa kwa waTanzania.
RIP dokta remmy.
kati ya nyimbo zake huwa sichoki kuusikiliza 'Karola'
kipande cha kwanza kinaenda hivi:
"Ukiwa mtenda mabaya
wewe mwenyewe haujijui
Ukiwa mtenda mabaya
kila siku unasema unaonewa
Ukiwa mtenda mabaya
huko unakokwenda ni pabaya
Ukiwa na roho mbaya eeh
kweli tutakuogopa
Ukiwa na pesa nyingi
usahau hata ndugu zako
kweli walimwengu hawana wema
Mola awape nini"
katika wimbo huu tumba, saxaphone na solo guitar la yeye mwenyewe huwa vinanikuna. hasa tumba.
Remmy Ongala katutangulia lakini nyuma kaacha kielelezo cha muziki wa dansi iliyo hai. Kifo chake kinathibitisha kutokomea muziki wa dansi na kushamiri huu wa "ubongo wa fleva"
hakika ni pengo
Mungu ailaze roho yake pema peponi!
RIP dokta remi
eti Mungu ailaze roho mahala pema peopni, unadhani kuna kusikokwema peponi??
Ninachomshukuru Mungu amekufa akiwa ameokoka.
Kapumzike kwa amani.
@Da Mija: Je angekufa MUISLAMU unafikiri isingekuwa poa zaidi?
Kitururu hata waislamu wapo waliookoka, na usisahau ukristo sio kuokoka.
Bado nalifikiria swali lako kiundani lakini..
Ubarikiwe sana.
Post a Comment