Tuesday, May 30, 2017

MSIBA MKUBWA UMETUPATA UKOO WA AKINA NGONYANI PERAMIHO /LUNDUSI BABA/BABU NA KIONGOZI WETU KATUTANGULIA MBELE ZA MUNGU LEO MAPEMA ASUBUHI

 Hii picha ni wakati wa uhai wake hapa ilikuwa 2005 nyumbani kwetu LITUMBANDYOSI yeye ni huyo mwenye miwani yupo pamoja na wdogo zake.
Na hapa yupo na moja wa wajukuu zake ilikuwa mwaka 2016 November. Babu yetu Lotary  amekuw akiugua tangu kipindi cha pasaka
Na hapa ni picha yake ya mwisho iliyopigwa 28/12/2016.Wewe Ulikuwa Kiongozi wa ukoo wa akina Ngonyani, babu yetu,  baba yetu na pia mshauri mzuri sana pale mtu atakapo ushauri. TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU  ATUTIE NGUVU KWA KIPINDI HIKI CHA MAOMBELEZO. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIMIWE. UPUMZIKE KWA AMANI BABU YANGU/YETU. AMINA

6 comments:

Anonymous said...

RIP Babu, Pole da Yasinta. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kaka Salumu....

Rachel siwa Isaac said...

poleni sana wapendwa Mungu akawe mfariji wenu..
Apumzike kwa Aamni Babu.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kachiki wangu

NN Mhango said...

Nguzo kama hii inapoanguka na kurejea ilikotoka wengi husikitika. Wajukuu hufurahi kwa sababu ya mazoea ingawa ndani ya mioyo yao huwa kuna masikitiko kuondokewa na waliyempenda na kumzoea. Najua ni kiasi gani inaumiza hasa kwa watu wa karibu. Najua uchungu na hasara wanayoihisi mioyoni. Kwani, japo binadamu kufa ni faradhi, huwa hatujiandai wala kukubali haraka inapotokea. Nawapeni mkono wa rambirambi au tuseme makiwa wafiliwa wote. Da Yasinta jikaze; hicho ndicho kilimwengu hasa unapokua.
Bwana alitoa; Bwana ametwaa. Bwana anajua; nasi twapasa kujua.

Mbele said...

Mungu awe nanyi daima.