Friday, May 5, 2017

BADO NIPO RUHUWIKO/SONGEA NAKULA VYETU VYA ASILI

ASUBUHI... Karibu chai na maboga
Na baada ya chai na maboga mchana huu karibu tule mahindi ya kuchoma

5 comments:

Mbele said...

Dada Yasinta, ni jambo la kushukuru kuwa una bahati hiyo ya kufika nyumbani kwenye hivyo vyakula bora, hewa nzuri, na kadhalika. Umenifanya nitamani ningekuwa huko Ruvuma wakati huu wa maboga na mahindi mabichi. Kuna dada yangu anaishi hapo hapo Ruhuwiko. Nakutakia mapumziko mema.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante...nakumbuka uliniambia hilo la dada yupo Ruhuwiko. ..kwa kweli ni vyakula bora na vitamu mno-:)

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yasinta, sikujua kuwa ulikwenda hijja. Una kila haki ya kusherehekea vya kwetu hasa ukizingatia kuwa huku ughaibuni vingi tunavyokula ni vya bandia ukiachia mbali wasi wasi wa kulishwa hata vyakula vilivyochezewa kinasaba. Hayo mahindi we acha tu. Natamani picha iwe kweli nichukue hapo hapo angalau. Huku napata mahindi lakini hayana ladha wala utamu kama ya nyumbani. Napata hata nyanya chungu na magimbi lakini havifikii vya nyumbani.
Endelea kufaidi hijja yako kwenye nchi takatifu chimbuko la kila kitu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango:-) najua n hamu gani uliyonayo kwa hiyo ni bora ukule kwa macho tu-:) Naungana nawe asilimia 100% kuwa vyakula vya kunyumba ni VITAMU SANA. umenitamanisha hizo nyanya chungu na magimbi...vipi unapata bambia pia?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bambia ndiyo nini au unaanisha bamia? Kama bamia zipo sana tu toka Mexico na Marekani. Karibu Kanada ule nyanya chungu hadi uzikimbie.