Wednesday, December 2, 2009

LEO NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WASOMAJI NA WATOA MAONI PIA USHAURI WENU KATIKA BLOG HII....

Kwa ajili yenu
Ni furaha kubwa kuweza kuchukua nafasi hii, na kushukuru jambo lolote zuri/jema na pia kuzikubali changamoto zinazotolewa. Leo ningependa kuwashukuruni wote kwa maoni yenu mazuri. Kwa kutembelea blog hii , kweli nasema upendo wenu na mshikamano ni mafanikio makubwa kwa mimi na pia kwenu. Kwani kama wote tujuavyo blog bila maoni hatuwezi kujua mafanikio na mapungufu yake. Kwa hiyo kwa jambo hili napenda KUWASHUKURUNI WOTE, NA NASEMA PAMOJA DAIMA bila kusahahu UPENDO DAIMA!!!!!

9 comments:

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta, tunashukuru sana kwa kutushukuru kwako. Maisha ya kublog ni ya ajabu sana. Nilipoingia katika ulimwengu wa kublog, nimejifunza mambo mengi sana. Ni ulimwengu wa kipekee utoao uhuru wa kueleza fikra zako na kutoa uhuru wa majadiliano juu ya fikra hizo. Mi nasema kublog ndiyo nyenzo sahihi ya mawasiliano.
Hivyo hukuza urafiki miongoni mwetu. Huchochea kuwajibika. Hivyo ni jambo la kawaida kila wasaa unajikuta una deni kwa marafiki/wasomaji wako. Kila mara unafikiria uwajuze kwa lipi.
Kwa mantiki hiyo, kublog kunaongeza sana uwezo wa kufikiria na uelewa wa mambo. Kublog kunakuza roho ya kujitolea. Mtu anafanya utafiti na kisha anautoa blogini pasipo kipato chochote. Ni jambo lenye kujenga mahusiano yenye thamani.
Nimesema mengi, la muhimu ni kukushukuru sana wewe kwa kuingia katika ulimwengu wa kublog.

Chacha o'Wambura said...

umnikumbusha ki-YCS-YCS vile....lol

Anonymous said...

Thanxx dada Yasinta ,Ubarikiwe sana ....Stay showered with blessingz....Cheerz

John Mwaipopo said...

kublogu kama aina fulani ya bangi hivi.

chib said...

Mwaipopo.... DUH!!!

Upepo Mwanana said...

Tunashukuru Da Yasinta kwa kutujali, japo wengine ndio hivyo tena tunapitia mara chache

Mzee wa Changamoto said...

Sijui nani kati yangu na wewe anapaswa kumshukuru mwenzake. Lakini ntapokea shukrani hiyo nikikushukuru kwa kufanya kile ambacho kimenifanya unishukuru.
PamoJAH

Glennis said...

Lovely Iris's did some nice young man give them to you? I hope so.

Yasinta Ngonyani said...

ahsanteni wote. Na mnapendwa wote Upendo daima.