Monday, January 23, 2017

ZILIPENDWA..UNAKUMBUKA HIVI?

FANTA SIO FANTA TU  BALI HAZIKUWA ZIKICHAKACHULIWA
Nakumbuka sana haya makopo vilikuwa na ubora sana hivi vitu, siku hizi duh! kaaazi kwelikweli...sijui  wenzangu mnasemaje?

7 comments:

daileth mbele said...

Dada umenikumbusha mbali sana.Kweli siku hazigandi.Kipindi hicho soda kunywa mpaka sikukuu.I remember my childhood that time in Mbinga

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu Mbele kwanza nachukua nafasi hii kukukaribisha katika kibaraza chetu hiki. KARIBU SANA . Na Ahsante sana kwa mcango wako...Mimi nilikuwa hata siijui soda sikuu ni togwa tu....ukiwa na bahati kama sio ni maji tu.

NN Mhango said...

Hiyo kitu Pride na Super-Ghee ilikuwa kama mana kwa jamaa waaminio katika dini nyemelezi. Nakumbuka sana kitu hiyo hasa kikiwekwa kwenye uji. Wakati ule mikate haikuwa mingi kama sasa. Ukija kwenye soda ndiyo usiseme. Akipewa kitu hiyo mgeni jua ni ima mkwe au mtu maarufu. Kama alivyosema ndugu Mbele: kweli siku hazigandi. Pamoja na umaskini wa taifa letu, siku hizo maisha hayakuwa na pressure kama sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Mmmm kuweka kwenye uji nimependa hiyo....ama kweli siku hazigandi

daileth mbele said...

Asante kwa ukaribisho.Mimi ni mdao wa blog yako kwa miaka mitatu sasa since 2014 but sikuwahi comment anything.But naipenda sana..wakati naanza kuitembelea nilikuwa najisikia niko nyumbani vile nilikuwa na miaka 15 sijaenda nyumbani.Niliondoka katoto nikarudi kijana.Napenda blog yako iko natural sana

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi kusikia hivyo...unazidi kunipa moyo wa kublog Karibu tena na tena.

daileth mbele said...

Asante sana. Kabisa unafanya kazi nzuri.