Thursday, September 3, 2015

SWALI NILILOULIZWA NA MSOMAJI /MFUATILIAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO:-

Swali lenyewe lipo hivi:- Hivi ni  kitu gani akina mama/wanawake kinawafanya wampende mtoto fulani zaidi kati ya watoto wao wa kawazaa?
Akaendelea:- Utamkuta mama ana watoto wanne, lakini anampenda mmoja zaidi ya wengine? Hii inakuwaje kwa upande wako? akanipa hili swali mimi......akaendelea nakuuliza kwa kuwa nadhani una watoto.....halafu akaendelea kusema ....Pia nadhani utakuwa umeshawahi kuisikia hii au inatokea.
Jibu langu lilikuwa kama ifuatavyo:- Binafsi kama mama nawapenda wanangu sawasawa na sijawahi kufikiria  KUWAPENDA  TOFAUTI.
Baadaye nikakumbuka kwanini niwashirikishe ninyi wasomaji/ ndugu zangu. Maana naamini palipo na wengi pana mengi
Hata hivo nami nikajiwa na swali:- Je?  Hiki kitu kipo? na kama kipo kwa akina mama/wanawake tu?  na sio akina baba/wanaume? Maana nao pia ni wazazi. NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA......Kapulya wenu!

2 comments:

Mama Jeremiah said...

Binafsi nawapenda watoto wangu sawasawa. lakini watoto wangu wapo tofauti. Kila mmoja ana kipaji chake, ana vitu anavyovipenda na asivyo vipenda. Kuna vitu anafanya vizuri zaidi ya mwenzake.
Je nawapima watoto wangu katika mzani mmoja? Hapana kwa sababu nikifanya hivyo nitakuwa nakosea. je kuna watu wanaona nampenda A kuliko B? Ndio, kwa sababu anayeona hivyo anatumia mzani mmoja kupima upendo wangu kwa wanangu. Hili swali ni gumu sana kulijibu na pia muulizaji kupata jibu la uhakika kwani huwezi kutumia kipimo kimoja kupima ni jinsi gani mzazi mwenye watoto 2, 3, 4 au 5 anawapenda watoto wake bila kuona kama kuna upendeleo..
Sisi wenyewe tulikuwa tunaonaa mama au baba anampenda fulani zaidi ya sisi wengine.. lakini tulikuwa tunaangalia kitu kimoja tuu...

Yasinta Ngonyani said...

Mama Jeremiah! Ahsante kwa mchango wako ni kweli hili ni swali gumu kidogo kwa sababu huwezi kuchagua mtoto na kama hivyo si afadhali basi kuzaa mtoto mmoja tu utakuwa huna wa kuchagua...