Wednesday, September 23, 2015

HEBU LEO TUANGALIE KICHEKESHO HIKI CHA MZARAMO V/S MCHAGA...KARIBU

Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: "unaumwa nini?"
MCHAGA: "Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa.."
MZARAMO: "sawa, toa laki kabisa.."
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; "Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu.."
MCHAGA akanywa akatema faster; "Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?"
MZARAMO: "Umepona karibu tena.."
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa.."
MZARAMO akamwambia "hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..'
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..'
MZARAMO: "nesi naomba kikopo no.27.."
MCHAGA: "ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?"
MZARAMO: "UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.
PANAPO MAJARIWA TUTAONANA TENA!

4 comments:

Anonymous said...

Kweli Mchaga kawezwa, chezea Mzaramo wewe! Eid Mubarak kwa wote. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ww Mzaramo nini?..LOL..Eid hii naona haijawa nzuri kama tulivyotegemea tuwaombee wenzetu!

NN Mhango said...

Da Yasinta licha ya kuipenda hii umenivunja mbavu hadi machozi yakanitoka jambo ambalo si kawaida kwangu. Shukrani sana na ubarikiwe sana kwa ubunifu wako. AAAMIN

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango...Ni furaha kusikia umevunja mbavu hadi machozi...Nashukuru kwa kuupenda ubunifu huuu pia kuacha lako la moyoni.