Friday, September 4, 2015

MATUNDA NI MUHIMU KWA AFYA ZETU!!

Nimeyatamani kweli machungwa...Niwaambie kitu nilipokuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza na pili. Shuleni kwetu Lundo kulikuwa na miti mingi sana ya matunda mbalimbali mojawapo machungwa...Basi nakuambieni baada ya shule unaaga nyumbani kwenda kuchota maji au kuokota kuni kumbe kula machungwa ya shule...shhhh.:-(.....Ila mmhhh ilikuwa ukikamatwa na mlinzi basi ni viboko tu ...Kaaazi kwelikweli:-) PAMOJA DAIIMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. Kapulya.

3 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Machungwa yenyewe unayotamani mbona mabichi? Ukikumbuka zama hizo unatamani siku zigandishwe au kurejeshwa nyuma lau ufaidi kidogo halafu urejee kwenye maisha yako.

Anonymous said...

Jamani machungwa mnafaidi peke yenu. Na mie kidogo! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! Ndiyyo ni machungwa mabichi...lakini kumbuka kuna mengine yanakuwa ya kijani lakini yameiva na åia kuna wengine wanapenda mabichi...Yaani natamani sana siku zirudi nyuma tena:-)

Kaka Salumu! wala sijakunyima wewe kula na macho:-)