Tuesday, August 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELEA SIJALIMA MBOGA MBOGA TU NIMALIMA NA.......

 Mahindi na sasa yamechanua ila nina wasiwasi kama nitakula maana bado hayajabeba :-)
 Kule kwetu Litumbandyosi tunalima sana Karanga kwa hiyo nikaona niendeleze kilimo..
 Na kulima mboga bila kiungo/pilipili si safi sana na hapa nilijaribu na matokeo yake ni kama muonavyo.
..na bila kusahau nyanya  nazo sasa ndo zinaanza kuiva na tumeshaanza kula...kazi ya mikono yangu/yetu mwenyewe/wenyewe.

10 comments:

Interestedtips said...

Hongera saaana dada yangu. Yaani juhudi ukiwa nazo na matunda yanaonekana

Manka said...

Hongera sana Dada Yasinta,na mimi mwaka nilifuata nyayo zako nimelima mchicha,sukumawiki,kunde,nyanya,hoho na zimestawi sana.

Yasinta Ngonyani said...

Manka nafurahi kusikia haya yote HONGERA SANA...NATAMANI KUINA BUSTANI YAKO...NA HIZO KUNDE NI KUNDE ZA AINA GANI? MAANA KUNA KUNSW ZA AINA NYINGI

Rachel Siwa said...

Huu ndiyo wakati wa kumtembelea dada wa mimi...KADALA...Niwekee na mimi...

Yasinta Ngonyani said...

Mama Alvin ahsante....ni kweli matunda twayaona.....karibu..

KACHIKI...YAANI USIHOFU YAANI HATA KESHO NJOO...

Anonymous said...

Hungera sana dada. Ubarikiwe! By Salumu.

Manka said...

Asante Dada Yangu,sikujua kama kuna kunde tofauti tofauti,mbegu zake ni ndogo kama za choroko ila zina rangi kama brown hivi.Nitakutumia picha uone

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ...ahsante sana na karibu kuja kuvuna.
Manka ndugu yangu nitafurahi kuona hiyo picha ya kunde.

Anonymous said...

Namie mwakani Inshaallah nitapanda.yaani umenifanya nitamani na kujutia muda wangu sama yote hii hata mchicha?Ubarikiwe sana dada yangu.Nafarijika sana kuingia humu.inanipunguzia home sick.
Mama Wane.

Yasinta Ngonyani said...

Mama Wane ...nami unanipa moyo zaidi..nakutakia kila la kheri ndugu yangu!!!