Monday, June 13, 2011

SHUKRANI ZANGU KWA WALEZI/WALIMU

Leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa WALEZI/WALIMU kwa kazi kubwa waifanyayo. Sijui kama wewe mwenzangu umewahi siku moja kufikiria ya kuwa hakuna mlezi/walezi wazuri kama walimu. Fikiria mtoto aanzapo chekechea, unampeleka huko chekechea/”shule ya Vidudu” na wewe mwenyewe unaenda kazini na baadaya ukishamaliza kazi unaenda kumchukua.
Na unakutana mtoto mwenye furaha tele kabisa. Na pia inawezekana baada ya muda mtoto atakuwa kamzoea zaidi mwalimu kuliko hata wewe na mwalimu atamfahamu zaidi mwanao kuliko wewe/mimi mwenyewe.
Nimejaribu kufikiria sana, sisi wazazi jinsi tulivyo na muda mchace sana kuwa na watoto wetu. Je? wewe pia umefikiria hili? Yaani hapa unaweza kusema walimu wa chekechea wao ndio wazazi kamili. NA INAWEZEKANA HATA KUANZA KUTEMBEA NA HATA KUSEMA MANENO YA KWANZA ANAANZIA HUKOHUKO CHEKECHEA.
Kwa kweli mnastahili PONGEZI WALIMU.
Na baada ya miaka ya kuanza shule ifikapo, hapo ndio inakuwa pia mtoto anaondoka asubuhi kwenda shule. Muda wote anakuwa na MWALIMU/WALIMU. Na mwalimu/walimu ndiye/ndio wamleao kwa asilimia kubwa. Kwani anakuwa muda mwingi san ana mtoto /watoto wako/wetu kuliko sisi WAZAZI. Nimejaribu kufikiria kwa mfano mimi mwenyewe binafsi, mara nyingi tunaagana asubuhi na halafu tutaonana tena kesho alasiri nirudipo katika mihangaiko yangu . Na kwa wengine huwa hawakutani kabisa na watoto asubuhi. Kwa vile labda baba au mama anahitajika kuwahi sana kazini, na anaporudi jioni watoto wanakuwa wamelala na kesho yako hivyo hivyo huondoka kabla watoto hawajaamka.


Kwa hiyo mimi kama mzazi napenda kutoa shukrani zangu kwa WALEZI/WALIMU WOTE KWA KAZI NZURI MUIFANYAYO. MAANA MNASTAHILI KWA KWELI. AHSANTENI SANA!!!!

7 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Sisi tuko hivi hapa mtandaoni kutokana na kazi njema za walimu wetu. Kweli mwalimu ni mzazi!

Anonymous said...

Kwa kauzoefu kangu,juu ya hawa waalimu,naweza kusema ni wachache sana ambao unaweza uka kaa chini na kusema bila mwalimu fulani nisingekuwa hapa.kwa mfumo wetu wa elimu ya Tanzania, kwangu mimi mchango wa mwalimu nikiasi kidogo,zaidi ya mikwara,vitisho,kukatishwa tamaa,nakuonekana mjinga katika kuwepo kwako hasa unapokuwa napokea mafunzo yao(elimu ya darasani).Labda walimu wa zamani enzi za mkoloni,lakini siyo hawa wa baada ya uhuru nahasa wale wa kipindi cha ' mido skuli' darasa la nne na darasa lanane zamani hawa wlikuwa namahusiano ya karibu kati ya mwanafunzi na mwalimu,hivyo ualimu ulikuwa kama wito.walimu wa sasa amboao wamenifundisha mimi hapana ,nakataa siwapi asilimia miakwamia tumeshirikiana mimi nawao kufika hapa,na hasa ni juhudi za mwana wanafunzi binafsi.wao kama walimu wame timiza wajibu, lakini nafasi kubwa ya kuweza kublong siyo wao.anyway ila pia neno lenyewe waalimu ukienda kwaundani nipana mmno,unapo amua kumshukuru,labda yeye ndo akushukuru wewe nimawazo yangu tu au ni kwanini mwalimu anakuwa mkali unapo shindwa kuandika sentensi ubaoni? je kosa nilako au ni la mwalimu? anauhakika gani kuwa alicho kufundisha umekielewa,je wewe binafusi kama mwanafunzi mchango wako niupi katika kuelewa elimu hiyo upewayo na mwalimu.Inazidi kuwa ngumu pale pia unapo muona mwalimu huyo kama mzazi,hivyo apewe shukrani? sijuwi! Kaka S.

John Mwaipopo said...

ya kwangu imekaa hivi:

juzi katika tembea tembea zangu hapa mbeya nimemuona mtu mmoja ambaye kipindi nasoma mbeya day nilimuona wa kawaida. huyu mjamaa, sasa umri umekwenda kiasi (late 40s may be), alikuwa dereva wa daladala moja tuliipanda sana kwa kipindi chote cha miaka mi4. kwa wakati ule nilimchkulia mtu wa kawaida tu. lakini nilipoluona juzi kuna wazo lilinijia.NA YEYE NADHANI ANA NAFASI YAKE KATIKA MAFANIKIO YANGU, haya haya niliyoyafikia.ingekuwaje kama siku moja kwa ulevi tu angaliingiza Leyland lile mtoni/darajani

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa mchango wenu..Kaka S! ndio maana kuna kutoa maoni kwani kila mtu ana mtazamo wake katika vitu mbalimbali pia hata chakula..kwa hiyo nakuelewa kakangu.

Goodman Manyanya Phiri said...

@Anonymous

Nimeasoma masikitiko na manung'uniko (kama ni Kiswahili sanifu) yako na nimesikitika.


Mtoto hana ule uwezo wa kumwona mwalimu mbaya kwa mzuri. Sasa kama wewe hapo unaweza kuwatenga walimu wako kwa wabaya kwa wazuri, inamaana hali ni mbaya sana katika ualimu siku hizi!


Kama unaoyasema ni ukweli, suluhisho ni nini?


Labda Wizara za Elimu barani zianzishe maoni (SUGGESTION BOXES) kwa wanafunzi juu ya walimu wao, kusudi wale wababaishaji wafukuzwe kazi papo hapo wasipopendea na watoto! Mnaonaje, Wenzangu?


Maana yake tumechoka sana na walimu wanaovunja mioyo za watoto, wanaopanda watoto kama wake zao au malaya hivi; walimu wenye uvivu, na kadhalika.

Pamoja na hayo, lazima tuwatukuze na kuwapa hongera walimu wazuri; na kila mmoja wetu aliewahi kwenda shuleni anaweza kuwataja kwa majina hao walimu wazuri!

ray njau said...

Makala yako imegusa sana moyo wangu kutokana na ukweli wake.
Mke wangu ni mwalimu wa chekechekea.Ugumu wa kufundisha/kulea watoto wa chekechekea si kupata maelezo yake kwa haraka.
Swali kwa wadau:
JE MAISHA UNAWEZA KUYAELEZEA MAISHA BILA WALIMU?

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec