Wednesday, June 8, 2011

MSAADA: RENATHA BENEDICTO ANATAFUTWA NA FAMILIA YA MUBELWA BANDIO!!!

Hapa ni bibi na bwana Bandio


Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu. Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html)

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio. Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.
Email yangu ni changamoto@gmail.com

NATANGULIZA SHUKRANI

http://www.changamotoyetu.blogspot.com/
http://www.youtube.com/user/mutwiba

5 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Renatha ni malaika yule! Katenda wema na kuondoka zake. Vilevile shukrani haidai kwa mtu yoyote.


Tunaweza Nduguzanguni kuwatafuta wale waliotufanyia mema ili tuwapongeze au tuwashukuru. Ukweli lakini ni kwamba kwao malaika hatudaiwi lolote kwa msaada wao; bali tunadaiwa kutoa shukrani zetu kwa Mungu hapo tulipo kwa wakati wa sasa kwa kusaidia nasi viumbe Vyake viliokuwa karibu nasi.

Anonymous said...

Manyanya, Umenena sana maneno yako ya uchaji sana tena unaonyesha ni msomaji wa Biblia.Usitafute kumsaidia yule aliyekusaidia kwa sababu Mungu anao wengi wa kuwafanyia wema kama uliofanyiwa wewe nawe katende hivyohivyo kwa wengine.

Kumbuka habari za Msamaria mwema.Mtolee mungu shukrani hapo ulipo kama Manyanya alivyokushauri.lakini kama kweli unaweza kuoanana naye ana kwa ana neno la shukrani halisiti na hata kumpa unachompa lakini isiwe kwamba unataka lazima umpate yeye tu.

Mzee wa Changamoto said...

Nawashukuru wote kwa ushauru na BUSARA.
Ni kweli kuwa TENDA WEMA UENDE ZAKO. Na niliposimulia hili kwa mara ya kwanza niliambiwa NI MALIPO YA FADHILA AMBAZO UMEKUWA UKITOA.
Lakini mimi simtafuti ili KUMLIPA FADHILA, ila nafsi yangu yanifanya nimsake na niendeleze mawasiliano.
Labda ni kwa kuwa hatujui mwisho wa njia tunayopitishwa, lakini yawezekana kuwa Mungu alimuwezesha kufanya aliyonifanyia kwa kuwa alijua kuwa kupitia yeye, kupitia nduguye ama ndugu yangu ama yeyote mwenye uhusiano baina yetu, kuna jingine jema zaidi, lenye kugusa wengi zaidi, kwa namna nzuri zaidi na kwa manufaa ya wengi zaidi linaweza kutokea. Sipendi ku-limit mipango myema ambayo MUNGU anaweza kuwa kaiweka mbele yetu
Lakini kwangu, bado naamini ni vema kumtafuta na kuendelea kuwasiliana naye. JAPO HILO
Na hata kwa malaika, haimaanishi kuwa hakuna haja ya kuwatafuta na kuthamini walichotenda kwetu.
Na ndio maana, licha ya kuwa kwa miaka 12 nimekuwa namkukumbuka, namuombea na kumtakia KILA LILILO JEMA, bado naamini nitafurahi zaidi kuendeleza mawasiliano naye.
NAWASHUKURUNI SANA WANDUGU

Goodman Manyanya Phiri said...

Mimi kwa upande wangu nimekuelewa, Mkuu. Na asante kwa kutuonyesha roho yako kama ilivyo. YATAKA MOYO!


Naamini utampata huyo. Na ukimkuta kichaa, na amini pia moyo wako uko tayari kumuuguza mpaka apone.


Kila siku na zidi kufurahia kukaa kwangu mtandaoni na watu kama wewe: hatuwazi sawa wala hatuna maadili sawa, lakini tunaelewana na tunatoleana fundisho ili dunia yetu iwe yenye furaha.


Jamaani wote, tutafute namna ya kuonyesha shukrani kwa vitendo na siyo kwa neno "shukrani" tu!

Ndugu yetu, Mzee Wa Changamoto ametupatia mfano wa kuigwa!!

Je, uliwahi kwendea shule zako za msingi na sekondari kutoa shukrani? Uliwaachia shilingi ngapi? Sema basi!!!


Je, bibi yako aliekulea na babu unawakumbukaje? Si wamekulea baada ya mama yako kukutelekeza?

Je huyo mama aliyemsaidia mama yako kukuzaa (MIDWIFE) unamshukuru kivipi? Si ungedondoka chini na kupasuka kichwa bila yeye kuwepo na kumsaidia mama yako kwa wakati wa kukuzaa wewe?

emu-three said...

Kuna usemi wa kiimani usemaoo `mvunjuka udugu hatauona ufalme wa mbinguni, sijui niliupata wapi, basi weye unayetafutwa kama utabahatiska kupita hapa au kusikia tangazo hili wasiliana na anayekutafuta, mkuu wa changamoto...utakuwa umeunganisha udugu na wale wanaojua yupo wapi wamfahamishe, watakuwa wameunganisha udugu...TUPO PAMOJA!