Wednesday, June 22, 2011

MBUGA YETU YA WANYAMA MIKUMI TANZANIA: UZURI WA NCHI YETU...NATEGEMEA KUPITA HAPA KARIBUNI:-)



TUTAONANA TENA BAADA YA MUDA... KILA LA KHERI

11 comments:

Rachel Siwa said...

Tunakutakia safari njema yenye amani na utulivu, Mungu awe nanyi daima.Naona umeamua kufanya utalii wa ndani inapendeza!!!

raynjau said...

Nakutakia safari njema na uwape salamu zangu zifike Songea na vitongoji vyake lakini usisahau kuwa Saadan ni mbuga inayokutana na Bahari "A bush meet a Beach" mbuga ambayo inapacha za mito miwili ya Wami na Ruvu inayomwaga maji katika Bahari ya Hindi na ambayo samaki aina ya kasa hutaga kati ya nchi za Pwani ya Mashariki ya mbali na Pwani ya Bagamoyo, ni Saadan ambayo Bushiri Bin Salim chotara wa Ki-Oman na Kiafrika alipigana na Wajerumani akipinga kutawaliwa hadi alipokamatwa na kunyongwa hadharani mwaka 1889. Saadan ina baadhi ya wanyama ambao hawapatikani katika mbuga nyingine Tanzania na Duniani.Twiga wenye mabaka meupe na meusi na mbega wekundu wanaonekana Saadan tu.

Mbele said...

Nami ninaelekea TZ katikati ya mwezi ujao. Nitazunguka hadi nyumbani Ruvuma, nikatue Mbamba Bay pia. Labda tutaweza kukutana. Tuwasiliane.

Mwanasosholojia said...

Mmmh, Da'Yasinta unanipa hamu ya nyumbani!Safari njema na salamu kwa wote!

John Mwaipopo said...

afadhali utapita mikumi kwa gari maana yale mambo ya ndege ya songea na nyie wangoni mnavyofahamika kwa kucheza ngoma mbona kungekuwa hapatoshi ndegeni.

karibu tanzania

chib said...

Safi sana, ukifika huko utujulishe tutandaze zulia jekundu. Nami nataraji kuwa nyumbani hivi karibuni, japo kwenda kwangu huko ni sawa na mtu anapoamua kupanda daladala, kwani haitaji kujipanga

Koero Mkundi said...

@Ray Njau.......
Ukiajiriwa wizara ya Utalii utatusaidia sana kututangaza maana umechambua vivutio vyetu kiasi kwamba hata mie umenifanya niwaze kwenda huko Saadani.....

Da Yasinta nakutakia safari njema, Kwa sasa napiga misele ya kiujasiriamali huku Mkoani Tanga, lakini nitarejea siku si nyingi na nitajitahidi tuonane uso kwa uso....LOL

Ebou's said...

Safi sana kwa future ukipita piga picha sana, utuwekee kwa blog!

Simon Kitururu said...

Safari njema Yasinta!

raynjawa said...

"JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI"[SALAMU KWA WAZAZI NA WADAU WOTE MKOANI RUVUMA]
-------------------------------
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa michache ambayo uoto wake wa asili haujaharibiwa. Jitihada zinaendelea kufanyika kulinda uoto huu usiweze kuharibiwa kutokana na shughuli za wanadamu.

Eneo la misitu iliyohifadhiwa ni kilometa za mraba 7,128. kati ya eneo hilo kilometa za mraba 6,958 ni hifadhi za Taifa na 170 ni hifadhi za Halmashauri. Eneo lililohifadhiwa ni asilimia 11 ya eneo la Mkoa. Maeneo mengine yapo katika mchakato wa kutengwa kama hifadhi za vijiji na Halmashauri chini ya Mradi Maalum wa Misitu Shirikishi Jamii (Participatory Forest Management) ulioanza katika mwaka wa fedha 2005/2006. Maeneo hayo pia yanahusisha vyanzo vya maji.

Katika kuyarudishia hali yake ya asili maeneo yaliyoachwa wazi baada ya kukatwa miti, katika mwaka 2006/2007 imepandwa miti 6,000 katika eneo la hekta 3,824. Miti iliyopandwa ni Migwina, Minyenda na miti ya matunda.

raynjawa said...

Mipango ya maendeleo Mkoa na Halmashauri katika Mkoa wa Ruvuma inazingatia Jinsia. Mipango ya maendeleo mkoani inashirikisha wanawake na wanaume kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.

Haya ndiyo mambo ya mkoani Ruvuma nyumbani kwa Yasinta Ngonyani.
-----------------------------------
Katika upangaji wa mipango ya maendeleo ya Mkoa na Halmashauri tunatumia mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD). Mfumo huu unawezesha wanawake na wanaume kushiriki katika hatua za kuandaa mipango shirikishi jamii. Unatumia zana shirikishi kutambua fursa na vikwazo vilivyopo ndani na nje ya jamii husika. Kisha, jamii inatafuta njia za ufumbuzi na kuweka vipaumbele vya mipango ya maendeleo ya vijiji/kata na wilaya, inayolenga kutekeleza Dira ya Taifa ya maendeleo 2025, kama mwongozo wa kisera wa jumla na hivyo kuwa msingi wa utekelezaji wa mkakati wa kuondoa umasikini.

Katika Mkoa wa Ruvuma, miradi mbalimbali inaibuliwa katika ngazi za vijiji kwa kutumia mfumo shirikishi jamii, miradi hiyo inakwenda kujadiliwa na kupitishwa katika ngazi ya kata katika kikao cha maendeleo ya kata. Kutoka ngazi ya kata miradi ya maendeleo inapelekwa katika ngazi ya Halmashauri kwa kujadiliwa na kupitishwa katika kikao cha madiwani cha Halmashauri. Miradi ya maendeleo ikipitisha katika kikao cha madiwani cha Halmashauri, miradi hiyo inapelekwa katika ngazi ya mkoa ambapo inajadiliwa na kupitishwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa na hatimae kupelekwa Bungeni.

Aidha katika Halmashauri kuna mfumo wa ukusanyaji wa takwimu unao zingatia masuala ya jinsia. Mfumo huo unakusanya takwimu za kila sekta na baada ya kupata takwimu hizo ndizo zinatumika katika kupanga baadhi ya mipango ya maendeleo. Mfumo huo unafahamika kwa jina la "Local Government Monitoring Data base (LGMD).