Monday, December 21, 2009

JAMANI MWENZENU JUZI NIMEONA MIUJIZA

Rafiki yangu mpya!
Kublog ni kuzuri sana maana kama wewe ni mtu wa kublog, basi kila unalokutana nalo katika mizunguko yako ya kawaida linakuvutia kuwashirikisha wasomaji na wanablog wenzako. Mimi huwa napenda sana kufikirisha upande wa pili katika kutafakari ili kujua kama niwazavyo mimi ni sawa na wezangu.

Nina kamkasa kadogo hapa ambako sio ka kawaida kalinitokea jana kakanivutia sana au niseme kaliifanya siku yangu ya jana kuwa ya kipekee…Jamani sio kwamba nimeokota almasia au dhahabu, la hasha. ngoja nisipoteze muda niwasimulie kisa kilichoifanya siku yangu ya jana kuwa ya pekee.

Juzi wakati nasubiri basi kwenye kituo cha basi kwa safari ya kwenda kusuka, mara akaja bibi mmoja,. Nikamsalimia akajibu kwa bashasha, nikashangaa sana kwani sio kawaida hapa, kumsalimia mtu usiyefahamiana naye akakuitikia tena kwa bashasha. Bibi yule hakuishia hapo, nikawa nimepata rafiki tukawa tunaongea mengi sana kuhusu maisha na kama kawaida hali ya hewa, maana huku hali ya hewa ni ya baridi mtindo mmoja, kila mahali ni theluji tu.

Yule bibi alionekana kunifurahia sana mpaka nikashangaa, maana tulikuwa tunaongea kama marafiki tuliofahamiana siku nyingi...ajabu eee!!!!

Najua wengi mtashangaa kwa nini nazungumzia jambo hili. Nimelizungumzia jambo hili kwa sababu hapa Sweden watu hawana ukaribu kama ilivyo huko nyumbani yaani Tanzania. Hapa watu wakiwa kwenye vituo vya mabasi wakingoja basi hawazungumzi na wala hawasalimiani. Sio kama nyumbani watu mnaweza kukutana kwenye kituo cha basi au kwenye basi na mkaanza kuzungumza kwa bashasha na kuzoeana na wakati mwingine mkajenga urafiki na hata kupeana namba za simu.

Huku hali haiko hivyo, eti umsemeshe mtu mmekutana tu kituo cha basi au kwenye mighahawa, mahospitalini au hata kwenye mikusanyiko isiyo rasmi….thubutuuu, mtu atakuangalia na asikujibu kitu.

Halafu hapa hata kukaa kwenye siti ndani ya basi watu wanakaaa kama mmoja mmoja hawakai pamoja na ukiingia wewe uliyezoea kuongea kama Kapulya mdadisi basi inakuwa shida kweli. Kukaa kama bubu safari nzima bila kuongea kazi kwelikweli.

Kuna mambo ambayo huenda angalau ukapata msaada kwa watu hawa, kwa mfano kama umepotea unaweza kusaidiwa tena utajibiwa kwa swali ulilouliza tu na hakuna blah blah zaidi au kama umepata matataizo ya kiafya na unahitaji masaada wa haraka kupelekwa hospitali, anaweza kujitokeza mtu akapiga simu kuita gari la wagonjwa au kama wakipata namba za simu za ndugu zako watawapigia kuwajulisha basi hakuna msaada zaidi ya huo.

Je mmeona ni kwa nini nilivutiwa sana na yule bibi? Ni kwa sababu nilijihisi niko nyumbani, na nilihisi kupendwa na mtu baki nje ya familia yangu.

Basi mwenzenu nilifurahi kweli nilijisikia nipo nyumbani ambako ni kawaida kuongea na kumsalimia kila mtu. Na hii Christmas wenzangu wee nilihisi niko Ruhuwiko kabisaaa…ama kweli bibi yule sijui ni muujiza au ni bahati.

Basi mwenzenu jana nilipata rafiki au niseme nimeona miujiza.

17 comments:

MARKUS MPANGALA said...

NITABAKI AFRIKA YANGU, NIMEJIFUNZA TAMADUNI TANGU ENZI ZA KUISHI NA WAJERUMANI

Mija Shija Sayi said...

Yasinta basi huko ni tofauti sana na uholanzi, waholanzi ni wepesi sana kwa maongezi hasa kwenye mabasi na usiombe kukaa na bibi kwenye basi ujue safari yote ni stori tu, kasheshe kama umechoka.

Huyo kwenye picha ndo bibi mwenyewe nini?

Yasinta Ngonyani said...

Markus Afrika ni ya wote yangu pia. Wenga gandayi ulolayi.

Da Mija kumbe unaishi Uholanzi? basi kama huko ni hivyo mwenzangu huna haja ya kutamanitamani nyumbani. Ndiyo huyo ndiye bibi mwenyewe (rafiki yangu)

malkiory said...

Wafini ndiyo mwisho wa safari, wako baridi kama winter yao ilivyo. Ni kweli kabisa alivyosama Mija hapo juu.Wakati nasafiri na KLM kwa summer holiday nilipatwa na mshtuku kuona nasemeshwa na mzungu niliyekaa naye kiti kimoja, baada ya kufahamiana nikagundua kuwa wadachi ni damu moto kwa maana ya kuwa ni wasemaji hata kwa foreigners. Nilipatwa na msituko kwani kwa kwetu huku hilo ni jambo ambalo haliwezi tokea katika hali ya kawaida, unless wamelewa pombe.

Faith S Hilary said...

Kweli ni miujiza maana a friend of mine back in Germany, alikuwa anataka kumuuliza bibi mmoja where the pharmacy was ila yule bibi akaishia kupiga kelele eti huyu rafiki yangu anataka kumuibia pochi yake. Kapiga kelele mpaka watu wengine wakatokea, kumbe binti wa watu alitaka kujua pharmacy iko wapi. Kwahiyo naona ni miujiza kweli (it doesn't apply much here in the UK but it depends where you live) huyo bibi kakuchangamkia maana wengine ndio wanafyatuka kama hivyo...

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

yawezekana pia akawa anataka umtafutie boyfriend wa kiafrika, ama!!!

ni vijimambo tu....lol

John Mwaipopo said...

sasa mliongea kingoni, kiswahili, kiswidi au kizungu. ha! ha! ha!

sekretari wangu ananiambia ni kiswidi kama ni kweli kusema na kuandika 'ugonile' kwa kiswidi kukoje? alafu unamjibuje?

sina sekretari msiogope

Anonymous said...

ulipona kwa bahati mbaya wewe, utakufa tu. subilia uone

chib said...

Huyo bibi alikupa picha yake au....

Serina said...

Karibu västragotaland basi...huku ubaridi umepungua kiasi :)

Unknown said...

Naomba niwe mtabiri: dada Yasinta hii inaashiria kuwa sikukuu hii ya X-Mas itakuwa njema kwako na familia yako. Hongera kwa muujiza

Koero Mkundi said...

Kuna uwezekano huyo bibi ni Mngoni wa uhuwiko....LOL
Dada kwa kweli nakuonea huruma kumbe uko kwenye nchi ya ajabu hivyo, jamani hata kusalimiana ni shida.
Duh! ama kweli huyo bibi ni mtu wa pekee. Naomba umfikishie salaam zangu.

Anonymous said...

Mi nafikiri ni whole europe kuwa watu huwa hawaongeleshani pasipo na umuhimu, ila mara nyingi wazee ni wachangamfu sana. UK watu hawaongei especially london ila ukiuliza utajibiwa bila matatizo. Holland ndio usiseme, watu ni wachangamfu sana. Sweden niliwahi kuja kutembea na nilikuwa pale Alander airport na nilimake very good conversation na mswidi kwani mwenyeji wangu alichelewa kuja kunipokea. Kwa ufupi sidhani kama its that bad unless sijui inakuwaje maana naona kuna watu wameshaanza kuogopa kuja europe lol!! Ukiwa na bahati mbaya sana ndio unakutana na wajinga wenye frustrations zao ndio wanakujibu vibaya, lakini si wazungu wote. Kila mahali kuna kind people na useless ones. Merry xmas dada

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

kwa kweli sintoshangaa kwa kuwa huko ughibuni vizee hukosa matunzo na hata mtu wa kuzungumza naye na kufikia kujenga urafiki na nyau na bobi....lol

una bahati umepata rafiki na hivo nyote kwa kuwa mna kiu ya kupata mtu wa kuteta naye JUST GO ON....

Yasinta Ngonyani said...

Jamani sio siri waswid ni baridi sana huwa nawalazimisha kuongea. Ila huwa wananiangalia na kufikiri mimi ni punguani pia wanaona kama nawasumbua tu. Naamini huyu bibi alikuwa kweli ni muujiza na nategemea kama alivyosema kaka kaluse Krismasi hii itakuwa njema kwangu na familia yangu. Kuna ule msemo usemao ukikuta wenyeji wanatembea uchi nawe fanya hivyo. Hili limenishinda siwezi kabisa na huu UKAPULYA nilio nao DUH! kazi kwelikweli. Upendo Daima na Tutafika tuu! Nachukua nafasi hii kuwashukuru wote kwa maoni na wala msiogope kuja Sweden.

Sisulu said...

haya haya yasinta!

Unknown said...

haha hongera yako,nakumbuka niliandika kitu kama hiki pia kwenye kibaraza changu.Sisi hatuna uzoefu wakuwa mabubu kama hawa wenzetu walivyo..siku hizi nimeanza wapatia..nawaongelesha na wasipo jibu huwa nawauliza kwanini hawajibu:):)