Sunday, January 19, 2020

KUMBUKUMBU:- JUMAPILI HII YA TATU TANGU MWAKA UANZE NIMETAMANI SANA CHAKULA NINACHOKIPENDA NA KILICHONIKUZA


Chakula nikipendacho chaitwa likungu hupatikana hasa kando kando ya ziwa  nimekula sana wakati naishi ziwa nyasa 

na hapa ni kumbikumbi  kama hujaonja basi jitahidi uonje ni watamu sana

Friday, January 10, 2020

HIZI PICHA NIMETUMIWA NA KAKA YANGU AISHIYE ZANZIBAR HAPA NI MAKAZI YAKE MAPYA YAANI MPAKA RAHA

Angalia mapapai yalivyojipanga.....  
...na muda si mrefu ndizi zitakuwa tayari kwa kuliwa ...ukiangalia kwa mbali hapo ardhini utaona aina za ambogamboga...aahhh mate yanachuruzika
na  hapa ni baadhi ya mahindi na mbogamboga tena
ooohh hapa nimekumbuka Matetereka.....Magimbi...hii ndo mtu unaweza ukaiita kazi ya mikono binafsi ila walaji tupo wengu. Tupo njiani;.)

Monday, January 6, 2020

JANA JUMAPILI 5/1 ILIKUWA KUMBUKUMBU YANGU YA KUZALIWA...NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNILINDA NA KUUONA MWAKA MWINGINE TENA!

 Jana tarehe 5/1/2020 mdada huyu ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Na hapa ni zawadi alizozawadiwa na famili pia marafiki zake. Bila kusahau kikombe cha chai 
Kwa vile ni msimu wa baridi nimepata zawadi ya kofia pia...
Muda wa chakula ulipofika...kwanza ni  LOBSTER  ambayo ina viungu vya asili na kitunguu saumu



Na mlo mkuu ulikuwa ni chakula kikuu cha KAPULYA ni SAMAKI ...kwa viazi  maalumu.
NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA YOTE .

Friday, December 27, 2019

SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!

Habari zenu jamani!!
Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2019 na kuingia katika mwaka mpya 2020. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2020 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA KISICHOWEZEKANA. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!

Thursday, November 28, 2019

NENO LA LEO ALHAMISI YA 28/11/2019

USIRUHUSU HOFU YA KUSHINDWA IKAWA KUBWA ZAIDI YA SHAUKU YA KUSHINDA
Hii nimeipata kwa kaka yangu Shabani Kaluse.
Ahsante!

Wednesday, November 27, 2019

UKIFIKA ZANZIBAR PAJE USIKOSE KUFIKA HAPA KWETU UFWUKE.....

....Maana kuna pizza  tamu sana  ni kwamba huwezi kupata sehemu nyingine karibu sana sana
.... na hapa ni PWEZA ( OCTOPUS)  kwa chips

Monday, November 18, 2019

HAPA NI KWETU UFUKWE RESTAURANG IPO ZANZIBAR PAJE USIKOSE KUFIKA....

....maana kuna chakula kitamu sana hasa  pizza karibuni sana sana  na kwa sasa ndo msimu mpya unaanza....ukitaka mawasiliana andika hapa utapata.

Wednesday, November 6, 2019

SASA NI MSIMU WA MASUKU....ILA ULAPO KUWA MWANGALIFU USIJE UKALA NA WADUDU

Masuku ni matunda pori na kwa sasa ni msimu wake nimeyatamani sana sana....sisi wangoni  twaita mapotopoto.

Monday, October 28, 2019

AINA MBALIMBALI YA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NA UDONGO WA MFINYANZI



Soko la vyungu vya asili vinavyotokana na udongo wa mfinyanzi. Si rahisi hasa kwa vijana wetu waliokulia mjini kufahamu umuhimu wa vyungu hivi. Kwani vijana wa zamani tunakumbuka jinsi mama zetu, shaangazi zetu na bibi wazaa mama au baba jinsi walivyotumia vyungu hivi kupikia na jinsi chakula kilichotoka humo kilivyokuwa na ladha na utamu wa aina yake. Lakini pi tunakumbuka jinsi ambavyo vyungu hivi vilitumika kama jokofu. Kwa kuweka chungu kilichojaa maji juu ya mafiga matatu, na kuweka mchanga chini ya chungu na kunyunyizia maji mchanga huo, maji yalikua yakipoa na kuwa ya baridi kana kwamba yametoka kwenye jokofu.

Sunday, October 13, 2019

VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA...SAMAKI NA VYOTE VYA ASILI HASA VYA KUPIKIA KWENYE VYUNGU

 Ni aina ya samaki kama hujaonja jaribu
Na hapa ni vyakula mbalimbali  vya asili viöivyopikwa kwenye vyungu utamu wake ni ngumu kuelezea  bora uonje mwenyewe.

Tuesday, October 1, 2019

LEO NILIKWENDA MSTUNIKUCHUMA UYOGA ...

Msimu ni ule majira ya kupukutika kwa majani. Kwa hiyo ni msimu wa uyoga pia kwa hiyo wapenzi wa uyoga tunafurahia sana kwenda mstuni na kuchuma/kutafuta uyoga. Kumbuka uwapo msituni sio unachuma uchoga tu ...La hasha ni mazoezi makubwa sana na pia  kama ulikuwa na msongo wa mawazo basi msitu ni sehemu nzuri sana na kuwa.
Nawatakieni kila la kheri  tuonane tena panapo majaliwa.....kapulya wenu!

Friday, September 27, 2019

VAZI LA IJUMAA YA LEO....IJUMAA NJEMA!

Mdada bado anapenda mkanda ebu meangalie....IJUMAA NJEMA

Wednesday, September 4, 2019

KILA MTU ALIMAPO ANATEGEMEA KUVUNA CHOCHOTE:- NAMI LEO NIMEVUNA NILICHOPANDA VIAZI

Nimevuna nichopanda ni viazi  matosani au wengine huviita viazi ulaya  katika kundi hilo la viazi 
...kumetokea kiazi cha umbo kama  la  moyo  angalia  mwenyewe

Friday, August 23, 2019

KAZI YA MIKONO YANGU....BUSTANI

Hapa ni zao la zabibu
Na hapa nimepanda mchicha na figiri ila nimechelewa kidogo. Lakini nina matumaini nitakula tu:-)

Wednesday, August 7, 2019

UFUKWE RESTRAND:- UKIWA ZANZIBAR USIKOSE KULA HAPA KUNA CHAKULA KITAMU

Hapa ni baadhi ya wafanyakazi wetu
...na hapa ni kundi nzima
Meneja, akiwa na baadhi ya wafanyakazi kama vile mpishi na  dada msaidizi wake

Monday, August 5, 2019

NYUMBANI NI NYUMBANI NA UFIKAPO NYUMBANI NI RAHA SANA KUONANA NA NDUGU


 Hapa nipo Lundusi na mama zangu yaani binamu zake baba yangu
 Na hapa nipo na dada yangu Anastasia  alikuja kunisalimia baada ya miaka 20 kupita bila kuonana
 Hapa tupo Mkurumo kwa mjomba wetu...mpiga picha ni mimi kapulya
 Hapa tulipata mgeni anaitwa Chacha  alikuja kututembelea  ilikuwa ni furaha sana.

 Hapa tulipata wasaa kuwatembelea mapadre na kupata chakula cha jioni...
Zanzibar Forodhani 24/7-19

Saturday, July 27, 2019

DAFU ZA ZANZIBAR. ..USIKOSE

 Nilifurahi sana hii siku kukaribishwa kwa mtindo huu...
Nsio mimi tu niliyefurahia..
.

Sunday, July 21, 2019

Sunday, July 14, 2019

NIMEPITA SOKONI SONGEA NIKAKUTANA NA VYAKULA NIVIPENDAVYO SAMAKI MBELELE NA LIKUNGU NILI

Hapa ni samaki aina ya mbelele watamu sana sana ila wana miba ndogo  ndogo ulapo yabudi uwe mwangalifu sana...

 Hapa ni likungu...hupatikana sana ziwa nyasa....na sasa ndio msimu wake

Wednesday, July 10, 2019

Saturday, July 6, 2019

PALE UFIKAPO NYUMBANI NA KUPOKELEWA KIASILI ...TWACHAGUA MCHELE

Ni furaha  ilioje kujumuika na familia na kufanya kazi  za jikoni pamoja....nyumbani  Songea/Ruhuwiko.