![]() |
| Chakula nikipendacho chaitwa likungu hupatikana hasa kando kando ya ziwa nimekula sana wakati naishi ziwa nyasa
na hapa ni kumbikumbi kama hujaonja basi jitahidi uonje ni watamu sana
|
Sunday, January 19, 2020
KUMBUKUMBU:- JUMAPILI HII YA TATU TANGU MWAKA UANZE NIMETAMANI SANA CHAKULA NINACHOKIPENDA NA KILICHONIKUZA
Friday, January 10, 2020
HIZI PICHA NIMETUMIWA NA KAKA YANGU AISHIYE ZANZIBAR HAPA NI MAKAZI YAKE MAPYA YAANI MPAKA RAHA
Angalia mapapai yalivyojipanga.....
...na muda si mrefu ndizi zitakuwa tayari kwa kuliwa ...ukiangalia kwa mbali hapo ardhini utaona aina za ambogamboga...aahhh mate yanachuruzika
na hapa ni baadhi ya mahindi na mbogamboga tena
ooohh hapa nimekumbuka Matetereka.....Magimbi...hii ndo mtu unaweza ukaiita kazi ya mikono binafsi ila walaji tupo wengu. Tupo njiani;.)Monday, January 6, 2020
JANA JUMAPILI 5/1 ILIKUWA KUMBUKUMBU YANGU YA KUZALIWA...NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNILINDA NA KUUONA MWAKA MWINGINE TENA!
Jana tarehe 5/1/2020 mdada huyu ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Muda wa chakula ulipofika...kwanza ni LOBSTER ambayo ina viungu vya asili na kitunguu saumu
Na hapa ni zawadi alizozawadiwa na famili pia marafiki zake. Bila kusahau kikombe cha chai
Kwa vile ni msimu wa baridi nimepata zawadi ya kofia pia...Muda wa chakula ulipofika...kwanza ni LOBSTER ambayo ina viungu vya asili na kitunguu saumu
Na mlo mkuu ulikuwa ni chakula kikuu cha KAPULYA ni SAMAKI ...kwa viazi maalumu.
NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA YOTE .
Friday, December 27, 2019
SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!
Habari zenu jamani!!Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2019 na kuingia katika mwaka mpya 2020. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2020 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA KISICHOWEZEKANA. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!
Friday, December 13, 2019
Thursday, November 28, 2019
NENO LA LEO ALHAMISI YA 28/11/2019
USIRUHUSU HOFU YA KUSHINDWA IKAWA KUBWA ZAIDI YA SHAUKU YA KUSHINDA
Hii nimeipata kwa kaka yangu Shabani Kaluse.
Ahsante!
Hii nimeipata kwa kaka yangu Shabani Kaluse.
Ahsante!
Wednesday, November 27, 2019
UKIFIKA ZANZIBAR PAJE USIKOSE KUFIKA HAPA KWETU UFWUKE.....
....Maana kuna pizza tamu sana ni kwamba huwezi kupata sehemu nyingine karibu sana sana
.... na hapa ni PWEZA ( OCTOPUS) kwa chips
Monday, November 18, 2019
HAPA NI KWETU UFUKWE RESTAURANG IPO ZANZIBAR PAJE USIKOSE KUFIKA....
....maana kuna chakula kitamu sana hasa pizza karibuni sana sana na kwa sasa ndo msimu mpya unaanza....ukitaka mawasiliana andika hapa utapata.
Friday, November 15, 2019
Wednesday, November 6, 2019
SASA NI MSIMU WA MASUKU....ILA ULAPO KUWA MWANGALIFU USIJE UKALA NA WADUDU
Masuku ni matunda pori na kwa sasa ni msimu wake nimeyatamani sana sana....sisi wangoni twaita mapotopoto.
Monday, October 28, 2019
AINA MBALIMBALI YA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NA UDONGO WA MFINYANZI
Sunday, October 13, 2019
VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA...SAMAKI NA VYOTE VYA ASILI HASA VYA KUPIKIA KWENYE VYUNGU
Ni aina ya samaki kama hujaonja jaribu
Na hapa ni vyakula mbalimbali vya asili viöivyopikwa kwenye vyungu utamu wake ni ngumu kuelezea bora uonje mwenyewe.
Na hapa ni vyakula mbalimbali vya asili viöivyopikwa kwenye vyungu utamu wake ni ngumu kuelezea bora uonje mwenyewe.
Tuesday, October 1, 2019
LEO NILIKWENDA MSTUNIKUCHUMA UYOGA ...
Msimu ni ule majira ya kupukutika kwa majani. Kwa hiyo ni msimu wa uyoga pia kwa hiyo wapenzi wa uyoga tunafurahia sana kwenda mstuni na kuchuma/kutafuta uyoga. Kumbuka uwapo msituni sio unachuma uchoga tu ...La hasha ni mazoezi makubwa sana na pia kama ulikuwa na msongo wa mawazo basi msitu ni sehemu nzuri sana na kuwa.
Nawatakieni kila la kheri tuonane tena panapo majaliwa.....kapulya wenu!
Nawatakieni kila la kheri tuonane tena panapo majaliwa.....kapulya wenu!
Friday, September 27, 2019
Thursday, September 19, 2019
Sunday, September 8, 2019
Wednesday, September 4, 2019
KILA MTU ALIMAPO ANATEGEMEA KUVUNA CHOCHOTE:- NAMI LEO NIMEVUNA NILICHOPANDA VIAZI
Nimevuna nichopanda ni viazi matosani au wengine huviita viazi ulaya katika kundi hilo la viazi
...kumetokea kiazi cha umbo kama la moyo angalia mwenyewe
Friday, August 23, 2019
KAZI YA MIKONO YANGU....BUSTANI
Hapa ni zao la zabibu
Na hapa nimepanda mchicha na figiri ila nimechelewa kidogo. Lakini nina matumaini nitakula tu:-)
Wednesday, August 7, 2019
UFUKWE RESTRAND:- UKIWA ZANZIBAR USIKOSE KULA HAPA KUNA CHAKULA KITAMU
Hapa ni baadhi ya wafanyakazi wetu
...na hapa ni kundi nzima
Meneja, akiwa na baadhi ya wafanyakazi kama vile mpishi na dada msaidizi wake
Monday, August 5, 2019
NYUMBANI NI NYUMBANI NA UFIKAPO NYUMBANI NI RAHA SANA KUONANA NA NDUGU
Hapa nipo Lundusi na mama zangu yaani binamu zake baba yangu
Na hapa nipo na dada yangu Anastasia alikuja kunisalimia baada ya miaka 20 kupita bila kuonana
Hapa tupo Mkurumo kwa mjomba wetu...mpiga picha ni mimi kapulya
Hapa tulipata mgeni anaitwa Chacha alikuja kututembelea ilikuwa ni furaha sana.Hapa tulipata wasaa kuwatembelea mapadre na kupata chakula cha jioni...
Zanzibar Forodhani 24/7-19
Saturday, July 27, 2019
Sunday, July 21, 2019
Sunday, July 14, 2019
NIMEPITA SOKONI SONGEA NIKAKUTANA NA VYAKULA NIVIPENDAVYO SAMAKI MBELELE NA LIKUNGU NILI
Hapa ni samaki aina ya mbelele watamu sana sana ila wana miba ndogo ndogo ulapo yabudi uwe mwangalifu sana...
Wednesday, July 10, 2019
Saturday, July 6, 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)










































