Monday, March 19, 2018

MICHEZO YA WATOTO:- UKUAJI NA MAARIFA WAYAPATAYO....!

 Watoto uwaleavyo ndivyo wakuavyo hapa wakiwa wanacheza bao mchangani....zaidi mchezo huu huchezwa na watoto wakiume....au vijana pia akina baba. Wengi wetu nadhani twaukumbuka mchezo huu...ni mchezo lakini hapo kunamambo wanajifunza kama vile hesabu nk.
 Na hapani watoto wa kike wakicheza mchezo wa mdako... nilipenda sana mchezo huu....maharage yalikuwa yanaungua kila mara :-)
 Watoto wengi hasa wa kiume walipenda sana kucheza huu mchezo kama baiskeli au gari vile ni ringi la baiskel ...hapa watakiwa kuwa na balansi...
Usipojifunza mapishi tangu udogo itakuwa shida...ni mchezo lakini ndiyo kujifunza huko.....zamani watoto walikuwa wakijifunza vitu vingi sana na kupata maarifa ...lakini sasa  mmmhhh wapo mitandaoni tu....

2 comments:

ray njau said...


Si ajabu kwamba mara nyingi wanariadha wachanga huathiriwa na tabia ya wazazi wenye hasira na makocha wenye bidii ya kupita kiasi. Katika mechi ya voliboli ya wasichana, marefa walishambuliwa mara saba na wachezaji. Msichana mmoja aliharibu gari la afisa alipotolewa katika mchezo wa tenisi. Refa alipopuliza filimbi ya kuonyesha kwamba mpiganaji wa mieleka wa shule ya sekondari alicheza vibaya, mchezaji huyo alimgonga refa kichwani kwa kichwa chake mpaka refa akazirai. “Michezo ya vijana [ilijulikana] kuwa yenye utulivu,” asema Darrell Burnett, mwanasaikolojia wa watoto na michezo ya vijana. “Lakini sasa hali zimebadilika. Hiyo si michezo tena.”

Jambo Ambalo Wazazi Wanaweza Kufanya

Inafaa wazazi wakumbuke kwamba watoto hupendezwa na michezo kwa sababu ya kupata furaha na kufanya mazoezi kwenye michezo hiyo. Wazazi wanapoigeuza michezo ya watoto iwe kazi yenye kuleta mkazo mwingi na mahali pa kuwafokea watoto, hawawezi kupata matokeo yaliyokusudiwa na hilo si tendo la upendo. Biblia inasema: “Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu.”—Waefeso 6:4, Biblia Habari Njema.

Mzazi awezaje kudumisha usawaziko katika jambo hilo? Kwanza kabisa, huenda ikafaa kukumbuka hali yako ulipokuwa kijana. Je, ulicheza kama bingwa? Je, inafaa kumtazamia mwanao acheze kama bingwa? Ukweli ni kwamba “watoto ni dhaifu.” (Mwanzo 33:13, Zaire Swahili Bible) Pia, jaribu kuwa na maoni yanayofaa kuhusu kushinda na kushindwa. Biblia husema kwamba roho ya ushindani isiyodhibitiwa ni “ubatili na kujilisha upepo.”—Mhubiri 4:4.

Kwa kupendeza, aliyekuwa mchezaji wa ligi kuu ya besiboli huwahimiza wazazi wadumishe maoni yanayofaa kuhusu kushinda na kushindwa, wasikasirike watoto wao wasiposhinda wala kusisimuka kupita kiasi wanaposhinda. Badala ya kuona ushindi ukiwa jambo la maana zaidi, wazazi wanapaswa kuzingatia furaha ya watoto na afya yao njema.

Hivyo, wazazi wengine wameona kwamba michezo mingi ya watoto huchochea roho isiyofaa ya ushindani. Hata hivyo, hiyo haimaanishi kwamba watoto wao hawawezi kucheza pamoja na wengine. Kwa mfano, wazazi wengi Wakristo wametambua kwamba watoto wao hufurahi wanapocheza pamoja na waamini wenzao katika ua wa nyumbani au bustanini. Hapo wazazi wanaweza kudhibiti mashirika ya watoto wao. Pia, watoto wanaweza kucheza wakati wa matembezi ya familia. Ni kweli, kucheza kwenye ua wa nyumbani huenda kusitokeze msisimuko mwingi kama kushiriki katika mashindano. Hata hivyo, usisahau kwamba “mazoezi ya kimwili ni yenye manufaa kidogo (tu); lakini ujitoaji-kimungu ni wenye manufaa kwa mambo yote.” (1 Timotheo 4:8) Kwa kudumisha mtazamo huo wenye usawaziko kuhusiana na michezo, unaweza kumwepusha mtoto wako kutokana na madhara yanayoletwa na wimbi jipya la jeuri.(Chanzo:www.jw.org/sw)

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray ulichosema ni kweli kabisa naongeza tu siku hizi watoto hawasikii kabisa inasikitisha sana.
Nukuu "Inafaa wazazi wakumbuke kwamba watoto hupendezwa na michezo kwa sababu ya kupata furaha na kufanya mazoezi kwenye michezo hiyo. Wazazi wanapoigeuza michezo ya watoto iwe kazi yenye kuleta mkazo mwingi na mahali pa kuwafokea watoto, hawawezi kupata matokeo yaliyokusudiwa na hilo si tendo la upendo. Biblia inasema: “Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu.”—Waefeso 6:4, Biblia Habari Njema." mwisho wa nukuu hapa nimepapenda sana tuwaache watoto wawe watoto