Maana: Chombo ambacho Yesu Kristo aliuawa juu yake huitwa na walio wengi katika Jumuiya ya Wakristo kuwa msalaba (Kiingereza, cross). Neno hilo la Kiingereza linatokana na neno la Kilatini, crux.
Kwa nini vichapo vya Mashahidi wa Yehova humwonyesha Yesu akiwa juu ya mti na mikono yake ikiwa juu ya kichwa chake badala ya kuwa juu ya msalaba kama kawaida?
Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “msalaba” katika tafsiri nyingi za kisasa za Biblia (“mti wa mateso” katika NW) ni stau·rosʹ. Katika Kigiriki cha kale, neno hilo lilimaanisha mti ulionyooka au nguzo tu. Baadaye likaja pia kutumiwa kurejezea mti wenye kijiti kilichokingamana ambao watu waliuawa juu yake. The Imperial Bible-Dictionary inakubali jambo hilo, inaposema, “Neno la Kigiriki linalotafsiriwa msalaba [stau·rosʹ], kwa kufaa lilirejezea mti, nguzo iliyonyooka au kipande cha mhimili, ambacho kitu chochote kinaweza kutundikwa juu yake, au ambacho kinaweza kutumiwa kuchomeka katika [kuzungushia ua] kiwanja. . . . Hata kati ya Waroma crux (chanzo cha neno la Kiingereza cross), yaonekana kwamba mwanzoni ilikuwa nguzo iliyonyooka.”—Iliyohaririwa na P. Fairbairn (London, 1874), Buku la 1, uku. 376.
Je, hivyo ndivyo ilivyokuwa Mwana wa Mungu alipouawa? Ni jambo linalostahili kuangaliwa kwamba Biblia pia inatumia neno xyʹlon kutambulisha chombo kilichotumiwa. A Greek-English Lexicon, ya Liddell na Scott, inafafanua neno hili hivi: “Mti uliokatwa na ulio tayari kutumiwa, ukuni, ubao, n.k. . . . kipande cha mti, gogo, boriti, nguzo . . . bakora, rungu, . . . mti ambao wahalifu walitundikwa juu yake . . . mbao, mti mbichi.” Inasema pia “katika AJ, msalaba,” na kutaja Matendo 5:30 na 10:39 kuwa mifano. (Oxford, 1968, uku. 1191, 1192) Hata hivyo, katika mistari hiyo UV, ZSB, na VB hutafsiri xyʹlon kuwa “mti.” (Linganisha tafsiri hiyo na Wagalatia 3:13; Kumbukumbu 21:22, 23.)
Kitabu The Non-Christian Cross, cha J. D. Parsons (London, 1896), kinasema: “Hakuna hata sentensi moja katika yale maandishi mengi yanayofanyiza Agano Jipya katika Kigiriki cha kwanza, inayotoa hata uthibitisho usio wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba mti uliotumiwa katika kisa cha Yesu ulikuwa tofauti na miti ya kawaida; ingewezekanaje basi mti huo haukuwa kipande kimoja cha mti bali vipande viwili vilivyopigiliwa misumari pamoja, kwa namna ya msalaba. . . . Walimu wetu wanatupotosha sana wanapotafsiri neno stauros kuwa ‘msalaba’ wakati wa kutafsiri hati za Kigiriki za Kanisa katika lugha za kwetu, na kuunga mkono tendo hilo kwa kuweka ‘msalaba’ katika kamusi zetu kuwa ndiyo maana ya stauros bila kueleza kwa uangalifu kwamba kwa vyovyote, hiyo haikuwa ndiyo maana ya msingi ya neno hilo katika siku za Mitume, haikuwa maana yake ya msingi mpaka muda mrefu baadaye, na basi ikawa hivyo, kwa sababu tu ya kwamba, ijapokuwa ukosefu wa uthibitisho wa kuunga mkono, ilikuwa ni kwa sababu fulani au nyingine iliyodhaniwa kwamba mti ule ambao Yesu aliuawa juu yake ulikuwa na umbo hilo hususa.”—Uku. 23, 24; ona pia The Companion Bible (Thetford, England, 1974), Nyongeza Na. 162.
Hivyo uthibitisho mwingi unaonyesha kwamba Yesu alikufa juu ya mti ulionyooka wala si juu ya msalaba kama unavyojulikana.
Kulingana na historia, msalaba wa Jumuiya ya Wakristo ulitoka wapi?
“Vitu mbalimbali, vya tangu zamani za kale kabla ya Ukristo, vimepatikana, vikiwa na alama za misalaba yenye maumbo mbalimbali, karibu katika sehemu zote za ulimwengu wa kale. Misalaba mingi ya aina hiyo imepatikana India, Siria, Uajemi na Misri . . . Matumizi ya msalaba kama mfano wa kidini katika nyakati za kabla ya Ukristo na kati ya mataifa yasiyo ya Kikristo yanaweza kuonwa kwamba yalienea kila mahali, na katika visa vingi sana yalihusiana na namna fulani ya ibada ya vitu vya asili.”—Encyclopædia Britannica (1946), Buku la 6, uku. 753 --------------- Chanzo:www.jw.org/sw
2 comments:
Msalaba
Maana: Chombo ambacho Yesu Kristo aliuawa juu yake huitwa na walio wengi katika Jumuiya ya Wakristo kuwa msalaba (Kiingereza, cross). Neno hilo la Kiingereza linatokana na neno la Kilatini, crux.
Kwa nini vichapo vya Mashahidi wa Yehova humwonyesha Yesu akiwa juu ya mti na mikono yake ikiwa juu ya kichwa chake badala ya kuwa juu ya msalaba kama kawaida?
Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “msalaba” katika tafsiri nyingi za kisasa za Biblia (“mti wa mateso” katika NW) ni stau·rosʹ. Katika Kigiriki cha kale, neno hilo lilimaanisha mti ulionyooka au nguzo tu. Baadaye likaja pia kutumiwa kurejezea mti wenye kijiti kilichokingamana ambao watu waliuawa juu yake. The Imperial Bible-Dictionary inakubali jambo hilo, inaposema, “Neno la Kigiriki linalotafsiriwa msalaba [stau·rosʹ], kwa kufaa lilirejezea mti, nguzo iliyonyooka au kipande cha mhimili, ambacho kitu chochote kinaweza kutundikwa juu yake, au ambacho kinaweza kutumiwa kuchomeka katika [kuzungushia ua] kiwanja. . . . Hata kati ya Waroma crux (chanzo cha neno la Kiingereza cross), yaonekana kwamba mwanzoni ilikuwa nguzo iliyonyooka.”—Iliyohaririwa na P. Fairbairn (London, 1874), Buku la 1, uku. 376.
Je, hivyo ndivyo ilivyokuwa Mwana wa Mungu alipouawa? Ni jambo linalostahili kuangaliwa kwamba Biblia pia inatumia neno xyʹlon kutambulisha chombo kilichotumiwa. A Greek-English Lexicon, ya Liddell na Scott, inafafanua neno hili hivi: “Mti uliokatwa na ulio tayari kutumiwa, ukuni, ubao, n.k. . . . kipande cha mti, gogo, boriti, nguzo . . . bakora, rungu, . . . mti ambao wahalifu walitundikwa juu yake . . . mbao, mti mbichi.” Inasema pia “katika AJ, msalaba,” na kutaja Matendo 5:30 na 10:39 kuwa mifano. (Oxford, 1968, uku. 1191, 1192) Hata hivyo, katika mistari hiyo UV, ZSB, na VB hutafsiri xyʹlon kuwa “mti.” (Linganisha tafsiri hiyo na Wagalatia 3:13; Kumbukumbu 21:22, 23.)
Kitabu The Non-Christian Cross, cha J. D. Parsons (London, 1896), kinasema: “Hakuna hata sentensi moja katika yale maandishi mengi yanayofanyiza Agano Jipya katika Kigiriki cha kwanza, inayotoa hata uthibitisho usio wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba mti uliotumiwa katika kisa cha Yesu ulikuwa tofauti na miti ya kawaida; ingewezekanaje basi mti huo haukuwa kipande kimoja cha mti bali vipande viwili vilivyopigiliwa misumari pamoja, kwa namna ya msalaba. . . . Walimu wetu wanatupotosha sana wanapotafsiri neno stauros kuwa ‘msalaba’ wakati wa kutafsiri hati za Kigiriki za Kanisa katika lugha za kwetu, na kuunga mkono tendo hilo kwa kuweka ‘msalaba’ katika kamusi zetu kuwa ndiyo maana ya stauros bila kueleza kwa uangalifu kwamba kwa vyovyote, hiyo haikuwa ndiyo maana ya msingi ya neno hilo katika siku za Mitume, haikuwa maana yake ya msingi mpaka muda mrefu baadaye, na basi ikawa hivyo, kwa sababu tu ya kwamba, ijapokuwa ukosefu wa uthibitisho wa kuunga mkono, ilikuwa ni kwa sababu fulani au nyingine iliyodhaniwa kwamba mti ule ambao Yesu aliuawa juu yake ulikuwa na umbo hilo hususa.”—Uku. 23, 24; ona pia The Companion Bible (Thetford, England, 1974), Nyongeza Na. 162.
Hivyo uthibitisho mwingi unaonyesha kwamba Yesu alikufa juu ya mti ulionyooka wala si juu ya msalaba kama unavyojulikana.
Kulingana na historia, msalaba wa Jumuiya ya Wakristo ulitoka wapi?
“Vitu mbalimbali, vya tangu zamani za kale kabla ya Ukristo, vimepatikana, vikiwa na alama za misalaba yenye maumbo mbalimbali, karibu katika sehemu zote za ulimwengu wa kale. Misalaba mingi ya aina hiyo imepatikana India, Siria, Uajemi na Misri . . . Matumizi ya msalaba kama mfano wa kidini katika nyakati za kabla ya Ukristo na kati ya mataifa yasiyo ya Kikristo yanaweza kuonwa kwamba yalienea kila mahali, na katika visa vingi sana yalihusiana na namna fulani ya ibada ya vitu vya asili.”—Encyclopædia Britannica (1946), Buku la 6, uku. 753
---------------
Chanzo:www.jw.org/sw
Amina nakutakia kwaresima njema sana!
Post a Comment