Thursday, February 23, 2017

KUMBUKUMBU:- BLOGG YA MAISHA NA MAFANIKIO LEO YAFIKISHA MIAKA TISA (9) YA KUBLOGG...!!

Napenda kuwashukuruni wasomaji wangu wa blogg ya Maisha na Mafaniko kwa kuwa nami bega kwa bega kuendesha libeneka hili. Nina uhakika bila ninyi nisingekuwa hapa leo...pia napenda kuishukuru familia yangu, kwani kublogg yataka moyo. Basi tuunganee pamoja kwa siku hii ya leo kwa kuisherekea BLOGG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO KWA KUTIMIZA MIAKATISA (9) YA KUBLOGG.

9 comments:

emu-three said...

Hongera sana kwa kufikisha miaka hiyo tisa, mengi tumejifunza kutoka kwako ndugu wa miye, nakupongeza kwa hilo, na umekuwa hukati tamaa...wengi wameshindwa kuendeleza blog zao lako wewe bado umo..HONGERA SANA, NA TUPO PAMOJA

daileth mbele said...

Hongera sana kwa kazi nzuri na tunamshukuru Mungu kwa vipaje alivyokupa.Huu ni mwaka wa tau tangu nimekuwa mfuasi wa blog hii na sijawahi kuichoka.Nisipoitembelea naimiss pia

daileth mbele said...

Niseme pia nakushukuru maana wewe ni miongoni mwa blogger mlionihamasisha kubenda kusoma blog hata na kuwa blogger pia.Napenda vile unablog so natural .Nami sasa nina blog kwenye chemchemi3.blogspot.com/

Anonymous said...

Hongera sana dada Yasinta kwa kutimiza miaka 9 ya hili libeneke. Nakuombea maisha na mafanikio itimize zaidi ya miaka 100 katika kutuhabarisha na kutuburudisha asante sana.By Salumu.

Nicky Mwangoka said...

Hongera sana Dada. Kiota cha Miasha na Mafanikio ni kisima chenye mengi tunayohitaji maishani. Endelea kutuhabarisha na kutufurahisha. Big up!

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana Kadala wa mimi..

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni sana kwa kuwa nami katika kuadhimisha miaka tisa ya Blog yetu ya Maisha na Mafanikio. Mmeonyesha ushirikiano mzuri sana PAMOJA DAIMA.

NN Mhango said...

Happy birthday Maisha na Mafanikio hata kama nilichelewa sherehe.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango wala hata hujachelewa..pia kipande chako cha keki chakusubiri na chai isiyo na sukari...maana nimesikia ww nawe hunywi chai ya sukari:-)