Saturday, July 18, 2015

BUSTANI YETU NA MAENDELEO YAKE...KAZI YA MIKONO YANGU

 Hapa ni MCHICHA upo katika hali nzuri kidogo
 Na hapa ni mboga MABOGA sisi wanguni tunasemana LIKOLO LA NANYUNGU/PITIKU:-)
Na hapa mnaona ndo mara ya kwanza kuchuma hiyo mboga ya Maboga na mchicha na pembeni mnaona ni pilipili. Kwa hiyo kwa jioni ya leo ni kujichana tu. KARIBUNI TUJUMUIKE NDUGU ZANGU:-) ni mimi Kapulya wenu.

5 comments:

Manka said...

Hongera Dada Yasinta Bustani imependeza,mwaka huu Bustani yangu haijastawi kabisaa,ningekuwa karibu ningekuja kuchuma mboga za maboga lol

Anonymous said...

Hongeara saaaaana, ni efurahi kuona unavuna sasa,

Yasinta Ngonyani said...

Manka dada yangu...yaani hata mimi mwenzio mwaka huu sina furaha kabisa na bustani yangu yaani sijui nimerudia kupanda mara ngapi...Mwaka huu hali ya hewa haina msimamo...ila ungekuwa karibu ungechuma tu mboga...

Usiye na Jina Ahsante sana ni kweli nimevuna kwa maera ya kwanza na kuonja na pia nyingine nimeweka akiba...Kwa ajili yako Karibu:-)

ray njau said...

Hongera sana!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kaka Ray, karibu kuja kula:-)