Friday, June 26, 2015

MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA

Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)

5 comments:

Ester Ulaya said...

dada umenitamanisha huu msosiiii...kesho nami nakula

Nicky Mwangoka said...

Tamu sana jamani

Yasinta Ngonyani said...

Ester! Mmhhh sasa hii si tabia njema kunitamanisha hivyo...ukipika nikaribishe...

Kaka Nicky ..ww acha tu

NN Mhango said...

Da Yasinta shukrani kwa mlo huu mtakatifu, kani nimekula kwa macho hadi nikavimbiwa. Nakushukuru sana kwa uchokozi wako hata hivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango! Kama umeshiba nashukuru...kuhusu uchokozi sijui kama nakubaliana nawe:-)