Monday, December 13, 2010

NGOJA LEO TUANGALIE METHALI ZETU:- METHALI ZAFAA SANA KWA MAFUNDISHO YA ADILI!!!

1.Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu.
2. Baada ya dhiki, faraja.
3. Baba wa kambo si baba.
4. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
5. Chombo kilichopikiwa Sakaki, hakiachi kunuka vimba.
6. Damu nzito kuliko maji.
7. Dawa ya moto ni moto.
8. Fadhili za punda, mashuzi; na msihadhari ni ngómbe.
9. Fumbo mfumbie mjinga , mwerevu hulingámua.
10. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuli.
11. Gonga gogo usikilize mlio Wake.
12. Hakuna siri ya watu wawili.
13. Hasira, hasara.
14. Ihsani haiozi.
15. Jungu kuu halikosi ukoko.
16. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza
17. Kila mlango na ufunguo Wake.
18. Kulea mimba si kazi´, kazi kulea mototo

9 comments:

Unknown said...

mmh kweli dada yangu. Methali hizi ni muhimu sana katika mafunzo katika jamii. Hata hivyo kuna baadhi ya methali zinakingana zenyewe kwa zenyewe na zingine zimepitwa na wakati... Je waweza fahamu ni zipi zilizopitwa na wakati?? Swali hili nakuachia na tafadhali naomba jibu!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mrope! hapana sijui ni zipi zimepetwa na wakati na sikujua kama methali zinaweza kupitwa na wakati NIAMBIE KAKANGU ni zipi hizo?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

.Asiyefunzwa na mamaye, hakumlea
2. Baada ya dhiki, maumivu.
3. Baba wa kambo ni baba, unajuaje kama babayako sio wa kambo.
4. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
5. Chombo kilichopikiwa Sakaki, hakiachi kunuka vimba.
6. Damu nzito kama maji tu.
7. Dawa ya moto ni moto! hauuguagi huu.
8. Fadhili za punda, mashuzi; na msihadhari ni ngómbe.
9. Fumbo mfumbie mjinga , mwerevu hulingámua.AFUMBE MJINGA kama sio kwa nini kufumba fumba?
10. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuli.
11. Gonga gogo usikilize milo Wake NITAUMIA.
12. Hakuna siri ya watt wawili ndio maana hutokeza mimba japo ilikuwa siri.
13. Hasira, faida kwa wengina.
14. Ihsani haiozi.
15. Jungu kuu halikosi ukoko hata kama umeoza, sasa wa nini.
16. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza
17. Kila mlango na ufunguo Wake master key je?.
18. Kulea mimba si kazi´, kazi kulea mototo ahaje? wewe mimba? hujui kilichomo ni kazi bora mtoto unamwona

emu-three said...

Mimi nahisi methali kupitwa na wakati wake ni kwa mtumiaji mwenyewe, na tafsiri ya mtumiaji(Kama Kamala alivyotoa). Unaweza ukaitumia kwa muda fulani na kwa muda fulani isifae kwa wakati huo, lakini bado ikaja kutumika kwa wakati mwingine!

WA UKAE said...

nisaidieni maana ya methali hii, "kozi mwana mandanda, kulala njaa kupenda".

Anonymous said...

Hello everyone, it's my first visit at this web site, and piece of writing is in fact fruitful in favor of me, keep up posting these posts.

my page - payday loan

Unknown said...

Maana ya methali kupitwa na wakati inatokana na maana ya watumiaji na uhalisia katika maisha ya kawaida.
Mfano,samaki mmoja akioza wote wameoza
.wengi wape.aliyejuu mngoje chini,asiyekujua hakuthamini.

Methali hizo kwa namna Fulani zimepitwa na wakati ukirejelea matumizi yake huwa na athari hasi kwa wa watumiaji .kwa maelezo zaidi nitafute

Anonymous said...

Zilizopitwa na wakati

Anonymous said...

Mifano mingine ya methali zilizopitwa na wakati