Friday, January 16, 2009

UZAZI WA MPANGO

Hili swali limekuwa likinikera sana akilini mwangu:- Na sasa nimeona inabidi sasa tuanze kuamasisha uzazi wa mpango. Kwa sababu kuna wengi wanafikiri watoto ni rasilimali.

Jamiii inabidi tuzingatie uzazi wa mpango. Ili kuepuka watoto wa mitaani. Pia ni lazima kujali afya ya mama na malezi ya mtoto n.k.

Kama tukirudi nyuma tunakumbuka kulikuwa na kitu kilikuwa kinaitwa nyota ya kijani. Nashangaa sasa kwa nini tunayumba.

Kwa hiyo inabidi tuanze kuhamasisha kwani hali imekuwa mbaya, watoto wanazaliwa kila "asubuhi" wakati wazazi hawana uwezo wa kuwapa watoto hao:- kama vile chakula, malezi, malazi, elimu nk.

Mfano mzuri ni katika bara letu la Afrika:- Watoto huonekana kama baraka, na kuwa na watoto wengi huonekana kuwa ni baraka kubwa. Hivi ndivyo ilivyo. Lakini, mara nyingine, badala ya baraka mtu hukuta huzuni, uchungu na masikitiko.

Tuzae watoto ambao tunajua tunaweza kuwapa malezi bora kuliko kuzaa wengi kwa sababu ya tu eti nina watoto wengi, huku ukijua huwezi kuwapa malezi BORA.

4 comments:

MARKUS MPANGALA said...

wanawake/mama zetu huwa na kawaida ya kusema KUZAA KUONDOA MARADHI, hakika nimeshindwa kuwasamehe kwa hili. mjitetee

Anonymous said...

we mtoto unatafuta radhi ya mzee Gervas Vincent Ngonyani. uzazi wa mpango ndio kitu gani hasa! kumbuka kuna mambo kibao yanachukua hao watoto, kuna simba, chui, mamba, ajali na kadhalika, ukimwi na kadhalika utabaki na nini kama umezaa wachache. wee zaa sana tu.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

nafikiri kuna zaidi ya uzazi wa mpango unaopelekea yote hayo..

ila nahisi sina jibu la haraka..

Koero Mkundi said...

Sisi kwetu tumezaliwa sita na tumeachana kati ya miaka mitatu hadi minne,

mdogo wangu wa mwisho nimeachana naye kwa miaka minne, mpaka nilianza kudeka nikijua ni mimi wa mwisho

Sijui mama yngu alikuwa anafuata uzazi wa mpango?

Mimi sijui labda nimuulize.