Tuesday, December 7, 2010

Elimu/kujitegemea na ushirikiano kati ya wanafunzi na wazazi!!.

Sokoni/Julmarknad!!


Wikiend iliyopita ambayo ilikuwa kama ifuatavyo. Sasa tuendelee:- Wanafunzi wa darasa la sita ambalo binti yetu naye anasoma wanataka kufanya safari (skolresa) darasa zima ili kuona mazingira mengine. Na safari kwa kila mwanafunzi ni 700kr ni sawa na 140000Tsh.

Wakawa wanajiuliza tufanyeje ili tupate hizi pesa?. Mmmh! Tuchangishe pesa kila mtu/kichwa kitoe 700kr Hapana, tupite kuuliza kila nyumba kama tunaweza kusafisha magari , Hapana.

Bahati nzuri sasa ni kipindi cha majilio(christmas) na wikiend hii iliyopita kulikuwa na soko kwa ajili ya christimas (Julmarknad) basi wakapata wazo kuwa watushirikishe wazazi kutengeneza chochote kile kama vile keki, pipi, kuoka mikate, kutengeneza Kanawa, chai, chokleti nk. Hakika hutaamini jinsi wazazi tulivyo/walivyowaunga mkono, wacha kazi za kuoka zianze...... binafsi nilioka mikate kama 100 vile.

Na baada ya kuoka ikabidi wazazi na watoto/wanafunzi waende sokoni jumamosi na jumapili siku ya mapumziko. Tukaacha shughuli nyingine na kumbuka hii shughuli itafanyika nje na baridi sio mchezo. Hilo halikuwa tatizo Kabila wazazi na watoto tulikwenda huko sokoni (julmarknad) na Kuuza hivyo vitu ili watoto wapate ppesa na kuweza kufanya safari (skolresa) yao. Kwa kweli huu ni mfano ambao kama sisi waTanzania tungeiga nina imani tungekuwa na maendeleo. Sio kila kitu kutaka kupata kwa mteremko tu. Ebu ingia hapa na usoma makala hiii inafanana sana Milano yako na huu.

9 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hii ni safi sana, kwa kweli kama ulivyosema inabidi tuige mfano huu wabongo.

Yasinta je mlifanikiwa kufikia lengo lenu la fedha? nina maanisha kama wanunuzi waliwaunga mkono..

Baraka kwenu.

emu-three said...

Ama kweli haya ndiyo yatakiwayo hasa huku kwetu...lakini mmmmh, mchango wa harusi utavuka lengo. Mchnago wa shule...mmmh, mwalimu atakauka kooo, kila mtu mmmmh, sina, hali ngumu!

Yasinta Ngonyani said...

Mija! si uungo mifano tuigayo wabongo ni mifano ambayo haina maendeleo ya maendeleo inaachwa kama nisemavu kila wakati waTanzania tumejifunga na hatujafunguka kwetu kila kitu tupo nyuma. Oh! kumbe! ndiyo tumefanikisha lengo wamepata fedha kutosha na mwezi wa tano watafanya huo msafara wao.

emu3 naona mmmhh nyingi kweli kumbuka ya kwamba mchango wa harusi ni mkubwa sana na labda harausi yenyewe inadumu siku tatu tu na elimu ya mwanao itadumu milele..... Ahsannteni

Anonymous said...

وكان هذا حقا للاهتمام. كنت أحب القراءة

Unknown said...

huu ni mfano wa kuigwa na wazazi huko bongo. Eeh! mbona kimya tena?? au ndio mambo ya sikukuu ya uhuru?

Mija Shija Sayi said...

Yasinta hukupiga picha mikate uliyoioka? Ninaihitaji sana kwenye kazi ya mikono yangu.

chib said...

Huyo anony anayecharanga sijui kiarabu vipi tena!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hii nimeipenda!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu nimekuelewa nashukuru kwa kuona umeipenda hii mada. karibu sana tena.

Kaka Mrope ni kweli kabisa ulixchosema. Nipo kakangu nilikuwa mdhaifu kidogo.

Mija bahati mbaya ilikuwa haraka na nikatingwa sikupiga picha. Nitafanya hivyo siku nyingine.:-(

Kaka Chib! Ndiyo ni kiarabu na maana yake "Hii ilikuwa kweli ya kuvutia. Mie napenda kusoma" ni hilo tu.

Kaka Chacha! Ahsante kwa mchango wako.