Saturday, August 21, 2021
Wednesday, August 11, 2021
Wednesday, June 9, 2021
Monday, May 10, 2021
MKE ASIYE NA MUME, AKAMCHUMBIE NANI?
Niolewe na nani mie!
Isingekuwa vigeni, mwanamke kuchumbia
Ningepita mitaani, mume kujitafutia,
Nisimuudhi Manani, ndio nimejizuia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Ndege maingainga, si jambo la kujitakia,
Mume mwema natamani, vipi tajitafutia?
Na mwanamume haini, sitaki kunichumbia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Nimetulia nyumbani, sina mume kunioa,
Wanifuatao ndani, si wachumba wa kuoa,
Hutaka kunirubuni, maasini kunitia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Ndege maingainga, si kosa langu sikia,
Niliolewa zamani na mume mwenye udhia,
Kanitia kilabuni, pombe kumchuuzia
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Mimi nikamuamini, huku machozi nalia,
Mume hii kazi gani, alokataza jalia?
Kheri tukate kuni, mimi nitakuuzia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Akapanda hasirani, na maneno akafyoa:
Mke wee mke gani, dini lini ulijua!
Alipozidisha kani, ndoaye nikajivua.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Wako mabwana wa shani, ningependa kunioa,
Hawamtii shetani, Munguamewaongoa,
Nao wamomashakani, kwa mabibi walooa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Tu wema hatujuani, wake na waume pia,
Twaingia mashakani, kwa wenzi waso murua,
Namlilia Manani, mume mwema kunioa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Nawe muombe, ndoa yenu kutulia,
Tusikuone mwakani, viragoumepania,
Mke na mume nyumbani, mumche Mola Jalia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?
Shairi hili limetungwa na Sheikh Amri Abedi, nami limenivutia nikaona niliweke hapa ili tujifunze kwa pamoja
Thursday, May 6, 2021
MAHINDI YA KUCHOMA NI BORA KULIKO POP CORN!
Hivi kwa nini tusile mahindi ya kuchoma tuingiapo sinema kama ilivyo utamaduni wetu badala ya kula pop corn?
Friday, April 16, 2021
Thursday, March 25, 2021
TUMALIZE MWEZI HUU WA TATU KWA UJUMBE HUU UFUATAO:-
UHURU WA NCHI NI SAWA NA AFYA YA MWILI/MWILINI.
NAPENDA KUWATAKIENI AFYA NJEMA NA TUUMALIZE MWEZI HUU SALAMA.
PAMOJA DAIMA!
KAPULYA WENU.
Sunday, February 21, 2021
Monday, January 18, 2021
Monday, December 21, 2020
Thursday, November 26, 2020
Sunday, November 8, 2020
Monday, October 26, 2020
TUFANYA HII IWE PICHA YA WIKI HII...SEHEMU FULANI TANZANIA
Nimeipenda hii mandhari nzuri ..kuingalia tu yavutia. Kwa hiyo nafikiria je nikiwa/ukiwa hapo iitakuwaje...mmhh nawaza tu kwa sauti! TUPO PAMOJA DAIMA!
Friday, October 2, 2020
NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA NA MWANZO MWEMA WA MWEZI HUU WA KUMI KWA BURUDANI HII
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/amL_MTCsOms" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe>
MWISHO WA JUMA UWE MWENYE AMANI NA FURAHA KWETU WOTE. TUSISAHAU KUWAOMBEA WAGONJWA WETU...
Friday, September 4, 2020
HII NI PICHA YA WIKI :- HAPA NIPO NA MARAFIKI TUPO SHAMBANI KWA WAKULIMA KUNUNUA MBOGAMBOGA BILA KUSAHAU MAHINDI
Nadhani hapo mwamuona kapulya wenu ... msione tumevaa makoto baridi imeanza
Hapa kapulya anashangaa mmea fulani ni raha sana kuwenda shambani na kuchuma mbogamboga na mkulima kazi yake ni kupanga bei tu...:-)
Saturday, August 29, 2020
Sunday, August 16, 2020
Sunday, July 12, 2020
PALE UNAOKOSA SEHEMU YA KULIMA MBOGA MBOGA/BUSTANI USIKATE TAMAA TUMIA NDOO AU MAKOPO KAMA NILIVYOFANYA MIMI HAPA
Hapa ni Nyanya, mchicha, Tangawizi Malimao, parachichi nk. Karibu tutaanza kula nyana mchicha nishakula mara nyingi tu
Friday, July 3, 2020
Saturday, June 20, 2020
JIONI YA JUMAMOSI YALEONIMEONA SI MBAYA KAMA TUKITEMBELEA KWETU MBAMBA BAY
Angalia mandhari ilivyo nadhani ukiwa hapa hutataka kutoka maana ni fukwe nzuri sana. Niwatakieni JIONI YA JUMAMOSI HII IWE YENYE UTULIVU MWANANA. Wenu Kapulya!
Sunday, June 14, 2020
Wednesday, June 3, 2020
Monday, May 25, 2020
USAFIRI WETU...AKINA MAMA TUNAWEZA
Nimeona tuanza wiki hii kinamna hii maana nadhani leo hap ni siku ya akina mama...kwa hiyo napenda pia kuwapa shukrani akina mama wote. Tuzidishe uaminifu maana ndiyo nguzo ya mafanikio.
Monday, May 11, 2020
UPUPU - MANGATUNGU CHAKULA CHA ASILI CHA WANYASA/WANGONI
JE? Wewe una chakula cha asili katika asili yako?
Friday, May 8, 2020
LEO NIMESHINDA NATAMANI HIVV VYAKULA MAANA NDIVYO VILIVYONIKUZA
Hapa ni mahindi ya kuchoma eeeh bwana weee acha tu
Dagaa na mboga maboga ni mboga tamu sana...
.....na bila kusahau ugali yaani natamani khali ya hewa iwe joto ili nianza kulima mbogamboga zangu
Subscribe to:
Comments (Atom)






















