Sunday, April 20, 2008

Aprili 20,2008 maisha,mila, desturi, ndoa na mahali

Nina rafiki mmoja anazungumzia kuhusu maisha ya ndoa ya Afrika na kila anapojaribu kuwaelezea watu kuwa. Sisi waafrika tunapokaribia umri wa kuoa kitu cha kwanza ni kutafuta mchumba na ukishampata zinaanza shughuli za kupanga mahali. Lakini wao wanashangaa sana hata hawaelewi kabisa kwa nini tunatoa MAHALI. Wao wanadai ya kwamba tunauza, kama kuku. Yaani mzazi wa msichana anamuuza binti yake. Wanasema kama tunatoa mahali kwa kuwashukuru wazazi wa upande wa kike je kwa nini na wazazi wa upande wa kiume wasipongezwe kwa kazi nzuri ya kumtunza kijana wao. hata kama ukiwaambia ni njia ya kuonysha respect pia. Ndugu wasomaji kusema kweli sisi wanadamu tunaishi katika mila na desturi tofauti kabisa. Kwani hapa wao hili jambo la ndoa halihusishwi kabisa kwa wazazi. Ni baina ya kijana na msichana. wanaelewana wao wawili tu kama kufunga ndoa au kuishi hivihivi. Sasa hapa bado sijaelewa sawasawa kama hii ni sababu ndoa zao hapa hazidumu muda mrefu. Haya wasomaji je kuna maelezo zaidi ya kuwaeleza watu hawa. MCHANGO basi.

Na; Yasinta Ngonyani

1 comment:

Anonymous said...

Mmm hii habari imenikuna sana yaani nimejikuta nikijiuliza je utamaduni wetu ni mbaya?lakini sitashawishika hadi naingia kaburini kukubali kwamba utamaduni wetu wa kushirikiana na mitindo mingine ya maisha ambayo ni mizuri kwamba ni mibaya.Lakini ukitazama maisha ya wazungu ni kama vituko ambavyo unaweza kudhani huenda mungu atawaadhibu sana{mimi sijui},lakini kwa kweli ni utamaduni safi sana ingawa bado nabaki na swali je kutoa MAHALI ni sahihi?kama siyo,tufanye nini?kipi mbadala wake?