Ulemavu wa viungo nao sababu zake zinafanana kabisa na zile za mtindio wa ubongo. Kama nilivyoeleza katika makala yangu moja wiki mbili zilizopita .
Kwa mfano, zipo baadhi ya dawa hasa za kutuliza maumivu ambazo zinapotumiwa na akina mama wajawazito, husababisha kuzaliwa kwa watoto wenye upungufu wa viungo au vilema (Deformed Children).
Ipo sababu nyingine ya kibaiolojia inayotokea wakati wa kutunga mimba. Hata hivyo unapotaka kuzungumzia jambo hili inahitaji ushahidi unaojitosheleza.
Ajali pia ni mojawapo ya sababu zinazopelekea ulemavu wa viungo. Kwa mfano, ajali ya gari, kuanguka na kuumia michezoni, zote hizi husababisha ulemavu wa viungo wa kudumu.
Ulemavu huu unaweza kusababisha hali ya kupooza (Paralysis), kukosa uwezo wa kutembea au hata kupoteza nguvu za kiume. Inawezekana umeshawahi kusikia au kuona mtu aliyeumia mpirani au kuanguka juu ya mti na kupata ulemavu wa kudumu.
Leo ningependa kuzungumzia zaidi tatizo la kupooza ambalo huwapata watu wengi.
Kwanza kuna kupooza kunakoanzia katika sehemu ya kiuno kwenda chini miguuni kwa lugha ya kitalamu kunaitwa paralplegic.
Pili kuna kupooza kunakoanzia shingoni kuja mabegani na kwenda chini miguuni kunakofahamika kitaalamu kama Quadriplegic. Watu wenye matatizo haya huhitaji kiti chenye magudumu ili waweze kutembea. Hata hivyo watoto wenye ulemavu unaoambatana na hali ya kupooza huweza kusaidiwa kwa kutumia njia zifuatazo.
Wazazi wenye watoto wanokabiliwa na tatizo hili wantakiwa wazitengeneze nyumba zao kwa kuzingatia hali halisi ya maradhi ya watoto wao. Kwa mfano wanapaswa kutengeneza njia ambayo itatumika katika kupitisha kiti cha magurudumu badala ya ngazi, vitu ama vifaa vya kuchezea vya watoto wa aina hii sharti vihifadhiwe kwenye kabati ambalo litawekwa kwenye sehemu ya wazi ambayo mtoto anaweza kuifikia na kuchukuwa vitu anvyohitaji bila kuomba msaada.
Pia ianshauriwa kuwaeleza watoto wenzake pale nyumbani au hata wale watoto wa majirani kuhusu ulemavu wa mwenzao, kwamba ni kitu ambacho kinaweza kumtokea mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wao, ingawa wamezaliwa wakiwa na viungo kamili.
Hii itawajenga kisaikolojia watoto hao wasimtenge au kumdharau mwenzao ambaye ni mlemavu.
Watoto wa aina hii haitakiwi kuwaonesha kwamba hawawezi kufanya kitu chochote. Hivyo inashauriwa kuwajengea tabia ya kujitegemea kwa kuwaruhusu wafanye yale wanaoweza kuyafanya, kwani kwa kufanya hivyo kutawajengea hali ya kujiamini.
Je watoto wenye maradhi ya kudumu wanasaidiwaje?
Watoto wenye maradhi ya kudumu kama vile pumu, kisukari au kifafa ni miongoni mwa watoto wenye kuhitaji msaada maalum, inashauriwa kuwafahamisha watoto hao juu ya maradhi yanayowa sumbua ili wayafahamu na kuyazoea, pia hata wanafunzi wenzao au watoto wa majirani ni vema pia wakafahamishwa kuhusu maradhi yanayowasumbua wenzao kwani itasaidia kupunguza utani na dhihaka dhidi yao. Kwa upande wa waalimu inashauriwa kuwa watoto wa aina hii upendeleo na uangalizi wa karibu pale inapobidi kulingana na tatizo la mtoto husika.
Ukweli ni kwamba kuzaa mototo mwenye matatizo niliyoyaeleza siyo dhambi na wala hatupaswi kuwatenga watoto au watu wa aina hii, kwani wakipatiwa elimu bora na ya kutosha wanaweza kabisa kujitegemea kwa kufanya kazi za aina mbalimbali na kulipa kodi na kuchangia pato la Taifa. Kama nilivyosema katika mada iliyopita kwamba sio lazima wawe na kazi ya maana ila cha msingi ni kuwa na kitu cha kufanya.
6 comments:
Bila kuwasahau wenye mtindio wa ubongo.
Ujumbe wako umetulia, ahsante
umesahahu dhambi za wanawake katika kusababisha matatizo. sumu wawekazo kichwani baadhi ya vipozi nk, huleta ulemavu.
pia kuna wanaopaswa kulemaa kufutana na karma za maisha yaliyopita. ulemavu na matatizo ya kiafya mengine ni ya kurirhi
Asanteni Chib na kamala! nawaombeni rudini nyuma na someni mada iitwayo:- WATOTO WENYE MATATIZO YA MTINDIO WA UBONGO niliandika tarehe 15/5
Asante Dada. Kuwathamini na kuwaheshimu na kuwapenda ni jukumu letu sote. Na ni hilo litakalowawezesha kuwa msaada kwetu.
Baraka kwako
haka ni kadarasa kenye mvuto.
ni vyema wanablog tukitoa elimu kama hizi ili jamii itambue kuwa kuzaliwa na ulemavu sio kikwazo cha kujiletea maendeleo.....walemavu wakiwezeshwa wanaweza, kinachotakiwa ni kuwapa fursa tu basi...
Dada Yasinta hili darasa lisiishie hapa liendelee......... kazi nzuri sana
Asanteni wote mnajua kwa mimi binadamu wote hapa duniani ni sawa na kila mmoja ana haki yake/zake.
Post a Comment