Thursday, February 2, 2012
Kweli pamoja tunaweza tukazuia hali hii isitokee katika nchi yetu?
Kw pamoja naamini tunaweza kufanya hali hii isitokee katika taifa letu ingawa kuna maeneo kuna hali ngumu ambao hata huwezi kuizungumza, ndugu zangu wazalendo tuungane pamoja bila kujali wewe ni chama gani, dini au ukabila tuseme sasa inatosha na hali hii.
Wednesday, December 21, 2011
MVUA KUB WA YASABABISHA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA!!
Hapa ni baadhi ya wakazi wa spenco Vingunguti wakiwa wamekusanyika kusubiri boti iwaokoe.Picha toka kwa michuzi-
Wednesday, October 12, 2011
HALI YA MTOTO CECILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI
Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.
Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.
Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.
Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapema kwa uchunguzi tunaweza tukawaepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
HABARI NIMEIPATA KWA KAKA:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog
Thursday, September 8, 2011
MATITI NI CHAKULA CHA MTOTO AU?
Sijui kwa ajili ya kukosa watoto au Kweli huu ni UUNGWANA kweli kumnyonyesha mbuzi?
Na huyo naye anamnyonyesha mtoto wa ndama kisa? Sijui akimngáta hapo atasema nini?
Hapa sawa, mama akimpa mtoto chakula ambacho ndicho chakula bora sana kwa watoto wachanga. Ila kuna simulizi nimeisikia kuwa, wanaume wengi huwa wanaona WIVU sana wakati mama/mke wake amnyonyeshapo mtoto. Hasa mtoto wa kiume. Sijui wenzangu nanyi mmewahi kusikia? Na kama kweli kwanini sio anyonyeshwapo mtoto wa kike?Wednesday, August 31, 2011
Mtoto huyu ametelekezwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa na ulemavu njia ya haja kubwa!!!!
----------------------------------------------------------------------------------------------
Mtoto huyo anasumbuliwa na tatizo la kutokwa na sehemu ya haja kubwa nje kila anapokwenda kujisaidia na kwamba sehemu hiyo hukaa nje kwa hadi saa tatu kisha huanza kurudi yenyewe taratibu ambapo mtoto huyo hupata maumivu makali.
Kutokana na mtoto Anna kuzaliwa na tatizo hilo,baba yake mzazi anadaiwa alikuwa anampiga mtoto huyo kila sehemu ya haja kubwa inapotoka nje wakati anajisaidia hatimaye aliamua kumpa talaka mke wake na kwenda kuoa mwanamke mwingine ambapo mama mzazi wa Anna naye aliamua kwenda kuolewa na mume mwingine katika mji wa Mbambabay mwambao mwa ziwa Nyasa.
Mtoto Anna akiwa na mama yake mzazi tatizo hilo liliendelea kumsumbua mtoto huyo ingawa alimpeleka katika zahanati ya kijiji pamoja na kwenda kwa waganga wa jadi kwa ajili ya kutafuta tiba za jadi ,hata hivyo tatizo liliendelea hali iliyosababisha mama huyo kumtelekeza mtoto wake baada ya kukata tamaa.
Mtoto Anna mapema mwaka huu alichukuliwa na shangazi yake ambaye anaishi mjini Songea na kwamba baba mzazi wa mtoto huyo alimwambia dada yake ambaye ni shangazi ya mtoto huyo kuwa amchukue ampeleke hata kwa wachuna ngozi yeye hamtaki kwa madai kuwa ameleta laana katika familia yake.
Shangazi ya mtoto huyo alimchukua mtoto huyo na kuanza kuhangaika ili kutatua tatizo hilo ndipo alimpeleka kwa rafiki yake katibu ya Tanzania Assemblies Of God TAG kanisa la Ruhuwiko Songea Veronika Milanzi pichani kulia akiwa na mtoto Anna ambaye alikuwa akimpeleka katika kanisa hilo kwa ajili ya kumfanyia maombi kila siku.
“Nilimpompeleka siku ya kwanza kanisani kwa ajili ya kufanyiwa maombi mtoto huyu alikataa kurudi tena kwa shangazi yake tangu wakati huo hadi sasa ni karibu mwezi wanne mtoto huyu anaishi na mimi ,shangazi yake amekubali niendelea kuishi naye hadi sasa lakini tatizo lake la kutoka haja kubwa bado linaendelea’’,alisema
Katibu huyo wa TAG licha ya kumfanyia mtoto maombi kila siku lakini pia alichangishana fedha na baadhi ya waumini ili kumpeleka mtoto katika hospitali ya misheni ya Peramiho ambako walimchunguza na kudai kuwa angekuwa na tatizo la kutoka utumbo wa haja kubwa bila kurudi ndani wangemfanyia upasuaji na kumaliza tatizo hilo na kwamba kwa kuwa utumbo wa haja kubwa wa mtoto huyo unatoka nje anapokwenda haja na kisha unajirudi ndani pole pole hawana uwezo wa kumfanyia upasuaji.
Akizungumzia kitaalamu kuhusu tatizo hilo Dk Henry Mayala anasema magonjwa katika njia ya haja kubwa kitalaamu yanaitwa bawasiri ambayo ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi.
Dk.Mayala anabainisha kuwa bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa na kwamba kuna aina mbili za bawasili ambazo ni bawasili ya nje na ndani“Bawasili ya nje hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid na bawasili ya ndani hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili’’,alisisitiza.
Kulingana na mtaalamu huyo bawasili ya ndani imegawanyika katika madaraja manne ambayo ni daraja la kwanza la ni kutotoka katika mahali pake pa kawaida,daraja la pili bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo,daraja la tatua bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo na daraja la nnebawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Amezitaja sababu zinazosababisha magonjwa ya haja kubwa kuwa ni pamoja na Tatizo sugu la kuharisha,Kupata kinyesi kigumu Ujauzito,Uzito kupita kiasi (obesity), Ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex),Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.• Umri mkubwa.
Milanzi ambaye anataka kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam au hospitali nyingine ambazo zinaweza kutoa matibabu anatoa rai kwa watu wenye mapenzi mema kumsaidia mtoto huyo gharama za matibabu,usafiri na kujikimu kwa kuwa yeye haina uwezo.
Iwapo umeguswa na ungependa kutoa ushauri au msaada wa wowote wa kufanikisha matibabu ya mtoto Anna Mapunda andika albano.midelo@gmail.com,simu+255 766463129
Friday, June 3, 2011
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO ERIK !!!/Grattis på Födelsedagen Erik!!!
Thursday, May 26, 2011
HAWA WAMEANZA WEEKEND LEO! KAAZI KWELIKWELI HAPA!!!
Friday, March 18, 2011
JAMANI HUU KWELI NI UUNGWANA? KWELI BINADAMU KUFUNGWA KAMBA KAMA MBUZI????
Habari hii imenigusa sana kwa kweli, yaani bado tunaishi miaka ya 1970-1990 sikutegemea kabisa kama mambo haya yatakuwa bado katika ulimwengu huu. Najua ni sehemu nyingi si Afrika tu walikuwa wanaona ni kama laana kupata watoto wenye mtindio wa akili. Nakumbuka nimewahi kushuhudia kwa macho yangu familia moja ilikuwa na mtoto mwenye mtindio wa akili. Walikuwa wakimficha ndani hakuna aliyejua, kama kuna mtoto wa aina hiyo pale nyumbani pao. Siku moja nilipita pale, na nikakutana na mama wa nyumba anampeleka haja kubwa nikamuhoji inakuwaje ndo akanisumulia. Kwa kwa kweli jamii yetu haina ule utu kabisa kwani walikuwa wakiwacheka na mambo mengine mabaya mengi. Lakini kitu kimoja ambacho kimenipa nguvu ni kwamba sio sisi tu. Hata wenzetu nchi zilizoendelea walifanya hivyo walipopata watoto wa mtindio wa akili waliwaacha sehemu maalumu, lakini hata hivyo hawakupata yale maisha ambayo kila binadamu anastahili. Kwa hiyo nachotaka kusema hapa kwa fikra zangu ni kwamba najua kwamba kila binadamu anastahili kupata maisha bora awe mwenye akili timamu au mwenye mtindio wa akili. BINADAMU WOTE NI SAWA. HEBU SOMA HABARI HII HAPA CHINI KUHUSU PICHA HIYO HAPO JUU yenye kichwa cha habari kama ifuatavyo.
HUYU NI MKOROFI NDIO SABUBU ANAISHI KWA KUFUNGWA KAMBA.!!!!?
"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 23 na 25
Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.
Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.
Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.Hapa ni mwanzo tu zaidi inga hapa .
Tuesday, March 1, 2011
NIMEJIFUNZA KUTOKA KWA CHRISTINA
Christina akiwa amelazwa KCMC Moshi

Akiwa mjini Arusha akifanya manunuzi baada ya kuruhusiwa kutoka KCMC

Akimsimulia rafiki yaka Laila, walipokutana mjini Arusha
Huwa tunajifunza kupitia kwa wengine hususan kwa yale mambo magumu na yaliyojificha. Naomba nikiri kwamba pamoja na kusoma ushuhuda mbalimbali kupitia magazeti na blogs, lakini sikuwahi kuzipa uzito shuhuda hizo. Naomba nikiri kuwa tukio la hivi karibuni lilipompata rafiki yangu na wifi yangu Christina aishiye Dar es salaam Tanzania nimejifunza kuwa imani ikichangizwa na ibada ina nguvu sana.
Christina Kaluse ni wifi yangu wa hiyari ambaye ni mke wa mwanablog mwenzangu na ambaye ni mwanautambuzi anayetuelimisha kupitia kibaraza chake cha Utambuzi na Kujitambua, huyu si mwingine bali ni mwanablog Shaban Kaluse, ukitaka kusoma habari zake waweza kubofya hapa.
Nimekuwa nikiwasiliana na Christina kwa takriban miaka miwili sasa, na tangu kufahamiana na familia hii ya mwanablog mwenzangu, nimejikuta nikiwa karibu nao tukiwasiliana mara kwa mara kama ilivyo kwa baadhi ya wanablog wengine.
Nisiwachoshe, niwasimulie kisa cha kuandika kile nilichojifunza kwa wifi yangu huyu Christina au mama Abraham.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumatatu ya Januari 31, 2011, majira ya mchana, nilipata ujumbe mfupi kupitia simu yangu ya kiganjani kutoka kwa Christina, na ujumbe wenyewe ulisomeka hivi, ‘Yasinta naomba uungane nami kwenye maombi, nimepofuka jicho moja’ .
Ujumbe huo ulinishtua sana, nikaamua kumpigia simu ambapo tuliongea kwa muda mrefu sana.
Kwa kifupi aliniambia kuwa mnamo siku ya jumatano ya Januari 19, 2011, akiwa dukani kwake, (Christina anamiliki duka la vifaa vya ushonaji na ubunifu wa mavazi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam) aliingiwa na vumbi kidogo kwenye jicho lake la mkono wa kushoto, na alijaribu kulisafisha jicho hilo kwa maji safi lakini halikupata nafuu na liliendelea kumuuma.
Alikata shauri kurudi nyumbani kwake ambapo sio mbali na mahali ilipo ofisi yake, alipofika nyumbani aliendelea kulisafisha jicho lake hilo kwa maji safi, lakini halikupata nafuu yoyote.
Usiku kucha hakulala pamoja na kumeza vidonge vya kutuliza maumivu.
Ilipofika asubuhi akiongozana na mumewe walikwenda hospiali maarufu hapo jijini Dar iitwayo Regency ambapo alionana na daktari bingwa wa macho na baada ya vipimo iligundulika kuwa mboni ya jicho imepata kidonda na daktari huyo alidai kuwa huenda lile vumbi liliambatana na mchanga na hivyo wakati alipokuwa analisafisha ule mchanga ukawa umejeruhi mboni ya jicho hilo.
Kumbe huo ukawa ni mwanzo wa safari ya jicho hilo kupofuka, Christina alinieleza kuwa pamoja na kupatiwa matibabu katika hospiali hiyo lakini hakupata nafuu yoyote na usiku kucha alikuwa akikesha kwa maumivu makali ya jicho hata pamoja na kumeza vidonge vya usingizi lakini hakupata lepe la usingizi.
Ilipofika siku ya jumamosi ya January 29, 2011,ikiwa ni siku kumi tangu aanzwe na tatizo hilo, jicho likapoteza uwezo wa kuona na mboni ya jicho ikageuka na kuwa kama ina mtoto wa jicho, kwa maelezo yake Christina alisema kuwa hata yule daktari bingwa wa macho pale Regency alionekana kuchanganyikiwa kutokana na hali ile na alionekana kukata tamaa, lakini hata hivyo alimwandikia dawa nyingine na kumtaka akazitumie kisha arudi siku ya jumanne.
Aliporudi nyumbani walishauriana na mumewe na wakakata shauri kuhamia katika Hospitali ya CCBRT ambayo ndiyo hospitali maarufu hapo nyumbani ambayo inasifika kwa kutibu matatizo mbalimbali ya ulemavu yakiwemo matatizo ya macho.
Siku hiyo ya jumatatu ya Januari 31, 2011 aliyonitumia ujumbe mfupi, ndiyo siku ambayo alikwenda CCBRT. Baada ya vipimo, daktari aliyempima bila kutafuna maneno alimweleza waziwazi kuwa jicho limeshapofuka, na alimlaumu eti amechelewesha jicho huko vichochoroni mpaka limepofuka ndio anakwenda kwao…..
Kauli hiyo ilimshangaza sana Christina, kwani tangu alipopata tatizo hilo alikwenda kupata matibabu kwenye Hospiali ya Regency ambayo inatambulika na inasifika kwa matibabu, sasa iweje alaumiwe na kuambiwa kuwa alikuwa vichochoroni? Christina alionesha kushangazwa kwake na maadili ya Daktari yule.
Yule Daktari ambaye ni Mtanzania mwenzetu (Hospitali hiyo inayo pia wataalamu wa kigeni) alimweleza kuwa tiba pekee iliyobaki ni kuweka uzingativu kwenye kutibu kidonda tu, na hata akipona hataweza kuona kabisa kwani jicho limeshambuliwa na bacteria kiasi kwamba limeharibiwa kabisa. Hata hivyo alikiri kushindwa kubaini aina ya bakeria waliomshambulia, pamoja na kukwangua kidonda hicho na kupima maabara.
Aliandikiwa aende siku ya Jumanne ya Februari 1, 2011, kwa ajili ya operesheni ndogo ya kuliweka dawa na kulifunga.
Wakati naongea naye kwenye simu walikuwa wamekata shauri yeye na mumewe wamgeukie Mungu wakaamua waende kwenye maombi.
Nilimuuliza zaidi ya mara mbili kuwa ana imani akienda kwenye maombi atapona, na alinijibu kwa kujiamini kabisa kuwa daktari pekee aliyebaki ni mungu.
Ingawa tunatofautiana kimadhehebu, Christina yeye ni Msabato na mimi ni Mkatoliki, lakini nilimuahidi kuungana naye katika maombi.
Ni kweli siku iliyofuata alinijulisha kuwa aliombewa na Mwinjilisti mmoja wa kanisa la Wasabato la Chang’ombe SDA aitwae James Ramadhan Rajabu na maumivu yakatoweka na jicho likafunguka na likaanza kuona siku hiyo hiyo….ingawa hata hivyo bado lilikuwa linaonekana kama lina mtoto wa jicho.
Aliniambia kuwa anasafiri kwenda Moshi KCMC kuendelea na matibabu lakini bado imani yake kwa Yesu ni kubwa na anaamini atapona, kwani Mungu ndiye atakayekuwa Daktari mkuu atakayewaongoza Madaktari watakaomtibu huko KCMC.
Tuliendelea kuwasiliana hata alipokuwa huko Moshi KCMC, na alinijulisha kuwa awali madaktari wa KCMC walikanusha kuwa jicho lake limepofuka baada ya vipimo, ingawa hawakuweza kuona aina ya bacteria waliomshambulia.
Walishauri alazwe halafu watajaribu kuwasiliana na daktari mwingine bingwa aliyeko Nairobi ili kuangalia kama anaweza kuja hapo KCMC kushughulikia kesi yake ambayo hata wao iliwachanganya sana, hasa baada ya kuwaeleza kuwa CCBRT wameshindwa kutibu jicho lake.
Siku iliofuata yule daktari kutoka Nairobi alifika na baada ya kulipima jicho lake mara kadhaa hakupata majibu ya kueleweka, aliamua kuchuna sehemu ya kidonda na kuchukua sampuli ambayo ingepelekwa Nairobi kwa ajili ya vipimo katika maabara kasha. Aliamuandikia dawa za matone ambazo zitazuia wale bacteria wasiendelee kushambulia jicho lake wakati akisubiri majibu.
Katika kipindi chote alichokuwa amelazwa hapo KCMC akisubiri majibu ya vipimo vyake kutoka Nairobi, alikuwa akiendelea na maombi kwa kushirikiana na Mwinjilisti James pamoja na Wainjilisti wengine wa dhehebu lake la Kisabato aliowataja kwa majina ya Mwinjilisti Japhet Magoti Matotiwa kanisa la Manzese, na Mwinjilisti Benson Kilango Izoka wa kanisa la Bombo SDA Tanga.
Baada ya siku tatu yule Daktari alirudi na majibu, lakini cha kushangaza alikuta kidonda kimepona kwa asilimia 75. Hali ile haikumshangaza yule daktari peke yake bali pia Madaktari wenzie nao walishangazwa na kule kupona kwake kwa haraka.
Kwa mujibu wa majibu aliyokuja nayo, iligundulika kuwa jicho la Christina lilishambuliwa na Fangasi.
Aliandikiwa dawa na siku iluyofuata ikiwa ni siku ya tano tangu alazwe Hospitalini hapo aliruhusiwa kurudi nyumbani Dar, lakini alitakiwa kurudi klinik baada ya wiki mbili ili kuangaliwa kama anaendeleaje.
Baada ya kurudi Dar, aliendelea na dawa pamoja na maombi, na ilimchukua wiki moja tu kupona kabisa, na jicho kurudi katika hali yake ya kawaida.
Aliporudi Moshi KCMC, Daktari alithibitisha kuwa amepona kabisa, na hakusita kuweka bayana kuwa kupona kwake kumekuwa ni kwa miujiza kwa sababu kutokana na hali ya jicho lake walidhani ingechukua muda mrefu hadi kupona.
Jana nilizungumza naye kwa muda mrefu sana akinisimulia safari hii ndefu ya ugonjwa wake huo na jinsi maombi pamoja na imani ilivyomsaidia kupona kwa haraka.
Kwa kweli nimejifunza jambo moja kubwa sana kutokana na mkasa huu uliompata wifi yangu huyu wa hiyari ya kutokata tamaa pale tupatapo changamoto za kimaisha kama vile ugonjwa na hali zetu kimaisha.
Kama Christina angekata tamaa na kusikiliza ushauri wa Daktari wa CCBRT, ni wazi kuwa leo hii angekuwa amepofuka jicho moja. Lakini yeye mwenyewe alidai kuwa alikataa katu katu kukubaliana na maelezo ya Daktari yule na aliiambia nafsi yake kuwa jicho lake halijapofuka na halitapofuka.
Naamini hata wewe unayesoma hapa kuna jambo utakuwa umejifunza.
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Christina kwa kuwa na ujasiri wa kukabiliana na changamoto hiyo. Namuomba Mungu aendelee kuibariki familia yao, awape ujasiri wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha, na asiwape moyo wa kukata tamaa.
Nimejifunza kutoka kwa Christina.
Monday, February 28, 2011
MWANAFUNZI WA MIAKA 12 KUWA MKE WA TATU WA MZEE VISENTI HAULE
Habari hii imenigusa sana sana sanaaaaaaa na nimeona niiweke hapa Maisha na mafanikio ili tuweza kujadili pia kwa pamoja. Jamani hivi SHERIA zinatungwa ili iweje??? Baada ya kusoma habari hii nimekuwa ninajiuliza:- Hivi huu ni mwisho wa dunia? Au wanawake wamekwisha? Miaka 12 kuanza maisha ya ndoa halafu mke wa tatu kweli huu ni uungwana/utu kweli? Haya hapa ni habari yenyewe tuwe pamoja.
Binti wa miaka 12 katikati Veronika Charlle wa darasa la tano, akiwa na mwenye kiti wa kijiji cha Sinai Talisis Mkanula na mhudumu wa afya msingi Christina Njovu.walijaribu kumsaidia mtoto huyo lakini kukawa na urasimu wa kushindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa Bwana Vinsenti Haule kwa kesi ya ubakaji maana huyu mtoto ni sawa na mjukuu wake.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Vinsenti Haule mkazi wa kijiji cha Sinai Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye ana wake wawili amemuoa mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Nakahuga Veronika Challe(12) kuwa mke wake wa tatu.Imeripotiwa na Albanos Midelo.
Thursday, December 30, 2010
"MJADALA ULIOVUNJA REKODI KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO MWAKA 2010"
Kwa hiyo basi nimeichagua mada hii kuwa ndio mada iliyovunja rekodi kwa mwaka 2010.
Natoa shukrani kwa wadau wote mlioshiriki katika kuichangia mada hii.
Naomba muungane nami katika kujikumbusha kile kilichotokea katika mjadala huu.
Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua, kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu. Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma
Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini. (picha na Albart Jackson).
Na: Yasinta Ngonyani kl. 1:14 AM
NA HAYA YALIKUWA NI MAONI YA WADAU...........
Koero Mkundi said...
Bora umeona na wewe Yasinta maan ningeona mie ninganangwa kweli na wahafidhina....
haya sijui na wewe utaitwa Femisist, kama mie...
Nakusikitikia kwa kuingia katika vita hii, jiandae kushambuliwa dada.....
April 8, 2010 7:20 AM
Yasinta Ngonyani said...
Koero mdogo wangu!Wala siogopi kabisa waiti watavyo na wanishambulie watavyo kwani atayefanya hivyo basi hajui utu na bado hajajua wanawake wana mateso gani na sio haki kupata mateso kama hayo. Tuna haki na tunatakiwa kupata.
April 8, 2010 7:40 AM
Anonymous said...
siku zotw huwa nanyata katika uwanja wako lakini leo nitacomment,huku ni ludewa kwetu na hii ilibiniwa kutokana na wananchi wanaoishi mjini ludewa kuwa na wageni mpaka 3 kwa mara moja (rejea extended family theory ya kiafrika) wakisubiri kujifungua hivyo ukabuniwa mradi huu wa kuwa na jengo lao.angalau sasa wanapumua...pia jengo hili lilitaifishwa toka kwa mjasiliamali mzalendo enzi za mwalimu......wageni wa hapa wengi ni wakisi,wamatumba,wamanda wapangwa ni wachache kwani huhudumiwa na lugarawa mission hospital
April 8, 2010 8:21 AM
Mija Shija Sayi said...
Mimi huwa nasema serikali inatakiwa ipinduliwe maana haifanyi kazi zake ipasavyo, sasa mwakilishi wa jimbo hili sijui ni nani ambaye anashindwa hata kupeleka ripoti serikalini kwa hospitali Ludewa hazina huduma nzuri.
Yasinta ukipata na picha za wodi za wanaume na watoto pia tuletee tuone nao wako katika hali gani.
April 8, 2010 9:19 AM
Baraka Chibiriti said...
Kwakweli maisha yetu yanasikitisha sana tena sanaaaa....basi tuu Mungu anatusaidia sana kutulinda kuendelea kwenda mbele na maisha haya ya tabu. Poleni sana akina mama jamani.
April 8, 2010 10:02 AM
John Mwaipopo said...
namnukuu mija shija sayi "Yasinta ukipata na picha za wodi za wanaume na watoto pia tuletee tuone nao wako katika hali gani."
nadhani za wanaume zitakuwa nzuri tu.
April 8, 2010 10:10 AM
Anonymous said...
kiukweli hii ni waiting home ya akina mama wanaosubiri siku zao zotomie,sio ward,kiuhalisia ward yao na inatosheleza mahitaji.na hii nyumba iko nje ya mazingira ya hosp yenyewe.si kweli kuwa kuna huduma mbovu za wazazi .............wa mkondachi
April 8, 2010 10:54 AM
Koero Mkundi said...
Ngoja ninukuu annony wa hapa.
"kiukweli hii ni waiting home ya akina mama wanaosubiri siku zao zotomie,sio ward,kiuhalisia ward yao na inatosheleza mahitaji.na hii nyumba iko nje ya mazingira ya hosp yenyewe.si kweli kuwa kuna huduma mbovu za wazazi .............wa mkondachi"
Mwisho wa kunukuu.
Kama hiyo kweli ni waiting home, ina maana kuwa hakuna vituo vya afya katika vijiji hivyo tajwa mpaka watu wakimbilie katika kituo hicho cha Afya cha Ludewa ambapo inabidi walundikwe kwenye hizo nyumba za kusubiri kujifungua.
kwa hiyo hata huyo mbunge wao hayajui madhila ya watu wake maana kama angeyajua basi wanawake hao tunaowaona hapo wangeshaondolewa tatizo hilo.
Ikumbukwe kamba walioshinda kwa ushindi wa kishindo walituahidi maisha bora kwa kila mtanzania na ujenzi wa zahanati kwa kila kata. sasa miaka mitano ndio hiyo inaishia........Je watakuja na msamiati gani?
Mimi nadhani kuna haja ya wananchi kuambiwa ukweli kuwa CCM imechoka na sasa ikae pembeni ili watu wenye utambuzi na uwezo wa kuongoza washike hatamu......hakuna haja ya kuimba CCM nambari wani kila baada ya miaka mitano wakati hata hawapo kwenye 100 bora.
Kwanza takwimu zinaonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya vijana hapa nchini ukilinganisha na wazee.....nadhani tunatosha kabisa kuondoa huu unafiki, watu mpaka meno yanang'oka kwa uzee lakini wamo tu kwenye siasa.....
nasema wameshindwa waondoke.....
nakubali kuwa wazee wanao mchango wao kwa taifa lakini kama hawazalishi idea za kulikwamua taifa hili kuondokana na tabia ya kuombaomba, lakini wameshindwa, basi wapumzike na tunawaahidi kuwalea na kuwatunza mpaka mungu atakapowachukua mbele ya haki ambapo huko watajua kile walichopanda tangu kuwepo kwao hapa duniani.
Narudia ena waondoke hawatufai.....
April 8, 2010 1:05 PM
Anonymous said...
Nikubali kutoka kwa koero kuwa huduma za uzazi katika vijiji si njema ndio maana akina mama hawa huja katika hospitali ya wilaya kwa huduma mapema zaidi na hutakiwa kusubiri katika nyumba hii.wanashauriwa kuja mapema ili kuepuka any complication ambayo inaweza kujitokeza ilikupata huduma mara uchungu unapoanza.viji vyenye angalau ya huduma ni manda,luilo,madunda,mlangali,makonde na lupingu kidooogo,but still vituom hivi si vya kutegemea sana kwani huduma thabiti pekee ni hapa ludewa na lugarawa mission hosp pekee.Koero pia hii ni wilaya katyi ya chache zinazowakilishwa na wabunge maprofesa,hapa yupo mh.Prof Raphael Mwalyosi.hao wasomi wataalamu wa afy ahawaja motishwa kwani huku ni moja ya wilaya ni tata kimazingira.......wa mkondachi
April 8, 2010 2:40 PM
Ramson said...
Name Raphael Mwalyosi
Surname Mwalyosi
First Names Raphael Benedict
Alternate Name
Title Prof
Country of Birth Tanzania
Positions
From To Organisation Position
2005 Ludewa Constituency
MP for Ludewa
Date of Birth 3 Dec 1946
Political Affiliation CCM
eMail
Telephone
Address
Notes EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Agriculture, Norway PhD 1988 1990 PHD
University of Dar es Salaam MSc. 1975 1979 MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam BSc. 1971 1974 GRADUATE
Tabora Boys' Secondary School A-Level Education 1969 1970 HIGH SCHOOL
Tabora Boys' Secondary School O-Level Education 1965 1968 SECONDARY
Madunda Middle School Primary Education 1961 1964 PRIMARY
Lufumbu Primary School Primary Education 1957 1960 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
University of Dar es Salaam/IRA Professor 1999 2005
University of Dar es Salaam/IRA Associate Professor 1993 1999
University of Dar es Salaam/IRA Senior Reseacher 1988 1993
University of Dar es Salaam/IRA Reseacher 1984 1988
Rufiji Basin Development Authority Ecologist 1979 1984
Tanzania National Parks Reseacher 1974 1979
--------------------------------------------------------------------------------
[ Retrieved on 13/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
April 8, 2010 3:04 PM
Anonymous said...
Namshukuru ramso kwa kupachika cv ya mheshimiwa wetu,na kama ujuavyo wataalamu wa mazingira ni wakereketwa wa nature zaidi kuliko vitu vingine kwani alishawahi endesha IRA pale UDSM IRA ni Institute of Resourcr assesment.Lakini kipimo cha picha hii tu kitatutosha kujudge au tukusanye takwimu zaidi lakini hata hali ya shle si njema sana na barabara hata uchumi pia au siju tumpate injiania aongeze na kasi ya uchimbaji wa makaa yetu ya mawe na chuma cha pua kule liganga,nina hamu nishuudie maana tangu nazaliwa niu habari ya upembuzi yakinifu mara mtalamu mshauri maka leo...daa twachoka......wa mkondachi
April 8, 2010 3:42 PM
Mbele said...
Hii makala imenigusa kiasi cha kuiweka kwenye blogu yangu, pamoja na utangulizi ambamo nimegawa vidonge kwa wahusika. Bofya hapa.
April 8, 2010 4:23 PM
PASSION4FASHION.TZ said...
Maisha bora kwa kila mtanzania.....?kweli? au watanzania ni wadanganyika kama watoto wadogo,wanaoambiwa usilie nikirudi nitakuletea pipi,mtoto ananyamaza na anakuwa na hope kuwa mama akirudi ataniletea pipi.
Jamani carne hii watu bado wanaishi maisha kama haya kweli? kinachosikitisha zaidi wanawake ndio wapiga kura wazuri wa kuichagua CHUKUA CHAKO MAPEMA(CCM) wanawake tuamkeni CCM haina shukurani wala fadhila, hawa wanawake wanahitaji msaada wa kuelimishwa,nahisi bado kuna watu wanamawazo finyu kuwa bila CCM haitakuwa Tanzania,kwa hali kama hii basi hayo maisha bora kwa kila mtazania zitabaki kuwa ndoto za alinacha!
April 8, 2010 4:52 PM
kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
kwani nyie si mko mijini?? mbona mimi nimebanana vijijini natoa hudma kwa wana vijiji. sasa nuoe kama wasomi na wabunge mko mijini mnalilia lia tu. anayeona huruma akawe diwani
lakini kwa wanawake ni kawaida kwani ndio wapiga kura wakuu
April 8, 2010 4:53 PM
Anonymous said...
Yasinta asante sana kwa kutujulisha yote haya mungu akuzidishie akupe afya njema wewe na familia yako. Ubarikiwe sana.Unapatwa na uchungu unalia unashindwa kujua ufanye nini? Mimi natokea Ludewa. Huu ni ujumbe ambao mkuu wa nchi ulitakiwa umfikie halafu ajitetee. Nafahamu si Ludewa peke yake lakini ni wilaya na vijiji vingi vina mapungufu haya. Huu ni upuuzi wa serikali yetu halafu tunawachagua viongozi wale wale wenye kujaza matumbo yao na kuwasahau wananchi. My take fukuza kazi watu wote husika kuanzia wizarani mpaka tukafike Ludewa kwenyewe huu ni upuuzi. Wanaludewa tufanyeje kukabiliana na hili? Kama tunaweza kufanya kitu basi wajameni tuwasiliane.Kukaa mbali na nyumbani hakuna maana tutashindwa kuleta msaada
April 8, 2010 5:21 PM
Yasinta Ngonyani said...Anony wa April 8, 2010 5:21 PM! Asante unajua ni kweli nimelia sana kutokana na jambo hili. Nimeshuhudia jambo hili kwa macho yangu wakati naishi Kijiji cha Kingoli kulikuwa na zahanati, lakini hakuna sehemu ya akina mama wajawazito kujifungulia na akina mama wengi walikuwa wana kufa. Hoospitali ya karibu ilikuwa ni Peramiho na kufika huko usafiri wake ulikuwa ni kutembea na mgonjwa/mamamjamzito amebebwa katika machela. Kufika Peramiho inachukua siku mbil. Je huu kweli uungwana?
April 8, 2010 5:44 PM
Anonymous said...
Hii picha imenisikitisha sana. Kwa hakika najua hiyo sio wodi ya hao akina mama wajawazito kama alivyosema mchangiaji mmmoja. Nafahamu utaratibu uliopo kule maeneo ya kwetu, ni kwamba akina mama wajawazito huwa wanapangiwa tarehe za kusogea jirani na hospitali ili kujitazamania kusudi siku ya kujifungua isiwe shida kufika hospital na kupata huduma inayostahili. Nafahamu hivyo kwa vile binafsi natoka jirani na hospitali kubwa na ya uhakika ya misheni Peramiho (kuna mpango wa kuifanya hospitali ya rufaa). Na katika utaratibu wa hiyo hospitali ni kwamba hata kama unatoka km kadhaa toka hospital ni lazima uende kujitazamia hapo hospital na tarehe za kwenda hapo wanakupangia wao wenyewe. Pale kwetu usafiri wa kufika Peramiho ni masaa 24 lakini hiyo hospital ni wakali sana, lazima uende kabla. Ukiuliza wanakupata vipi mpaka wakuamuru kwenda hapo mapema ni kwamba kama mjamzito anahudhuria clinic basi hapo ndio wanapokupata na kukuingiza katika utaratibu huo. Sasa hoja ninayotaka kusema hapa ni kwamba huu ni mpango mzuri sana hasa kwa maeneo ambayo huduma za hospital zipo mbali. Lakini sasa inabidi kuyafanya hayo mazingira yawe mazuri, yavutie na akina mama wakiwa hapo wawe na amani na sio kuwaweka katika mazingira kama hayo ya kwenye picha.
Inasikitisha sana kwa kweli hizo picha.
April 8, 2010 9:40 PM
Yasinta Ngonyani said...
ninenukuu toka kwa Hapa kwetu yaani Pro.Mbele kwa vile nimeyapenda haya maelezo yake! "Inasikitisha kuwa katika nchi yetu, yenye mali nyingi, hali ya watu katika vijiji vingi na mijini ni mbaya kiasi hiki.
Wenye madaraka wanafuja utajiri wa Tanzania. Kwa mfano, hivi karibuni tu, CCM imeagiza magari 200 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Fedha hizi zingeweza kutumiwa kuboreshea huduma za afya kwenye hospitali kama hii ya Ludewa, au kuwapa mitaji hao akina mama, wakabadilisha maisha yao.
Wako ambao wanachuma mishahara na marupurupu kwa mamilioni ya shilingi. Wako ambao wanatumia mamilioni kwenye sherehe na starehe. Wengine wamechota na labda bado wanachota, mamilioni ya shilingi na kuyahamishia nje, kwenye akaunti binafsi. Badala ya kutumia hela kuboresha huduma za afya sehemu kama hii ya Ludewa, Tanzania imetumia mabilioni ya shilingi, tangu miaka ya mwanzo ya Uhuru, kwa kuwapeleka wachache nje, kwa matibabu au hata tu kuchekiwa afya, mambo ambayo yangeweza kufanywa katika hospitali za nchini, kama vile Muhimbili. Ninafahamu jinsi gharama ya matibabu ilivyo mbaya katika nchi kama Marekani. Fedha zilizotumika miaka yote hii zingekuwa zimeboresha huduma katika hospitali sehemu mbali mbali za nchi." Mwisho wa kunukuu. Ni kweli inaumiza na kusikitisha shana na ningependa hii serikali ipinduliwe kabisa! Upendo Daima.
April 9, 2010 12:44 AM
Mija Shija Sayi said...
Yasinta, swali muhimu linakuja sasa wa kuipindua ni nani katika jamii yetu hii iliyofunzwa nidhamu ya WOGA?
April 9, 2010 1:18 AM
Yasinta Ngonyani said...
Da Mija ni sisi vijana wa leo au? ni lazima kuna mmoja asiye mwoga.
April 9, 2010 3:19 PM
Albert Paul said...
"Tanzania na Watanzania tuna amani" hii ndio hirizi iliyofungwa kwenye vichwa vyetu imiminayo nidhamu ya "WOGA" kwenye akili zetu. Mawazo haya "POTOFU" tumeyakumbatia kiasi kwamba yanatufanya tunashindwa kutetea haki zetu ipasavyo na kukosa umoja miongoni mwetu.
April 9, 2010 7:53 PM
penina Simon said...
Ha ha ha maybe yatasaidia jamani,manake mimi kwa uzoefu wangu sidhani kama mimba ni ugonjwa, ila hufuata unavyojiendekeza,
Mfano inaweza kukufanya uteme mate kila wkt na ukiendekeza utajikuta unatembea hadi na kikopo. Au kukuletea uchovu na ukiiendekeza basi utaamuka sa4,5..
etc.
April 10, 2010 3:23 PM
samuel blandes said...
Inasikitisha,Kliniki au hospitali kama hizo ziko nyingi nchini.Serikali isikimbilie kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi au idadi ya wilaya ni matumizi mabaya.Gharama za kujenga kliniki 20 na kuziendesha vizuri ni nafuu kuliko gharama za kuongeza jimbo mmoja la uchaguzi.Kupanga ni kuchagua.
Rwegasira
Singapore
April 11, 2010 8:29 AM
Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
Enzi za Prof Mwalyosi pale IRA mambo yalibadilika yakaifaya IRA ikatoka kuwa Institute of Resource Assessment ikawa Institute of Resource Assassination kwani Environmental Impact assessments za ajabu ajabu zilikuwa na bado zinafanywa na watu wa taasisi hiyo. Utaona miradi mikubwa ambayo utategemea kuwa haitopitishwa lakini waapi!!!
Hayo yanayotokea Ludewa yako kila pahala na ukistaajabu ya hospitali za wilaya utakuta kuwa hata hospitali za mikoa kama Mara utayakuta :-(
April 12, 2010 8:19 AM
nkwera said...
Yasinta
Hii picha umepewa au umepiga mwenyewe?
Mimi ninaishi mita chache kutoka kwenye nyumba hizo.
1. Hiyo siyo wodi ya akina mama, wodi ya akina mama wajawazito Ludewa ina vitanda zaidi ya 6o
2. Nyumba hiyo ipo ukingoni mwa eneo la hospitali na hutumiwa na wote wenye wagonjwa hapo hospitali lakini hawana pa kufikia. Bionafsi naona ni jambo jema hata nyumba si nzuri
3. Akina mama wanaosubiri kujifungua au wenye magonjwa hatarishi walishajengewa na vosacom foundation jengo zuri tu, ungeweza kuomba picha zake au kupiga mwenyewe:-) Habari zake zinapatikana hapa http://www.jambonetwork.com/blog/?p=59059
Hali ni mbaya vijijini lakini picha ulizotumia si sahihi na sielewi ulikuwa na nia gani kutumia picha hizo. Bottom line, those are not wards and probably you know it!
pdn
April 13, 2010 8:27 PM
Yasinta Ngonyani said...
Kaka nkwera ahsante kwa taarifa na hiyo link nitapita kuangalia.
April 13, 2010 10:51 PM
Simon. said...
poleni sana ndugu zetu watanzania wa huko ludewa na maeneo ya jirani na hapo ambao mnategemea matibabu kutoka katika hiyo hospitali. lakini sio ninyi tu huko hata sehemu mbali mbali za hii nchi wote wanateseka sana hasa linapokuja suala la hospitali na huduma za kina mama wajawazito nchini..hii ni kutokana na usimamizi wa serikali yetu kuwa ni wa kubabaisha!NADHANI NI WAKATI MUAFAKA SASA KWA SERIKALI KUWA SERIOUS KATIKA KUTATUA MATATIZO SUGU YANAYOWASUMBUA WALIPA KODI WA NCHI HII!!! tumeshachoka na sanaa zao!
April 15, 2010 5:36 PM
Anonymous said...
dada yasinta nipo mbioni kutangaza nia ya kushirikiana na wananchi kuondoa kero hizi sasa hakuna haja mpaka kusubiri "KUOMBWA NA WAZEE"wenye nia ya dhati trujitokeze si ubunge tu hata udiwani uongozi wa vijiji na mitaa unahitaji watu makini na wenye upeo wa kuondoa kero na si kuiongeza kero kama hizi.IWE NI WODI ISIWE NI WODI IREKEBISHWE HUDUMA ZA HAPA HAZIKIDHI VIWANGO VYA AFYA.Tuzindukesasa na tusababishe hali njema
April 20, 2010 10:56 AM
Friday, December 17, 2010
KUMBUKUMBU KWA MAMA YETU ALANA NGONYANI!!!!
Halafu natamani kweli kukusimulia jinsi wajukuu wako wanavyoendelea pia makuzi yao. Wao pia wanakukumbuka sana. Unakumbuka mara ya mwisho uliwapa zawadi Camilla ukamnunulia gauni na Erik shati na kaputula, bado wanavitunza mpaka leo. Na wanaviabudu mno.
Najua unanisikia huko uliko, sisi wote tunakukumbuka sana mama Ustarehe kwa Amani. SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA ZAIDI. AMINA.
AU MIMI NAMI NIKUKUMBUKE KWA WIMBO HUU HAPA CHINI NA KAKA ALBINO FULANI!!!!
Wednesday, October 27, 2010
Chai inapunguza mshtuko wa moyo!!!
Tuesday, October 26, 2010
Hawa ni ndio wacheza mpira watarajiwa!!
Hapa ni Erik mwaka huu mwezi wa nane anavyoufurahia mpira.
Na hapa ni shangazi zangu nao hawapo nyuma. Hawa ndio wale wanawake wa shoka Picha kutoka hapaFriday, October 22, 2010
Swali:- Ni ubunifu au?
Monday, September 20, 2010
NILIDHANI KUWA NI KAPULYA MDADISI TU KUMBE KUNA:- KIMWAGA MDADISI PIA!!!
Nimekisoma mimi na sasa watoto wangu wanasoma ama kweli raha
Hapo zamani palikuwa na motto moja aliitwa Kimwaga. Mtoto Hugo alimpenda sana babu yrke Lukindo. Kimwaga na babu yrke waliishi katika kijiji cha Kwemasafi, Wilayani Korogwe. Jioni, baada ya jua kuzama, Kimwaga alikuwa akikoka moto kwenye Kilanda chao cha mazungumzo. Babu yrke alikuwa akipenda sana kuota moto na kuzungumza na mjukuu Wake.
Siku moja jioni, Mzee Lukindo na Kimwaga walikuwa wakiota moto. Kimwaga alikuwa motto mdadis sana. Alimsimulia babu yrke habari moja iliyomshangaza. Alisema, “Babu, leo tulikuwa tukilima katika samba letu la shule. Mimi niliinua jembe kwa Nguru ili nichimbue magugu. Jembe likagonga jiwe, nikaona cheche za moto zinamulika. Hivi babu moto ulitoka wap?”
Babau yrke akamuuliza, “Hivi mjukuu wangu hujui hadithi ya moto?” Kimwaga akamjibu, “Sijui,” Babu yrke akamwambia, “Basi nikueleze kidogo, Hapo zamani za kale binadamu hawakuwa na moto. Waliishi katika mapango yenye giza. Walikula matunda na Nyala mbichi. Maisha yao yalikuwa ya tabu sana.
“Kwa Bahai, siku moja mzee moja akachukua mawe, akayagongagonga ili yavunjike apate jiwe la kuchimbia viazi mwitu. Alipoyagonga aliona yakitoka cheche za moto. Akafikiri sana. Halafu akaweka manyasi makavu karibu na ylle mawe, na akaendelea kuyagongagonga. Mara ylle manyasi yakawaka moto. Kumbe alikuwa amegundua moto kama ulivyoona wewe leo wakati ulipolima huko shuleni.”
Kimwaga akamwambia babu yrke, “Kumbe hata mimik nimegundua moto.” Kisha akaendelea, “Babu, juzi tulipokuwa tunatoka shule tulinyeshewa na mua tukalowa. Tulipofika kwenye samba moja tulijificha chini ya Kilanda kimoja kidogo. Mwenzetu Kimweri akapekechapekecha vijiti viwili vikavu. Mara tukapata moto, tukautumia kwa kukaushia nguo zetu. Je, babu moto ule ulitoka wapi?”
Mzee Lukindo akasema , “Aaa, wewe Kimwaga unadadisi sana. Basi nitakueleza hadithi nyingine. Hapo zamani sana, kabla mimi sijazaliwa, palikuwa na motto moja mtundu sana. Siku moja alitaka kutoboa kigogo kikavu ili atengeneze kidude cha kuchezea. Akachukua kijiti akaanza kupekecha. Kile kigogo kikatoa unga mweusi. Akaendelea kupekecha kwa nguvu sana. Akaona Moshe. Mwisho ule unga mweusi ukashika moto. Akachukua nyasi kavu na kuziweka karibu na ule unga. Nyasi zikawaka moto. Kumbe naye alikuwa amegundua moto.”
Siku nyingine tena, Kimwaga akamweleza babu yrke namna alivyomtazama buibui. Akamuuliza babu yrke, “Je, babu, ule uti ambao buibui hujengea nyumba unatoka wap?” Mzee Lukindo akajibu, “Buibui ni mdudu wa ajabu. Anapotaka kujenga nyumba yrke, hutoa maji kutoka tumboni make. Maji haya yanapotoka nje tu huganda, na anapokwenda huonekana kama uti.”
Babu yrke Kimwaga alipomaliza kusimulia habari za buibui, Kimwaga alikuwa anasinzia kwa sababu siku ile alichelewa sana kwenda kulala. Mzee Lukindo akamwambia, “Sasa mjukuu wangu, Nena ukalale. Nitakueleza hadithi nyingine kesho.” Kimwaga akaenda zake kulala.
Monday, September 6, 2010
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
Mama mkwe Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.
Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam. Mama Kelvin pole sana kwani inaonekana huyo mama mkwe wako hajaelimika vya kutosha. Uzuri wa mwanamke haupimwi kwa kazi za nyumbani pekee, bali kuna mambo mengi na mkwe wako anapaswa kutambua kuwa wewe unafanya kazi hivyo huwezi kukaa nyumbani muda wote na ndiyo sababu ukatafuta msaidizi.
Lakini pia ni vyema ukiwa nyumbani ufanye kazi zilizopo ikiwamo kumpikia mumeo na kumhudumia ipasavyo. Usiwe na hasira za haraka kwa msichana wako wa kazi kwani inawezekana aliulizwa kimtego naye akajibu vizuri tu lakini mkweo akawasilisha kwa mumeo vibaya. Nadhani mumeo pia anapaswa amweleze mama yake kwa upole kuwa wewe unafanya kazi na huwezi kufanya kazi zote za nyumbani. Pia amweleze kuwa huyo msichana wa kazi kamwe hawezi kuwa mke wa mtoto wake.
Naamini mtoto wake akimwelimisha na akawa na msimamo, mama mkwe wako ataelewa au hata kama hataelewa, atashindwa kuendelea kusisitiza anachotaka. Ni vyema pia ukakaa na mshichana wako na kumhoji ilikuwaje hata wakazungumza hayo na mkweo na ukiona kama alichokonolewa basi mtahadharishe akae mbali na mama mkwe na asiwe mwepesi kueleza mambo ya ndani ya nyumba kwa mkweo.
Hata hivyo fanya uchunguzi wako kwa siri na ukiona msichana wako anapalilia ili aolewe yeye, basi ni vyema ukatafuta msichana mwingine wa kazi na huyo kumwondoa ili asije kuharibu ndoa yako. Haina haja kugombana na mtu yoyote kwani naamini huyo mkweo ataondoka na nyinyi mtaendelea na maisha yenu. Pia jifunze kuvumilia kwani wakwe wengine uelewa wao ni mdogo.
Habari hii nimeipata jamii forum na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa Maisha na Mafanikio.
Monday, August 30, 2010
Umejiuliza kwa nini mwanafunzi wa kike anakutaka?
Umejiuliza kwa nini wanafunzi wa kike au wanawake wanafanya ngono? Inawezekana kusiwepo na jibu la moja kwa moja na kwa wewe msomaji wa makala hii labda unaweza kutaja sababu kadhaa kama vile kutafuta watoto, kujiridhisha nafsi zao na hata ishara kuwa wanawapenda wanaofanya nao tendo hilo. Mwandishi Wetu Christine Chacha anafafanua zaidi.
UNAWEZA kuendelea kutaja sababu kadhaa unazozijua lakini ukweli ni huu, wanawake wana sababu nyingi sana zinazowasukuma kufanya ngono tena nyingine unaweza usizijue.
Kwa mujibu wa kitabu kilichochapishwa hivi karibuni kiitwacho " Why Women Have Sex kuna sababu 237 zinazowafanya wanawake kuvutiwa na tendo hili.
Hivi ndivyo wanavyosema wanasaikolojia wawili Cindy Meston na Davis Buss walioandika kitabu hiki kilichopata umaarufu mkubwa wa kupendwa na watu wengi duniani.
Unaweza ukashangaa lakini huu ndio ukweli, sababu nyingi zinazotajwa na wanawake zaidi ya 1000 waliohojiwa hazihusiani kabisa na kitu kinachoitwa mapenzi na kwa zile zinazohusiana basi si kwa uhusiano wa ukaribu.
Kwangu, habari hii niliipokea kwa mstuko kwa kuwa najua hakuna hata mmoja asiyezungumzia kwa nini tumekuwa tukifanya ngono.
Nilichokuja kukimaizi mwishoni ni kwamba sababu zinazowasukuma wanawake kujihusisha na tendo hili zinatofautiana kwa sababu za kiumri na nyakati.
Nitoe mfano kwa wanafunzi wa shule za sekondari hasa ile ya juu, wengi wetu tuliweza kufanya tendo hili kimajaribio, tulitaka tudadisi ladha ya jambo hili hatimaye tukapoteza usichana wetu.
Kwa ngazi ya chuo kikuu, ngono haikuwa tena mchezo wa majaribio bali kitu tofauti, kipi hicho? Wengi tulifaya kama mojawapo ya njia za kujipa raha na kila mmoja alikuwa akifanya.
Muulize mwanachuo yeyote wa kike hatosita kukwambia kuwa njia rahisi zaidi ya kumpata mwanamume basi zungumza naye kuhusu ngono. Huwezi kufeli kama utamkabili kwa kutumia mtego huu. Wapo hata waliokuwa wakilazimika kufanya ngono ili wawe karibu na wanaume ili hatimaye waje kupata alama nzuri katika masomo.
Leo ninapohudhuria katika sherehe za kuwafunda wanawake wanaoolewa maarufu kama kitchen party, ngono huku imechukua sura nyingine. Wanaotarajia kuolewa wanaambiwa ngono ni sawa na kazi ama jukumu lao muhimu pale wanapokuwa kwa waume zao. Na lazima jukumu hili walikamilishe ipasavyo wanapokuwa katika maisha ya ndoa.
Tena jukumu hili ni maalum kwa ajili ya kumfurahisha mume na ilivyo wanatakiwa walifanye kiustadi mkubwa ili wawavutie waume zao ili wasipate mawazo ya kwenda nje kutafuta wanawake wazuri zaidi katika tendo hili. Hapa ngono hailengi kumpa raha mwanamke bali mwanaume.
Kwa mujibu wa kitabu nilichokitaja hapo awali, asilimia 84 ya wanawake walisema wanafanya ngono kuwaridhisha wanaume zao na si kama wanafurahia kwa kiwango kikubwa kufanya hivyo.
Mpaka hapa nikawa hoi, ndipo niliopoamua kutafiti hapa mkoani Dar es Salaama nikitaka kujua kwa nini wanawake wanajihusisha na tendo la ngono.
Visasi
Kumbe kulipiza kisasi kunaweza kuwa sababu ya wanawake kujiingiza katika tendo la ngono hasa pale wanaposalitiwa na wapenzi wao. Wengine hutaka tu kuwarusha roho wanaume zao kwa kuwapa hisia kali za wivu.
Martha Peter (29) anayefanya kazi za usanifu kurasa ni mfano mzuri wa wanawake walioamua kufanya ngono kulipiza kisasi baada ya kusalitiwa na wapenzi wao waliowachunuku kwa kiwango kikubwa.
"Nilitaka alipe kwa mabaya aliyonitendea, nilitaka nimkabili katika njia ambayo ingemuumiza sana,’" anasema
Nini alichokifanya kumuumiza mpenzi wake wa zamani? Anasema, "Nilijua ukaribu aliokuwa nao na kaka yake wa kufikia hivyo nikatembea naye, kilichotokea ni vurumai kubwa katika familia yao, baadaye nikaachana na wote."
Kusambaza magonjwa
Wapo wanaofanya ngono kwa lengo la kusambaza magonjwa waliyo nayo. Nakumbuka niliwahi kusoma habari moja kuhusu mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu fulani aliyetenmbea na wanaume zaidi ya 100 kwa lengo tu la kuwaambukiza ugonjwa wa Ukimwi.
Alipoulizwa alisema alifanya hivyo kulipiza kisasi baada ya yeye kuambukizwa na mpenzi wake wa kiume waliokuwa wakisoma pamoja chuoni.
Ngono kama njia ya kujifurahisha
Leo wanawake wanakataa ule usemi eti kwa sababu za kijinsia wao hufanya ngono kwa kuwa tu wanawapenda wapenzi wao na kwamba wanaume wao ndio pekee wanaolichukulia tendo hilo kama njia ya kujipa raha.
Ilivyo hata wanawake nao wanapenda kufanya ngono kwa kuwa wanaburudika kufanya hivyo. Tena kwa wanawake vijana hii ni njia nzuri ya kuburudika na kujiliwaza kimwili. Kama ilivyo kwa wanaume, hii nayo ni raha na wala hawajuti kufanya hivyo.
" Nafanya ngono kwa sababu nataka kufanya hivyo, ngono inaburudisha na kusisimua," anasema Bella Roman, Meneja wa Fedha wa kampuni moja nchini.Anaongeza kwa kusema:
"Tupo katika jamii huru, sina sababu nyingine ya kufanya ngono.
Kwa nini nami nisifanye nikafurahi kama wanaume."
Roman (34) anashangaa kwa nini jamii inakubali wanaume kupenda ngono lakini ikitokea kwa wanawake wanashukiwa kwa sababu kadhaa kama vile kuitwa makahaba. Anauita huu kuwa ni mtazamo wa unaopaliliwa na hisia za mfumo dume.
“Inawafanya wanawake kujihisi vibaya pale wanapotaka kutimiza matakwa yao ya kufanya ngono. Naweza kufanya ngono kama kujiridhisha moyoni na wakati huo huo nisiwe kahaba, jamii lazima ilikubali hili,†anatetea mtazamo wake.
Roman anakiri kuwa ana marafiki kadhaa wa kiume na wote anafanya nao ngono pale anapojisikia. Na wanaume hawa wote wanajua kuwa hawana mkataba naye kwa kuwa anawatumia kutimiza haja zake kingono.
Kumchunga mwanaume
Baadhi ya wanawake akiwemo Aysha anayesoma chuo kikuu wanaamini kuwa ukitaka mwanamume awe wako pekee basi usimyime raha.
"Nimekuwa nikifanya ngono na rafiki yangu wa kiume ili kumweka karibu nami katika uhusiano na asijaribu kunitoroka. Niliamua kufanya hivi baada ya kuomba ushauri kutoka kwa marafiki walioniambia huwezi kumchunga au kummiliki mwanamume kwa kumpenda tu, waliniambia nitumie ngono kumweka katika himaya yangu," anafafanua.
Aysha hana jinsi amekuwa akifanya ngono ili kumridhisha mpenzi wake ambaye hakika ndiye aliyekuwa kinga’ng’anizi wa kutaka kufanya kitendo hicho. Na kwa kuwa hataki kumpoteza Aysha hana jinsi ila kujisalimisha.
Anawakilisha wanawake wengi ambao wamekuwa wakifanya mgono kwa kuwa kwa namna fulani wanalazimishwa na wapenzi wao japo wao wenyewe hawapo tayari.
Wengine huruma huwaponza, kwa nini wasiwape unyumba wanaume wanaowazengea kwa muda mrefu wakiomba kupewa bahati ya kukutana nao kimwili? Kwa wengine hawa wana lao jambo, wanataka ngono na wanaume ili kujua tu ukubwa wa maumbile walioyajaaliwa.
Fanya ngono umsahau wa zamani
Kwa hili Aysha ana haya ya kusema: " Baadhi ya marafiki zangu nami nikiwemo baadhi ya nyakati tunafanya ngono kama njia ya kuwasahau wanaume wa zamani. Sote tunaamini njia bora ya kumsahau mwanamume ni kuanza uhusiano na mwanaume mwingine."
Huna haja ya kuomba ngono inatosha
Baadhi ya watu wanafikiri wanawake wanaofanya ngono kwa lengo la kutaka kupewa chochote ni makahaba, si kweli. Ukweli ni kuwa hata walio katika ndoa na aina nyingine za mahusiano ya kimapenzi wanatumia ngono kama silaha ya kuwalazimisha wapenzi wao wawape yale wanayoyataka.
"Ninapotaka kitu fulani kwa rafiki yangu basi nahakikisha usiku nampa raha zote kisha asubuhi inayofuata namwomba kitu hicho, najua hawezi kusema hapana,’" anasema Anna Tagaru
Hata kwenye maeneo ya kazi wanawake wamekuwa wakitumia njia hii kupata nafasi za juu au kupendelewa na wakubwa.
Kinachofanyika mwanamke anaanza uhusiano na wakubwa katika utawala na hatimaye kama ni mshahara aliotaka au cheo vinaongezeka.
Kwa Tagaru hili kwake si tatizo kama anavyobainisha:"Nawajua marafiki kadhaa wanaotumia ngono kujipatia fedha, si makahaba lakini ni wanawake wanaohakikisha wanapata wanavyovitaka kwa gharama yoyote."
Anasema ana marafiki kadhaa waliotoa miili yao kwa wanaume na kufanikiwa kulipiwa pango katika nyumba wanazoishi, kulipiwa bili za bidhaa na kupewa zawadi za gharama kubwa.
“ Wanaume wanalichulia tendo hili kwa uzito mkubwa na wapo tayari kufanya chochote ili walipate. Kwa kufanya hivi wanawapa wanawake nguvu ya kuitumia ngono kama njia ya kutaka wanayoyataka," anaongeza Tagaru, mama wa mtoto mmoja.
Aidha anasema wakati mwingine anatumia ngono kama njia ya kumpa pongezi au kumwadhibu rafiki yake. Atamfariji kimwili pale anapofanya jambo zuri na pale anapoboronga asahau kama kuna kinachoitwa ngono.
Kuongeza uzao
Hii ni sababu maarufu ya wanawake kufanya ngono na hata dini zimekuwa zikisisitiza hili kuwa mojawapo ya malengo makuu ya kufanya jimai kwa wanandoa.
Hivi ndivyo ilivyo japo leo hii sababu zimekuwa nyingi huku baadhi ya wanawake wa kisasa na wasomi wakitaka tu watoto lakini si kwa kupitia ndoa.
Sikiliza anachosema tena Tagaru"Nilipogundua muda unayoyoma, nilichofanya ni kumtafuta mwanaume anayeweza kunizalisha mtoto mwenye sifa ninazotaka."
Kwa nini tusiwe kama wengine?
Kwa miaka mingi wanaume wamekuwa wakiichukulia ngono kutimiza shauku zao na hata kushindana wenyewe kwa wenyewe kujua nani ana nguvu zaidi. Wapo wanawake nao wanasema kwa nini asiwe kama wanaume?
"Nilipokuwa shuleni, marafiki zangu walikuwa wakizungumzia jinsi walivyotembea na wanaume na kuona uzoefu wa tendo hili, nami nikajaribu," anasema Safia Abdul anayefanya kazi kitengo cha huduma kwa wateja katika kampuni moja ya simu.
Anasema alichotaka ni kuona kwa namna gani angeweza kufika kileleni jambo alilokuwa akilisoma tu vitabuni na hata kuhadithiwa na wenzake.
Alipata alichokitaka kama anavyobainisha: "Nilijaribu kufanya ngono na wanaume kadhaa ili nijaribu kufikia kileleni, nilifanya hivyo hadi nikafanikiwa."
Ushindani wa ngono
Hii inaweza ikawa sababu ngeni lakini ipo na baadhi ya wanawake wanaitumia. Hapa nakusudia kundi la wanawake wanaotoka kwenda kumtafuta mwanaume mmoja mzuri na kisha kila mmoja kufanya awezalo kuhakikisha anafanya naye mapenzi.
Safia anasimulia kuwa hili liliwahi kutokea kazini kwake pale wanawake kadhaa walipokuwa wakimtaka mwanaume mmoja aliyeonekana kuwa mzuri wa umbo na aliyejaaliwa fedha mfukoni. Kila mwanamke akiwemo yeye alimtaka.
“Alikuwa ni ndoto ya kila mwanamke, wote tulitaka kujua atamtongoza nani. Nilipoona kila mtu anamtaka niliamua niwe wa kwanza kumpata kwa gharama yoyote, nilijiuliza hivi kuna njia nyingine ya kumpata zaidi ya ngono?’’
*Makala hii ya Christine Chacha kwa mara ya kwanza ilichapishwa katika gazeti la The Citizen toleo la Novemba 14 ikiwa na kichwa cha habari Why Women Have Sex na imetafsiriwa na Abeid Poyo kwa ajili ya wasomaji wa Kiswahili.
Sunday, August 1, 2010
Malezi ya Watoto Katika Mpango wa Mungu!!!!
Malezi bora kwa watotoKwanza kabisa yakupasa uifahamu thamani ya mtoto ambaye Mungu amekupatia. Umhesabu kama zawadi toka kwa Mungu na sio mzigo hata kama haukupangilia kuwa naye kwa wakati huo maana Mungu alishamfahamu kabla hata hajazaliwa. Katika vitabu vya Yeremia na Zaburi tunaona kuwa Mungu anayafahamu maisha ya kila mtoto kabla hata mimba yake yaijatungwa.
Yeremia 1:5a Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;
Zaburi 139:16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
Tambua kuwa Mungu amekuheshimu na kukupendelea kwa kukupa watoto/ mtoto ili umlee na kumtunza, kwa hiyo yakupasa umpende na kumlea kwa hekima ya ki Mungu na hata siku moja usimuone kama mzigo au kumsema vibaya kwa watu wengine. Hata kama mtoto wako atakuwa na mapungufu kitabia wewe kama mzazi unayemjua Mungu na unaitambua thamani ya mtoto uliyenaye, usimseme vibaya kwa watu bali umuombee, kumuelekeza kwa upendo na kumuonya kwa busara. Fahamu kuwa mtoto wako anathamani kubwa mbele za Mungu naye ndiye anayemjua vyema. Wewe kama mzazi unawajibika mbele za Mungu kwa jinsi unavyomlea mtoto wako ha hivyo yakupasa kujitoa kwa uaminifu katika kumlea kwa upendo na uvumilivu wote.
Tafuta kulifahamu neno la Mungu na kuitafuta hekima ya kiMungu katika malezi ya mtoto wako kuliko hekima ya mwanadamu. Jifunze Mungu anasema nini kuhusu malezi ya watoto na uyafuate hayo kwa uaminifu hata kama kibinadamu yanaonekana yamepitwa na wakati. Tumia muda kwenye maombi kumwombea mtoto wako na maisha yake ya kimwili na kiroho ili aweze kuongozwa na Mungu siku zote za maisha yake. Mfundishe mtoto wako tangia akiwa na umri mdogo habari za Mungu na kweli yote ya neno la Mungu. Katika maisha ya siku hizi ni kawaida kuona baba na mama wote wanafanya kazi nje na nyumbani hali inayopelekea watoto kubaki na mlezi muda mwingi wa mchana. Hali hii usipoiwekea mikakati katika malezi ya mtoto wako kiroho inaweza kuleta madhara makubwa hapo baadaye. Hakikisha muda unaoupata kuwa na mtoto wako unautumia kumweka karibu nawe na kumfundisha habari za Mungu.
Kuna njia nyingi ambazo mzazi unaweza kuzitumia katika kumfundisha mtoto wako habari za Mungu kwa ufanisi kuanzia katika umri mdogo kabisa. Anza kwa kuomba na mtoto wako wakati wote iwe ni asubuhi, wakati wa kula, usiku na wakati mwingine wowote ambao unafanya maombi. Mfundishe kuwa ni muhimu kuomba kabla ya kula na kulala na pia asubuhi baada ya kuamka. Kwa kufanya hivi mara kwa mara basi taratibu ataaza kuona kuwa maombi ni kitu cha muhimu na kadiri anavyokuwa mkubwa ataendelea na tabia ya maombi. Biblia katika kitabu cha mithali inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).
Msimulie hadithi za biblia kwa njia ya kufurahisha huku ukiwa unamsomea biblia. Mwanzoni itakuwa ngumu kukuelewa lakini kadiri unavyoendelea na kurudia rudia mara kwa mara itakaa ndani yae na itamjengea hamu ya kusoma biblia ili ajue kwa undani zaidi habari ambazo unamsimulia pale atakapokuwa anajua kusoma. Ukiweza mtafutie biblia ya watoto yenye hadithi fupifupi za biblia kwa picha. Waweza pia kutafuta video za hadithi za biblia kwa watoto na mkawa mnaangalia pamoja naye huku ukimsimulia , pamoja na kupata nafasi ya kumfundisha neno la Mungu pia utapata muda mzuri wa kufurahi na mtoto wako na kuwa karibu naye.
Mfundishe kuonyesha shukrani pale mtu anapompatia kitu au kumtendea jambo jema. Hata kama hajui kuongea mwambie sema asante hii itamfundisha kuwa ukitendewa jambo ni lazima kuonyesha shukrani. Mfundishe kumshukuru Mungu kwa kuamka salama, kupata wazazi wanaomlea vyema, kununuliwa michezo mbali mbali, n.k Moyo wa shukrani utamsaidia kumjua Mungu zaidi na atakuwa anatafuta mema ya kumshukuru Mungu kila siku. Ishi maisha ya upendo, furaha, amani na ukarimu wakati wote ili mtoto aone uhalisia wa Mungu katika maisha yako.
Nenda na mtoto wako kanisani kila jumapili na uwe unamwambia kwanini unaenda kanisani. Usisahau kumpa sadaka naye awe anatoa na umweleze kwa nini tunatoa sadaka kuwa ni njia ya kumshukuru Mungu kwa vingi alivyotupatia. Kumbuka kila mara kumkumbusha upendo wa Mungu, wema na ukuu wa Mungu.
Malezi ya mtoto ni huduma inayojitosheleza, ni jukumu ambalo umuhimu wake ni mkubwa sana na pale unapokosea matokeo yake kuyabadilisha huwa ni kazi ngumu sana. Mwamini Mungu katika jambo hili na mtegemee na kumtazamia yeye pekee, kama alivyokupa mtoto atakuwezesha kumlea katika njia impasayo.
–Magreth Riwa–




