Showing posts with label afrika. Show all posts
Showing posts with label afrika. Show all posts

Saturday, April 23, 2016

AFRIKA- KUMEKUCHA.....


NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA.... PAMOJA TUTAFIKA......KAPULYA

Tuesday, April 21, 2015

SWALI LA LEO:- UNAJUA NI KABILA GANI HUTUMIA MBINU/UBUNIFU HUU NCHINI TANZANIA?

Hakika watu ni wabunifu ...ila binafsi ningependa kuwabeba mgongoni..au wewe mwenzangu unasemaje?

Friday, July 18, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA UKIPATA WASAA SIKILIZA KIPANDE HIKI....




Au tu labda tusikiliza na hii pia

MUNGU IBARIJKI AFRIKA YETU..PAMOJA DAIMA . IJUMAA NJEMA

Thursday, June 26, 2014

NIMEIPENDA RAMANI HII YA AINA HII YA AFRIKA...UBUNIFU HUO!!!

RAMANI YA AFRIKA
Imetengenezwa kwa kubandikizwa majani ya ndizi yaani ni asili kabisa ...ngoja niimbe na kawimbo haka ka afrika yetu:-
Mungu ibariki Afrika, Wabariki Viongozi wake,
Hekima Umoja na Amani, Hizi ni ngao zetu, Afrika na Watu wake,
Ibariki Afrika, Ibariki Afrika, Tubariki watoto wa afrika.
 
SIKU IWE NJEMA KWA WOTE...TUPO PAMOJA DAIMA

Monday, May 19, 2014

JUMATATU YA LEO TUANZE NA CHANGAMOTO HII KUHUSU NCHI ZETU ZA AFRIKA!!!!

SWALI:- Je? ni nchi gani/zipi  haina/hazini  herufi A katika bara la Afrika?
NAWATAKIA KILA LA KHERI. PAMOJA DAIMA!!!

Friday, April 4, 2014

Tuesday, February 25, 2014

VAZI LA KANGA NI MUHIMU KWETU TUSISAHAU VAZI HILI NA TULIKOTOKA: KANGA!!

 Kanga ya kwanza imetegenezwa mwaka 1870 na mwanamke kutoka kisiwa cha Zanzibar.

Kanga ni kitambaa chenye umbo la mstatili na rangi mbalimbali. Kipimo chake cha upana ni 44 inchi hivi na kipimo chake cha urefu ni inchi 60 hivi.
Kwa watu wa Afrika ya Mashariki, hasa wanawake, kanga ni  nguo muhimu sana. Mara kwa mara, wanawake wanavaa kanga wakati wa kupika, kusafisha nyumba, kuteka maji, na kadhalika.
Tena, kanga zinavaliwa na wanawake kwenye arusi, kwenye msiba, nk. Kanga si nguo tu. Matumizi ya kanga ni mengi. 
Kama kanga hii isemavyo TUSISAHAU KWETU...!!

Friday, December 6, 2013

AFRIKA TUMEPATWA NA MSIBA BABU YETU NELSON ROLIHLAHLA MANDELA HATUNAYE TENA.

Nelson Mandela wakati wa uhai wake
 
1918-2013....ni pengo kubwa umeacha. Utakumbukwa daima. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema. Amina.


TUTAKUKUMBUKA DAIMA MKOMBOZI WETU. AMINA

Monday, September 30, 2013

JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TISA INATUKUMBUSHA AFRIKA....TANZAN IA NA MALIASILI YAKE...MBUGA!!!


Nawatakieni wote mwanzo mwema wa wiki hii. Binasi  nina furaha isiyo kifani leo kwani rafiki yangu mpendwa tumeongea leo..tulikuwa tumepoteana miezi kadhaa. AHSANTE MUNGU KWA HILI.

Friday, September 6, 2013

NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA ......SEHEMU FUALANI NDANI YA AFRIKA...



NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMA WA JUMA TUWE NA AMANI NA KILA LA KHERI KWA KILA KITU TUKIFANYACHO...NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA....Sisi sote ni ndugu na ni watoto wa baba mmoja ....Kapulya

Friday, May 10, 2013

UMETOKA MKOA UPI HAPA?

1. Dar es salaam - Utapeli
2. Arusha - Heka heka
3. Mbeya - Matukio
4. Tanga - Majini
5. Dodoma - Ombaomba
6. Mwanza - Fujo
7. Kagera - Misifa
8. Rukwa - Uchawi
9. Kilimanjaro - Ujanja
10. Mara - Ukatili
11. Kigoma - Ubishi
12. mtwara - Umaskini
13. Ruvuma - Ugoni
14. Singida - Upole
15. Tabora – Majungu
16. Shinyanga - Miujiza
17. Morogoro = Starehe

18. Iringa - Ukorofi
19.Zanzibar ???
 20.Pemba ??
NAWATAKIENI MWANZA MWEMA WA MWISHO WA JUMA...

Wednesday, March 20, 2013

TANZANIA NCHI YANGU ...NAKUPENDA TANZANIA

Nitakutangaza nchi yangu tanzania,nakupenda Tanzania nchi yangu Tanzani na najivuna kuwa mTanzania.JUMATANO NJEMA KWA WOTE...

Thursday, December 6, 2012

JINSI WATOTO WA KIKE WANAVYOJIFUNZA MAISHA ...

....mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..ila kuna wakati katika jamii yetu huwa tunazidisha kidogo..mtoto anakuwa kama mtu mzima kabisa. Kwa maana hiyo anakosa ule muda wa kuwa mtoto. Ila tumejifunza mengi na tumekuwa kwa kiutu uzimauzima si kama sasa..au wenzangu mliopitia maisha haya mnasemaje?..Duh!  siku zinakimbia tayari leo ni Alhamisi ya tarehe 6/12/2012..KILA LA KHERI WANDUGU!!!!

Friday, October 19, 2012

BINTI ACHUMWA KISU NA MAMA KWA TUHUMA ZA "KUTEMBEA " NA BABA!!

Mfanyakazi wa ndani, Angel Lema (22) amechomwa kisu kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba mwenye nyumba anakofanya kazi.

Angel anayefanya kazi za ndani katika kijiji cha Leganga wilayani Arumeru mkoani Arusha, inadaiwa alifanyiwa unyama huo na mama mwenye nyumba baada ya kumhisi ‘kutembea’ na mumewe.

Akizungumzia tukio hilo jana, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Dkt. Aziz Msuya, alithibitisha kumpokea msichana huyo akiwa na hali mbaya, kutokana na jeraha tumboni Oktoba 8. Dkt. Msuya alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi, ilibainika alichomwa kisu tumboni na mwajiri wake.

“Lakini binti huyu tulipomhoji, kwanza alikataa na kudai kujichoma mwenyewe, ila baadaye ilibainika alichomwa na mama mwenye nyumba kwa hisia za kufanya mapenzi na mumewe na kumeonya asimtaje kuwa ndiye amemchoma kisu,” alidai.

Dkt. Msuya alisema kutokana na jeraha kuwa kubwa, walihofia usalama wa utumbo wake na kulazimika kumfanyia upasuaji wa tumbo ili kuangalia usalama zaidi ndani, “Tulipomfanyia upasuaji tuligundua hajaathirika utumbo na ulikuwa salama, tukamshona,” alisema Dkt. Msuya na kuongeza: “Lakini cha ajabu kidonda kikiwa kibichi, msichana huyo alitoroshwa usiku Oktoba 14, kitendo kilichotushangaza,” alisema Dkt. Msuya.

Alisema baada ya kugundua hilo, walitoa taarifa Polisi, ili wachunguze tukio hilo ili kuokoa maisha ya msichana huyo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas baada ya kupigiwa simu na gazeti hili, kuuliziwa tukio hilo, alisema hana taarifa, “Mimi sina taarifa, lakini tukio hilo linaweza kuwapo… kwa kuwa niko mbali huku Moshi kwenye maziko ya Kamanda Barlow (Liberatus), bado sijapata muda wa kufuatilia taarifa za huko na kupata habari zaidi, lakini pia huku mawasiliano yanasumbua sana,” alisema.
Kamanda Sabas aliahidi kulifuatilia suala hilo mara atakapopata nafasi na kutoa taarifa.
---
Habari imeandikwa na John Mhala, HabariLeo, Arusha

Monday, October 15, 2012

Wednesday, October 3, 2012

Mwanamke maarufu kuliko wote duniani....

Kila mtu akiulizwa ni mwanamke gani maarufu au aliye ngangari zaidi, kama anatafakari vizuri, atasema kuwa ni mama yake, hasa kama alimlea kwa uadilifu. Pengine mwingine atasema ni mkewe, kutegemea na namna wanavyoishi kwenye uhusiano wao wa kindoa.
Lakini, linapokuja suala la mwanamke ambaye hakuhusu, ambaye unaamini au kudhani kwamba, ndiye ngangari zaidi hapa duniani, hasa katika siasa na uchumi, inaweza kuwa mtihani mgumu kwako kutoa jibu sahihi.
Ni kweli, unaweza kutoa jibu, lakini siyo lazima jibu lako liwe sahihi.
Kama ni sahihi, itakuwa ni kwa sababu tu, unamjua huyo uliyemtaja, na wengine huwajui.
Hivi ndivyo ambavyo imetokea kwenye kura iliyofanyika ya kuwataja wanawake wanaodhaniwa kuwa maarufu hapa chini ya jua kwenye nyanja ya siasa na uchumi.
Karibu kila Mtanzania angetarajia kuwa wakitajwa wanawake 100 duninai ambao ni maarufu kwa sasa, huenda Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro angetajwa. Matarajio hayo yangetokana na sababu mbalimbali.
Kwanza, unaibu wa Katibu Mkuu wa UN, siyo nafasi ndogo hapa duniani. Pili, kwa mwanamke kutoka Afrika tena kwa nchi ambayo ni miongoni mwa zile maskini kabisa, kushika nafasi hiyo, ni jambo la kinasibu zaidi kwa mitazamo ya mgawanyo wa dunia. Tatu, ingetarajiwa naibu atoke angalau bara Amerika, kwani Katibu Mkuu anatoka Asia, bara maskini karibu sawa na Afrika kwa uwiano.
Kwa bahati mbaya, jarida maarufu duniani kwa kufanya tathmini za viwango mbalimbali kuanzia utajiri, uzuri na umaarufu wa binadamu, la Forbes linaonesha katika taarifa zake za wiki mbili zilizopita kwamba, Migiro hayumo kwenye orodha ya wanawake 100 maarufu duniani katika nyanja za uchumi na siasa.
Kutoka Afrika ni wanawake wawili tu walio kwenye orodha hiyo. Kwanza ni , Waziri Mkuu wa Msumbiji, ambaye anashikilia nafasi ya 89 diuniani kwa umaarufu. Halafu anafuatiwa na Rais wa Liberia, , ambaye anashikilia nafasi ya 100.
Hii ina maana kwamba, Waziri Mkuu wa Msumbiji ni maarufu zaidi duniani, ukilinganisha na Rais wa Liberia, , nchi iliyoweka historia duniani kwa vurugu kubwa za kisiasa, zilizopelekea marais wawili kuuawa kinyama na mmoja kupamba vyombo vha habari dunia kuhusiana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Rais Ellen Johnson ndiye Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, lakini anakuwa Rais baada ya uchaguizi huru na wa haki uliofuatia umwagikaji wa damu nyingi ya kutosha. Bado huyu anashikilia nafasi ya 100, wakati Waziri Mkuu wa Msumbiji anashikilia nafasi ya 89!
Hapa ndipo ambapo matokeo haya ya jarida la Fobes yanatia mashaka. Ni kweli kwamba, uchaguzi huo umefuatia kura kutoka kwa watu duniani kote.
Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti.
Katika orodha hiyo kuna majina ya wanawake ambayo huenda kwa umaarufu, akili ya kawaida inaweza kukuonesha kwamba, hawawezi kumzidi Asha Rose Migiro. Hebu kwa mfano, tuchukulie mwanamke kama , ambaye ni mtendaji kuuu wa Benki ya Leumi ya Israeli. Je, huyu mama uliwahi kumsikia au hata kumsoma kwenye chombo chochote cha nje? Huyu anashikilia nafasi ya 83 kwa umaarufu.
Huenda inabidi Afrika nayo sasa iwe na utaratibu wa kutafuta maoni ya dunia nzima ambapo waafrika nao watashiriki sawa kusema kuhusu nini wanaona, sawa na watu wengine duniani. Inaonekana wazi kwamba, hata viwango vya umaskini vinavyopangwa kutoka Ulaya na Marekani ni kwa vigezo ambavyo havifutu na kukidhi ukweli mkubwa zaidi unaowahusu Waafrika.
Kwenye orodha hiyo, inaonekana kuwa, Rais wa Ujerumani, , ndiye mwanamke maarufu zaidi duniani. Wu yi, ambaye ni makamu mwa Rais wa China anashikilia nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Temasek Holdings, ya Singapore.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anashikilia nafasi ya nne.
Wengine ni , mwenyekiti wa kampuni ya PepsiCo ya Marekani. Namba sita ni , Rais wa India. Namba saba imeenda kwa, mtendaji Mkuu wa kampuni ya Anglo American ya Uingereza.
Nafasi ya nane anaishikilia ambaye ni mwenyekiti, kampuni ya Archer Daniels Midland ya marekani.
Namba tisa ni , mwenyekiti kampuni ya Kraft Foods ya Marekani, na namba kumi ni , Mtendaji Mkuu wa Alcatel-Lucent ya Marekani.
anashikilia nafasi ya 21, wakati Malkia Elizabeth anashikilia nafasi ya 23.
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, , anashikilia nafasi ya 25.
Kama orodha hii ya Forbes inaonesha ukweli na uhalisia wa umaarufu unaotokana na michango ya wanawake katika jamii zao au jamii ya dunia, ina maana kwamba, kwa Afrika, wanawake hawajafanya lolote kwa jamii zao na jamii ya dunia.
Lakini, huo utakuwa pia ni uongo mkubwa, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wanawke hapa Afrika ambao wamejitahidi kwa viwango vya kimataifa kubadili hali za watu wengine katika jamii.
Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika. Orodha hiyo ni wanawake maarufu duniani katika nyanja za siasa na uchumi, ambapo ni uongo kudai kwamba, kati ya wanawake 100 duniani, Afrika inaambulia nafasi mbili, tena za mwisho.
Hii ina maana dunia inawatambua wanawake wawili tu Afrika katika nyanja hizo? Ndiyo maana naamini kwamba, Migiro angepaswa kuwemo kwenye orodha hiyo, kama kweli inakagua mambo kwa uhalali.
Lakini, mtu akikagua orodha hii tena na tena anaweza kupata picha kubwa zaidi na kuikubali, ingawa baadaye anaweza kuipinga. Ni matokeo ya kura yenye utata. Kwa mfano, Hilary Clinton anafahamika, kama ilivyo kwa Oprah Winfrey, lakini nao wametupwa hadi nafasi za 20, kama ilivyo kwa Malkia Elizabeth.
Lakini, hapohapo kuna majina kati ya namba 11 hadi 20, ambayo ni ya wanawake ambao hata watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wazuri wa vyombo vya habari vya nje hawajawahi kuwasikia.
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, hasa uchumi, vyombo vya habari vya Magharibi, bado vinaitendea Afrika kama vile ni bara wanamoishi wanyama, badala ya binadamu.
Vyombo vyetu vya habari, kwa bahati mbaya, navyo ni kama sauti za vyombo vya habari vya Magharibi.
Vikifanya tafiti zao, vinafanya kwa njia finyu na iliyofubaa, isiyoweza kuwahamasisha Waafrika.

Hii iliandikwa kwenye gazeti la jitambue iliandikwa na Hayati Munga Tehenan.

Wednesday, May 16, 2012

Wanafunzi wanasomea vibanda vya nyasi!!

Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUTEMBELEE WILAYANI NAMTUMBO.ELIMU NIMEIPATA HABARI HII  Albano Midelo Haya KARIBUNI. 



 Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi
 SelousWilayani Namtumbo wakiwa darasani.

WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.
Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi 296 wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi.
.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.
Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .
Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.
Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu .
“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’,alisema.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa Wilayani
Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga,Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini,Kidagulo,Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’,alisisitiza.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi .
“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’,alisisitiza.

TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO KWA JINGINE LA ZAMANI!!

Saturday, May 12, 2012

RUDI NYUMBANI AFRIKA/TUSISAHAU TULIKOTOKA!!



Mmmhh nimepata hamu kweli kweli hapa ya kula vyakula hivi  mpaka naanza kufikiria kuwa ...naacha  bwana  labda ntasema siku nyingine. Je? nawe umepata hamu kidogo? ngoja Baba gaston amalizi na RUDI NYUMBANI AFRIKA!!!!
JUMAMOZI NJEMA. NYUMBANI NI NYUMBANI TUSISAHAU TULIKOTOKA.!!!!

Wednesday, May 9, 2012

JIONI NJEMA NA :-WANAWAKE WA SHOKA/ WANAWAKE NA VILEMBA ("WRAPS")

 Dada Mija wa http://damija.blogspot.se.
 Mama Ana Tibaijuka.
Na Winnie Mandela, aliyekuwa mke wa Mstaafu Rais Nelson Mandela.
JIONI NJEMA!!!