Showing posts with label mchezo. Show all posts
Showing posts with label mchezo. Show all posts

Thursday, October 31, 2013

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUUFUNGE MWEZI HUU WA KUMI KWA UBUNIFU WA MCHEZO HUU!!!

Napenda kuwatakieni wote mwisho wa mwezi huu wa kumi. Naamini umekuwa mwezi mzuri kwa wengi na kwa wale walikuwa na majukumu kupita kiasi basi nawaombeeni mwezi uanzao kesho uwe mzuri. NAWATAKIENI WOTE MWENZI MPYA WA KUMI NA MOJA UWE MZURI NA WENYE AMANI NA FURAHA. MWAPENDWA WOTE....KAPULYA

Monday, July 23, 2012

PICHA YA MWEZI:- KUJIFUNZA MAPISHI (KUJIPIKILISHA)!!

Picha hii inanikumbusha mbali sana, jinsi ya kujifunza kupika MAPISHI. Eee bwana weee basi hapo ndiyo hapo hapo pa  kujifunza maisha baba na mama...Je wewe msomaji uliwahi kucheza mchezo huu?.

Thursday, September 2, 2010

Tunaomba msaada wenu:- Ni vipi mchezo huu wa Bao/nchua uunachezwa?


Bao/nchua!!
Wakati nipo likizo na mpaka sasa kuna mvua kila siku na hata kunasababisha mafuliko sehemu fulani fulani. Sasa mimi na familia yangu baada ya kuona hatuwezi kufanya michezo mingine ya kuwafurahisha watoto tukakumbuka tuna bao/nchua ambayo tuliinunua Tanzania. Tukachukua kila tukijaribu kucheza ubongo haukumbuki kanuni inakuwa vipi. Nikaona mmmhhh! kuuliza si ujinga aulizaye anataka kujua na umoja ni uwingi. Kwa hiyo nimeona niwaulize je ni vipi kanuni inakuwa? Tutashukuru sana kama mkitusaidia.

Sunday, April 19, 2009

JE? UMEGUNDUA HAPA NI NINI KATIKA PICHA HII?

Siku hii ilikuwa ni siku ya kupita kwa ustadi ili hii picha isianguke. Na kulikuwa hamna amani kwani ilichukua siku nzima. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

Friday, October 31, 2008

SWEDEN NA FINLAND


Natumanini wote mnajua huu mchezo unaitwa ishockey