Habari hii nimetumiwa na kaka Mjegwa.....
-------------------------------------------------------------------------------------
Ndugu zangu,
Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.
Ndugu zangu,
Ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri, hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.
Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.
Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ' Wao Wakristo' na ' Sisi Waislamu'. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ' Nchi Yetu' na maslahi yake.
Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.
Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).
Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.
Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.
Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.
Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.
Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.
Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.
Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.
Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.
Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0788 111 765, 0754 678 252
http://mjengwablog.com
Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts
Saturday, October 20, 2012
Saturday, August 18, 2012
Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania....!" Na Maggid Mjengwa
..... Hatuwezi, Hatuwezi!... Mchakamchaka, Chinja, Mchaka mchaka, chinja!
Ndugu zangu,
Utotoni niliwasikia kaka na dada zangu wakiimba wimbo huu wa mchakamchaka uliojaa hisia za utaifa. Ni kwenye mchakamchaka wa shuleni kila asubuhi.
Naam, hata wakati huo kulikuwa na utata wa masuala ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi . Zilikuwa ni enzi za Rais Kamuzu Banda.
Na Watanzania hatukuwa na ukame wa nyimbo za kebehi dhidi ya Banda. Mwingine uliimbwa hivi; " Kipara cha Banda kina ukoko!" Hakyamungu. Hata wakati huo kulikuwa na harufu ya vita baina ya ndugu wawili; WaMalawi na WaTanzania. Maana, ukweli sisi ni ndugu wa damu.
Kuna hata simulizi za kweli za Watanzania upande wa pili wa Ziwa Nyasa waliokesha kusheherekea Uhuru wa Malawi. Hivyo basi, tunaweza kabisa kidiplomasia kutamka, kuwa "Jambo la Malawi ni letu!" Ndio, shida yao ni yetu, furaha yao ni yetu.
Na tushukuru kuwa JK wetu ni mwanadiplomasia. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa JK anaweza kutuingiza katika ' Vita vya kiwendawazimu' dhidi ya jirani na ndugu zetu wa Malawi.
Na picha hiyo hapo juu inaongea; JK na JB ( Joyce Banda), wanazungumza kwa furaha kama ndugu. Wawili hao hawatoi nafasi kwa wachonganishi wale wa enzi za ugomvi wa utotoni. Maana, utotoni ilikuwa hivi, kaka zetu walipotaka kufurahia wadogo zao tukipigana makonde, walisubiri pale mmoja anapomkasirikia mwenzake. Haraka atatokea kaka na mchanga mkononi. Atatamka kwa mmoja kati ya wawili walio mbele yake;
" Haya, puta mchanga wangu kama kweli wewe ni mwanamme!" Nani asiyetaka kuwa mwananme? Atauputa mchanga. Kisha kaka anamgeukia mwingine; " Haya sasa, nilipie ng'ombe wangu!".
Kulipa ng'ombe ilikuwa na maana ya kuanza kurusha konde. Na hapo ugomvi ulianza rasmi!
Na kuna miongoni mwetu wenye kutamani vita. Anayetamani vita ni mtu mjinga. Mwalimu alipata kutamka; " Vita si lelemama". Na katika dunia hii inasemwa; Chagua vita vyako. Vita vingine havina lazima ya kupiganwa.
Na tofauti zetu na Malawi zinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kama anavyoonekana JK pichani akiongea na dada yake; JB- Joyce Banda.
Na wala hatuwahitaji tena akina Moses Nnauye kututungia nyimbo za Mchakamchaka. Eti twende tukiimba; " Banda ( Joyce) Wa Malawi, Katuvalia Kitenge Cha Ngozi Ya Mamba, Kututishia Watanzania, Hatuwezi, Hatuwezi!".
Naama. Wakati umebadilika.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
mjengwablog.com
Tuesday, February 7, 2012
Sakata La Mgomo Wa Madaktari; Tafsiri Yangu

Nimetumiwa habari hii na Kaka Maggid Mjengwa.
Ndugu zangu,
Mgomo wa madaktari wetu ni habari kubwa. Umeingia sasa kwenye wiki ya pili. Hata kama ungekuwa ni wa siku mbili, bado ungesababisha madhara makubwa kwa nchi. Kwamba sasa una zaidi ya siku kumi na nne ni balaa kubwa kwa nchi yetu.

Tafsiri yangu;
Uliopo ni mgogoro kati ya madaktari na Serikali. Na kwenye mgogoro kama huu, siku zote,wenye kuathirika zaidi ni wananchi walio wengi.
Ni ukweli, kuwa karibu kila Mtanzania anayeamka asubuhi, ama nimgonjwa au ana ndugu, jamaa au rafiki aliye mgonjwa.
Hivyo basi, kuna mamilioni ya Watanzania wenye kutaabika kila siku na maradhi ya aina mbali mbali. Ni Watanzania wenye kutegemea sana huduma ya tiba inayotolewa na madaktari wetu. Na katika nchi zetu hizi, daktari ni rafiki muhimu sana wa mwananchi.
Ni jambo baya sana, pale Serikali inapoingia kwenye mgogoro namadaktari. Inapoingia kwenye mgogoro na marafiki wa wananchi. Hakuna mahali popote duniani wananchi wakatokea kuwachukia madaktari.
Hivyo basi, ni balaa pia pale Serikali inaposhindwa kumaliza tofauti zake na madaktari wawananchi kwa njia ya mazungumzo na hata kufikia hatua ya madaktari kugoma.
Katika nchi zetu hizi, mganga wa tiba aliyesomeshwa kwa fedha zawalipa kodi na kwa miaka mingi anahitajika sana. Mganga wa tiba msaidizi anahitajika sana. Na hata kama angelikuwapo Msaidizi wa Mganga Msaidizi wa tiba , naye angehitajika sana. Vivyohivyo kwa wakunga wakuu na wasaidizi, wauguzi wakuu na wasaidizi wao. Wote hao wanahitajika sana.
Na katika nchi zetu hizi, Serikali hazipaswi kufikia hatua yakuwatisha na hata kuwafukuza kazi madaktari. Hilo la mwisho lifanyike tu pale ambapo njia nyingine zote za kumaliza tofauti nakusuluhisha migogoro na madaktari zitakapokuwa zimeshindikana. Nakwanini ishindakane?
Tufanye nini sasa?
Taarifa kwamba Kamati ya kudumu ya Bunge inayohusika na masuala yahuduma za jamii imepanga kukutana na madaktari wetu ni hatua njema na ya busara. Maana, katika mgogoro huu taarifa zimekuwa zaidi za upande mmoja; upande wa Serikali. Niwakati sasa pande zote mbili zikasikilizwa na Kamati hiyo ya Bunge. Ndio, ni wakati pia hata madaktari wetu wakapewa nafasi tuwasikie.
Huu si wakati wa kufanya ’ propaganda’ za kisiasa kwenye masuala ya afya za wananchi.Na hata pale Waziri wa Afya alipokaririwa jana Bungeni akitamka kuwahali ya huduma za mahospitalini zimerejea katika hali yake ya kawaida ni mfano wa ’Propaganda’ za kisiasa ambazo Watanzania hatuzihitaji kwa sasa.
Hivi ni hali gani hiyo iliyorejea kwenye kawaida yake kwenye hospitali zetu baada ya mgomo huu wa madaktari unaoendelea sasa? Kwamba askari wetu wa Jeshi la Wananchi wamelazimika kwenda kutibu wagonjwa Muhimbili hiyo haiwezikuwa ni ’ Hali ya kawaida’. Kwamba madaktari wameripoti lakini hawaonekani mawodini hiyo haiwezi kuwa ’ hali ya kawaida’. Na kama ni kawaida, hivi ni nini tafsiri ya ’ kawaida’?
Hapa kuna ukweli unaopaswa kusemwa, na si kitu kingine bali ni ukweli. Watanzania tunatakakujua; ni kwanini watendaji wa Wizara husika wameshindwa kulitatua suala la madaktari wetu na hata kutufikisha hapa tulipo?
Yumkini, kulikuwa na hali ya kuyapuuzia madai ya madaktari katika hatua za awali. Yawezekana pia watendaji wa Wizara hawakuwa karibu na wawakilishiwa madaktari hao ili kutoa fursa ya kuongea na kutafuta ufumbuzi watatizo. Labda ndio maana tumefika mahali sasa mgogoro umekomaa na wahusika kuonyesha hali ya kutunishiana misuli. Kuna mahali kosa limefanyika. Ni wapi?
Ndio hapa, kuwa hata kama Kamati ya Bunge itafaulu kusuluhisha mgogoro huu, bado Watanzania tutahitaji iundwe Tume huru itakayochunguza namna watendaji wa wizara husika walivyolishughulikia suala hili kwa upande wao.
Tume hiyo itusaidie kuupata ukweli mzima ili kama taifa, tujifunze. Na wakati tume kama hiyo itakapokuwa ikifanya kazi yake, itakuwa ni busara, kwa watendaji wakuu wa wizara husika wajiweke pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi huo.
Kama Tume itabaini kuwa hakukuwa na mapungufu makubwa katika utendaji wao na hususan walivyolishughulikia suala hili la mgogoro na madaktari, basi, itajulikana hivyo, na wana nafasi ya kurudi tena kwenye nafasi za utendaji Serikalini. Inahusu umma kurudisha imani yake kwa Serikali yao. Ndio maana ya umuhimu wa wahusika kupisha pembeni kuruhusu uchunguzi ufanyike. Maana, haitakuwa busara kuliacha suala hili likapita kama yanavyopita mengine ili hali limegharimu maisha ya Watanzania.
Na kubwa zaidi kwa sasa, ni kwa pande zote katika mgogoro huukutambua; kuwa kwa sasa mvutano unaoendelea hautatoa mshindi, ni kwa vile, katika kilichotokea na kinachoendelea kufanyika sasa, sote, kama taifa, tumeshindwa.
Huu ni wakati wa kutanguliza busara na hekima. Tufanye yote, lakini,njia mujarab ya kutanzua mgogoro huu uliopo sasa ni mazungumzo katika mazingira ya kuheshimiana, basi.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam, Jumamosi, Februari 4, 2012 http://mjengwablog.com/

Tuesday, September 27, 2011
Makamu Wa Rais Dr Bilal Atoa Mhadhara Chuo Kikuu Cha Uppsala, Sweden!!!!
Pichani: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao katika mkutano Septemba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kushoto ni kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa Sweden, Prof. Lodhi. Picha: Muhidin Sufian.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametoa mhadhara kuhusu changamoto za kisayansi katika maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa kwa kifupi ISP ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Uswidi ambapo amefafanua kuwa, mchango wa wanasayansi kutoka katika chuo hiki una manufaa makubwa katika kukuza teknolojia katika sayansi kwa nchi za Afrika.
Makamu wa Rais ambaye alikuwa mhadhiri wa somo la Fizikia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kuingia katika siasa, amealikwa na wanasayansi wa kariba yake katika maadhimisho haya yaliyo na lengo la kutanua uwanda wa tafiti katika nchi za Afrika na hasa Tanzania, ambayo kwa sasa imeanzisha chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ambayo Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Telezya Huvisa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Burton Mwamilwa.
Ujumbe wa Makamu wa Rais ulifika hapa na kupata nafasi ya kuzungumza na Watanzania waliopo Uppsala ambao wengi walitaka kujua kama Tanzania imejipanga vema kukabiliana na tatizo la umeme nchini. Makamu wa Rais ambaye katika ziara hii amekuwa akikutana na wanasayansi mbalimbali wa Sweden na hasa waliobobea katika sekta ya nishati aliwaeleza Watanzania waliokuwa katika mkutano naye kuwa; kama taifa tuna kila sababu ya kukubali kuwa tulifanya makosa huko nyuma kwa kutotambua utanuaji wa vyanzo vya umeme wa uhakika hali inayotuumiza sasa lakini pia akawaambia kuwa serikali imejipanga vema kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linapata tiba katika kipindi kifupi na pia kuwa na umeme wa uhakika katika miaka miwili ijayo.
Maeneo makubwa ambayo Makamu wa Rais amekuwa akiwasikiliza kwa ukaribu wanasayansi wa Uppsala na Sweden ni kuhusu vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vikiwemo vile vya upepo na maji ya bahari huku pia ikiwa Tanzania imeshasaini mkataba wa uzalishaji wa umeme wa makaa yam awe na kampuni ya kutoka China, mkataba uliosainiwa wiki mbili zilizopita katika ya NDC na kampuni ya China ambazo zitashirikiana katika miradi mikubwa katika ukanda wa Mtwara.
Eneo jingine ambalo Makamu wa Rais amekuja kulihamasisha ni juu ya uhusiano wa chuo hiki kikongwe katika uwanja wa Sayansi na namna chuo hiki kitakavyozidisha ushirikiano wake katika kusomesha wataalamu wa Tanzania katika ngazi za Shahada za Uzamivu na mchango mkubwa ukiwa kukipatia uwezo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.
Katika ziara hii ya kitaaluma aliyoalikwa Makamu wa Rais inayochukua siku mbili, Makamu wa Rais pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Jamii wa Uswidi Ulf Kristersson na Waziri wa Mahusiano na Maendeleo Gunilla Carlsson. Katika ratiba hiyo pia Makamu wa Rais atatembelea Taasisi ya Mazingira ya Uswidi sambamba na kuzungumzia mafanikio ya Kilimo Kwanza kwa wadau wa maendeleo wa Uswidi.
Monday, September 26, 2011
MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA!!!!
Mimi leo nataka tutumie maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu kujadili swali lifuatalo :-Baba wa Taifa hayati mwalimu Nyerere, aliamini na kuja na falsafa ya maendeleo iliyokuwa inasema ili tuendelee kama taifa tunahitaji mambo muhimu manne(4) watu, ardhi, siasa safi na Uongozi bora. Lakini pia akasisitiza ili hayo maendeleo yafikiwe tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Kwa zama hii tuliyonayo pamoja na kuwa na hivyo vitu vinne kumeongezeka suala la UFAHAMU NA MAARIFA.
Swali katika ngazi ya familia na koo zetu za Kitanzania tunahitaji mambo gani ya msingi ili kuendelea.
Maana kwa hali ilivyo hasa kwa sisi watanzania tumebobea katika kulaumu, kulalamika na kulaani wakati hata siku moja kulaani na kulalamika hakujawahi kuwa suluhu ya kile unacholalamikia, kulaani na kulaumu.
UJUMBE HUU:- Nimetumiwa na kaka yangu pia msomaji wa MAISHA NA MAFANIKIO SALEHE MSANDA AMBAYE NI MKAZI WA NJOMBE. TUJADALI PAMOJA....
Sunday, September 11, 2011
Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu shakani - Zitto
Ndugu zangu salaam kwenu,naomba mnifikishie ujumbe huu kwa watanzania. Natanguliza shukrani zangu za dhati.
(Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not Zitto a Politician).
Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.
Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.
Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.
Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili.
'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa.
Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni. Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.
Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza.
Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.
Nimeamua kutotumia simu ya ngu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.
Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!
Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.
Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.
Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.
Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.
Zitto Kabwe.
Thursday, September 1, 2011
Picha ya wiki:- Kuelekea miaka 50 ya Uhuru!!!!
Monday, February 7, 2011
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPATA MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA UTALII

Na Tulizo Kilaga wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii amemteua Bw. Ibarahim Mussa kuwa
kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kuanzia tarehe 01 February 2011.
Uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa kifungu cha 6 (1) (b) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002.
Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu
mwaka 1982 hadi sasa ambapo alifanya kazi katika ngazi mbalimbali, katika
Idara ya Misitu na Idara ya Utalii.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utalii, Ibrahim A. Mussa alikuwa
Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia Utafiti, Takwimu na Mafunzo katika Idara
ya Utalii.
Bw. Mussa ana Shahada ya Uzamili (International Tourism Management)
aliyoipata mwaka 2005 kutoka chuo cha Sheffield nchini Uingereza
Bw. Mussa anachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutoka kwa Bi.
Maria Mmari ambaye amepangiwa kazi nyingine.
Monday, January 31, 2011
Naomba msaada jamani, nahisi masikio yangu yamejaa nta sijui maana nasikia sauti za hawa waimbaji ni kama mtu mmoja anaimba au wenzangu mnasemeje?
halafu sikiliza huyu
Jumatatu njema kwa wote!!!
Thursday, October 28, 2010
TANZANIA NAIPENDA SANA NA NADUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO!
Tanzania; Utulivu na Amani ni siraha yetu, tudumishe Amani yetu tunu yetu njema. Tunu hii tumepewa kwa upendeleo...hatukuinunua kwa fedha tunu hii, bali Amani imetawala...Amani ni namba moja Tanzania.Madaraka yasituchanganye, utajili usituchanganye, bali amani ni mhimu na ni namba moja kwa Tanzania. Tunapo kosoana wapendwa, tunapo elezana ukweli...Amani itawale daima! kwenye shida na kwenye furaha, kwenye njaa na kwenye huzuni...Amani itawale daima!
Tukumbuke ametupa bure, tukimwuzi ataiondoa Amani hii...tuitunze kama yai tunu hii njema ya Amani, tuilee na tuipambe vizuri tunu hii njema, tuitunze ili nayo itutunze, tuilishe na tuinyweshe daima kwa Utulivu na Amani sisi Watanzania hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
IDUMU DAIMA AMANI TANZANIA.
-Mimi kila ninapopata wakati mgumu wa kutafakari, wanapotupeleka viongozi wetu, huwa natafuta solitude kwenye Amani waliotuachia Wazee wetu wa enzi za Mwalimu, Baba wa Taifa letu. Unajua Amani ni kila kitu, hata kama umezingirwa na mafisadi...lakini walau unapata wasaa wa kuburudisha roho yako ukiwa kwenye Amani yako.
Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa letu, alicheza sana aliposema; Ukabila uishie utani, dini iwe ni mapenzi ya mtu na nafsi yake. Maneno haya yametuweka hapa tulipo leo. Nasikitika tu generation ya watoto wetu, maana sisi Baba zao tunadhani Amani hii tuliyo nayo Mungu anaona aibu kutuondolea na kuwapa wenye akili na mapenzi nae.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE!
Makala hii nimeipenda na nimeona si mbaya nikiibadika hapa. Ni kutoka kwa kaka Baraka CHibiriti. Duh! naa sasa ni siku tatu tu zimebaki kwa kweli naiombea nchi yetu Tanzania uchaguzi uwe wa amani. Mwenyezi Mungu atutangulie.
lebo:
amani na upendo,
siasa,
tanzania,
uchaguzi wa rais
Saturday, October 16, 2010
Chagua CCM chagua mahitaji haya............................
TUKO HIVYO, Hatuoni,Hatusikii.
Tunadanganyika kirahisi Tunafuata mkumbo BAADAE TUNALALAMIKA Chagua CCM
MAKAZI YETU
SHULE ZETU
DARASANI WATOTO WETU
HUKO VIJIJINI-DISPENSARY
Ubalozi wa Tanzania Wasington
Tunadanganyika kirahisi Tunafuata mkumbo BAADAE TUNALALAMIKA Chagua CCM
OFISI ZETU
MAKAZI YETU
SHULE ZETU
DARASANI WATOTO WETU
HUKO VIJIJINI-DISPENSARYWAO WAKICHAGULIWA........................
Ubalozi wa Tanzania WasingtonOfisi zetuBunge
Kuna cha kuongeza?
Sasa tucheze na hesabu 6,900,000/= kwa mbunge mmoja,zidisha mara miezi 12 then zidisha kwa miaka 5 = 414,000,000/= jumlisha 50,000,000/= anayopewa mara baada ya kumaliza miaka 5 = 464,000,000/= kwa mbunge mmoja.
464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.
464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.
Thursday, September 9, 2010
Friday, September 3, 2010
KIBAO CHA CCM CHA MARLOW NA VUVUZELA!!
Mungu ibariki Tanzania na Mungu mbariki Rais mtarajiwa na bila kusahau utubaribi sisi wananchi tuweza kumchagua rais mchapakazi!!!
Saturday, May 1, 2010
WANASIASA WASIO NA HURUMA NA NIA YA KUSAIDIA WALEMAVU HAWAFAI KUCHAGULIWA
WATANZANIA wametakiwa kutowachagua wanasiasa wasioonyesha utashi wa wazi katika kuwasaidia na kuwatetea walemavu wa aina mbali mbali nchini.Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na ndugu Jacob Malihoja Mwezeshaji katika mafunzo ya siku nne juu ya Uongozi na Utawala Bora yaliyoandaliwa kwajili ya viongozi wa chama cha wasioona nchini Tanzania League of the Blind (TLB) Wilaya ya Temeke.
Ndugu Malihoja alitoa kauli hiyo kwa masikitiko baada ya wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi kadhaa waliolikwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo ya wasioona kutotokea kwenye shughuli hiyo jambo ambalo liliwafanya Walemavu hao kujikuta wako peke yao kwa ufariji wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa waliyejitokeza na kumua kumwakilisha Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abasi Mtemvu ambaye alipata dharula ya kutembelea wananchi wake walioathirika na mafuriko.
Aidha ndugu Malihoja amesema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa sisi sote hatuoni, alitolea mfano Mhe. Mudhihiri alikuwa salama na viungo vyake vyote lakini alikuwa haoni, kwani laiti angekuwa anaona asingefanya safari ambayo ilisababisha na yeye sasa awe mmoja wa walemavu nchini.
Kwa kutambua hilo amesema Watanzania na wote tunawajibu wa msingi sana kuwasaidia walemavu kwani hakuna anayeona kesho atakuwaje.
Aidha amesema mbali na hilo walemavu wana akili na uwezo mkubwa sana katika kuchangia maendeleo yao wenyewe na maendeleo ya Taifa na kwamba kinachohitajika ni kuwawezesha washiriki maendeleo yao na maendeleo ya taifa kimamilifu kwama watu wengine..
Zaidi unaweza kusoma hapa.
Thursday, March 11, 2010
BROWN ASHIKA TAMA
“Mmetawala nchi hii kwa muda usiopungua miaka arobaini , na maisha ya watu yamekuwa ya wasiwasi mpaka sasa. Twawaambieni kwamba fungeni virago mrudi kwenu Ulaya, mtuachie nchi yetu tuiongoze wenyewe. Tunawahakikishieni kuwa kwa muda wa miaka kumi ya uhuru wetu, nchi itakuwa imebadilika. Wakati huo, njooni mwone, nchi itakuwa imefika kiwango gani cha maendeleo.” Maneno hayo yalisemwa na Mheshimiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere wakati TANU ilipokuwa inadai uhuru.
Usemi wa Rais wetu haukuadhirika. Siasa safi na uongozi bora ndiyo ulionufaisha usemi huo. Siasa tunayoifuata ni ile yakutofungamana na upande wowote wa nchi nyingine za ulimwengu. Ni siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo si ngeni katka nchi hii. Sisi tunafuata mfano wa jadi zetu. Ufanisi uliopatikana katika maendeleo yetu umeshtua ulimwengu mzima. Watu wa mataifa mbalimbali huja Tanzania kujionea wenyewe jinsi wananchi tunavyojenga taifa letu.
Siku moja Brown, Mwingereza ambaye aliwahi kuwa Bwana Shauri katika sehemu mbalimbali za Tanzania wakati wa ukoloni, alitalii Tanzania. Yeye alikuwa mwandishi wa gazeti moja huko Uingereza: na aliona kuwa angeweza kukusanya habari nyingi za Tanzania na maendelea yake. alikuja kuona ukweli wa maneno ya Rais Nyerere ambayo zamani aliwaambia wakoloni. Brown alifika Tanzania baada ya mika tisa tu tangu nchi kupata uhuru.
Baada ya kuwasili Dar es Salaam kwa ndege, akaamua kukaa jijini kwa muda wa siku mbili. Halafu alisafiri Tanzania bara kutembelea mbuga za wanyama na sehemu nyingine za kuvutia. Alitembembelea vijii vingi vya ujamaa katika mikao ya Mtwara, Ruvuma, Mbeye, Tabora, Mara, Pwani na mingineyo. Kila alipotembelea, alizungumza na wananchi habari za maisha yao katika vijiji hivyo vya ujamaa. Mazungumzo yaliyomfanya Bwana Brown ashike tama hasa ni yale yaliyosemwa na Mzee Kaswiga wa kijiji cha Mbalizi Mkoa wa Mbeya. Walizungumza chini ya mti mkubwa uliosimama kando ya barabara ya mtaa mmoja wa kijiji hicho.
Bwana Brown alianza mazungumzo kwa kuuliza, “Je, Mzee Kaswiga, unaweza kuniambia shabaha za kuanzisha vijiji vya ujamaa katika nchi hii, au unafahamu sababu ya kuanzisha kijiji hiki tu basi? Mzee Kaswiga akajibu, “ndiyo naweza. Shabaha katika vijiji vyote vya ujamaa ni Umoja. Tumekuwa wanyonge wa maisha kwa muda mrefu sana kwa sababu ya kuishi kwa ubinafsi. Sasa tumeamua kuishi kijamaa ili tufanye kazi pamoja, na mapato ya kazi yawe kwa faida ya wote vijijini. Matokeo yake ni haya unayoyaona katika kijiji hiki.” Bwana Brown akauliza tena, “Unamaanisha nini unaposema kuishi pamoja kijamaa? Kwani hamkuwa mnaishi hivyo kabla ya sasa?” Mzee akajibu, “Babu zetu wa kale walikuwa wanaishi namna hii, wakoloni walipotawala wakaingiza ubinfsi ili mabepari wastawi. Maendeleo ya watu yalikwama, kwani waligeuzwa kuwa na mioyo ya ubinafsi. Lakini sasa hali hiyo hatuna. Wana-Kijiji hujiona kuwa ni kitu kimoja. Kazi zetu tunazozifanya zina lengo la kuinua maisha yetu. Mwana-kijiji huwa amejiweka katika bima ya maisha kwa vile huwa chini ya uangalizi wa kijiji. Huo ndio msingi wa kuishi pamoja, kwa ajili hiyo watu hupendana, huheshimiana kindugu na kusaidiana katika matatizo mbalimbali. Bepari au kabaila hana lake tena.”
Bwana Brown aliandika maneno katika daftari yake. alimtazama mzee Kaswiga kwa tabasamu ya husuda, kisha akamwuliza, “Kwa hiyo una maana kwamba hizo tu ndizo faida mnazopata?” Mzee akajibu, “La, hasha, hizo ni baadhi tu. Shule na hospitali zimejengwa. Maji yamepelekwa vijijini kwa mabomba, pia kuna faidanyingine nyingi. Siku hizi maisha yameanza kutakata ukilinganisha a enzi za wakoloni.” Bwana Brown alionyesha kufadhaika kwa vile maneno ya Mzee Kaswiga yalimsuta. Akajitetea kwa kusema. “Lakini wakoloni walikusudia kutenda hayohayo, kwani walianza kujenga shule na hospital..........” Mzee Kaswiga akamdakiza, “La, la, la, sisemi hamkufanya lolote. Ingawa mlipanga kutenda mengi, kutimiza kulikuwa kwa pole pole; na kwa upande mwingine nataka ufahamu kuwa kukusudia si kutenda, kwani mawazo peke yake hufiki mbingu ya saba! Ni kama ruya ya kupaa hewani usiku.”
Mazungumzo yalizidi kukolea. Bwana Brown akatambua kwamba yule mzee alikomaa na siasa ya ujamaa na mabadiliko ya maendeleo nchini. Hata hivyo alimuliza swali jingine. “Mambo gani yanasababisha kuanzisha vijiji vya ujamaa?” Mzee alichelewa kidogo kujibu swali hilo kwani alikuwa ananusa ugolo. Baada ya kufuta pua na machozi alijibu, “Vijiji vingine vimeanzishwa kwa sababu ya mafuriko ya maji. Watu wanaoishi kando kando ya mito huingiliwa na mafuriko, kwa hiyo huamua kuhama na kuanzisha makao mapya sehemu zilizoinuka. Vijiji vya ujamaa katika wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani vilianzishwa namna hiyo. Sababu nyingine ni ya kudumisha usalama wa maisha ya watu kwa urahisi. Wakikaa pamoja, huwa ni rahisi kujilinda kutokana na maadui. Vijiji vingi vya Mkoa wa Mtwara vilianzishwa kwa sababu hiyo. Vijiji huanzishwa kwa njia mbalimbali. Njia ya kwanza ni kwa hiari ya watu wenyewe badala ya kuelewa na kuridhika na siasa ya ujamaa. Pili nikwamba watu wanaweza kugeuza kijiji chao cha zamani na kukifanya cha ujamaa.” Wakati Mzee Kaswiga alipokuwa anasimulia hayo, Bwana Brown alikuwa ameegemesha shavu lake juu ya kiganja cha mkono wa kulia huku akimsikiliza kwa makini. Alistaajabu kumwona mzee huyo akisimulia habari za vijiji mbalimbali vya Tanzania kwa uhakika kabisa.
Wakati ulikuwa mwingi sana, lakini Bwana Brown hakuonyesha dalili ya kuchoka. Alitaka kufahamu uongozi wa kijiji kwa jumla. Mzee Kaswiga akamweleza Bwana Brown hivi, “Uongozi wetu unatawaliwa na Katiba ya kijiji ambayo imetengenezwa na wana-kijiji wenyewe. Katiba inaonyesha viongozi na kamati za kijiji. Kadhalika inaonyesha masharti yanayotawala maisha ya wana-kijiji, utaratibu wa kufanya kazi na kadhalika. Mipango ya uchumi imepangwa ili itimizwe kwa muda ule wa miaka ya maendeleo iliyopangwa na serikali. Ili mipango hiyo itimizwe ipasavyo, wana-kijiji hugawanywa katika vikosi. Kila kikosi hupewa kazi maalum ya kufanya kila siku iliyo tofauti na kazi ya kikosi kingine. Kwa mfano katika vijiji vya Rufiji kila mabalozi kumi hufanya kikosi kimoja ambacho kinakuwa chini ya kiongozi anayeitwa Mhenga. Kazi ya Mhenga ni kuangalia na kuhakikisha kuwa kazi ya siku inafanywa, na baada ya kazi hupeleka ripoti kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambaye huingiza mahudhurio yote katika daftari. Kwa njia hii inakuwa rahisi kuwafahamu watu wasiohudhuria kazi. Wapiga uvivu huchukuliwa hatua kwa mujibu wa katiba. Kazi muhimu hasa zinazoweza kuendeshwa katika vijiji vya ujamaa ni kama kilimo, ujenzi, uvuvi, ufinyanzi ususi, na kadhalika. Ni shabaha ya wana-kijiji kuendesha viwanda vidogo vidogo ili kupata mahitaji yao ya kila siku. Natumaini umeona kazi kama hizo katika vijiji vingine ulivyotembelea.”
Bwana Brown alitosheke sana na maelezo hayo. Alijionea mwenyewe jinsi Watanzania walivyokuwa wanapiga vita umaskini, maradhi na ujinga. Maneno ya Rais hayakuwa bure na kwamba Tanzania yastahili pongezi machoni pa ulimwengu. Baadaye Bwana Braun aliwaaga wazee wa Mbalizi kwa furaha na alimsifu sana Mzee Kaswiga alivyozungumza naye kwa busara sana. Aliwatakia kila la heri katika kukiendeleza kijiji chao na nchi yao kwa ujumla.

Subscribe to:
Posts (Atom)