Showing posts with label kupendana. Show all posts
Showing posts with label kupendana. Show all posts

Monday, November 21, 2016


Leo nimetumiwa huu ujumbe na RAFIKI nami nikaona ni ujumbe mzuri nisiwe mchoyo nikaona niuweka hapa kibarazani kwetu...ukipata wasaa basi soma...

Bwana mmoja maskini sana aliishi na mkewe. Mkewe alikuwa na nywele ndefu za kuvutia. Siku moja mkewe akamwambia bwana huyu akamnununulie chanuo la nywele zake ili azichane zirefuke na kunawili vizuri. Bwana huyu alijibu hana pesa kabisa hata ya kutengenezea saa yake iliyokuwa imevunjika. Mwanamke huyu hakuendelea tena kusisitiza ombi lake. Kesho ilipofika bwana yule akiwa anarejea nyumbani alipitia dukani akaiuza ile saa yake na kununua chanuo kwa ajili ya mke wake. Alipofika nyumbani akiwa na lengo la kumshangaza mkewe  akastaajabu kumkuta mkewe kanyoa. Mke naye kumbe alizinyoa nywele zake na kuziuza kisha akamnunulia mumewe saa mpya. Wote walikuwa na furaha  ya kupendana na kujitoa kwa mwenzie wakajikuta wanalia kwa furaha.
UJUMBE:- KUMBUKA KUPENDA SIO KITU  ILA KITU NI KUPENDA . ILA KUPENDANA NI ZAIDI YA KITU. MPENDE AKUPENDAYE!

Tuesday, February 2, 2016

TUPENDANE, TUSAIDIANE MAANA SISI SOTE NI NDUGU....


Watoto wengi  wanatamani kuishi maisha ya furaha na upendo ebu tazama wanavyoishi watoto hawa katika mazingira magumu tuishi kwa kufikiriana kusaidiana.  Ebu chukua dakika chache kusikiliza ujumbe wa wimbo huu wa  Ben Paul na halafu linganisha na picha hii ya hawa watoto. 


TULICHO NACHO TUGAWANE TUACHE UBAHILI SISI SOTE NI NDUGU NA BABA YETU NI MMOJA. UPENDO DAIMA!