Showing posts with label samaki. Show all posts
Showing posts with label samaki. Show all posts

Wednesday, May 29, 2019

VYAKULA/MILO AIPENDAYO KAPULYA

Chakula cha asubuhi mayai, soseji na vinginevyo na bila kusahau matunda kama papai, nanasi na  zabibu. Bila kusahau chai(chingambwe) yaani chai isiyo na sukari

Hapa ni samaki mzima mkubwa aliyeokwa kwenye oven na aina nyingine za samaki kama pweza, kamba nk. Karibuni tujumuike wapendwa.
Hapa ni viazi  kwa samaki wa kuchoma/banika  yaani hapa ndo walinikumbusha kwetu LUNDO/NYASA.
PAMOJA DAIMA.

Tuesday, March 26, 2019

LEO NIMETUMIWA ZAWADI HII NA RAFIKI YANGU

Baada ya kushukuru nimemlaumu sana kwa kunitamanisha.....ahsanten  kwa zawadi rafiki yangu umenikumbusha kwetu Lundo/nyasa

Friday, March 9, 2018

PALE UPATAPO WASAA WA KUPUMZIKA BASI PUMZIKA KWANI NI MUHIMU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Hapa yaonekana kuna kitu alikuwa akishangaa  au sijui hakuwa na njaa?
CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA KULIKO VYOTE HAPA DUNIANI NI SAMAKI
BAADA YA KAZI YA WIKI NZIMA SIO MBAYA KUJOPONGEZA KIDOGO. NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA WIKI HII NA IWE YA FURAHA NA AMANI ITAWALE KATIKA KAYA ZENU.

Wednesday, August 2, 2017

HIVI NDIVYO VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU

Ugali wa ulezi na nyama ya kuku, na sio ugali tu ugali na mlima wake juu ukiisha huu ni lazima usingizi mnono utapatikana iwe mchana au usiku:-)
Samaki waliokaangwa kwa ustadi haswaaaa
Au tu chips MIHOGO...nimekula sana mlo huu wakati nipo chuo kwanza naupenda pia ilikuwa bei rahisi  na unashibisha . Ukipata na kachumbali yako mmmhhh utajiuma kidole au pia ulimi:-) Haya niwatakieni mlo mwema siku ya leo chochote utakachokula kiwe kitamu.....PANAPO MAJALIWA

Friday, June 24, 2016

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA ...NYASA HII! CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA

Ugali wa muhogo, Kisamvu, dagaa wabichi na kipande cha samaki tena kichwa...nakwambia hapo ni utamu tu....


Wednesday, June 15, 2016

NIMEOTA NDOTO NIPO LUNDO/NYASA NAKULA UGALI KWA SAMAKI NA KISAVU... MLO AUPENDAO KAPULYA...

Nilipoamka kumbe sio...maana hapa nilipo hata unga sina wa kusonga huo ugali sina. Nitabaki kula kwa macho tu......Ngoja nikatafute unga......

Sunday, May 8, 2016

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JIONI HII YA JUMAPILI YA LEO KWA MLO HUU...

UGALI, KACHUMBALI NA SAMAKI WA KOKA
Mwenyezi Mungu na aubaribi mlo huu na watakaokula nao pia washibe na kupata baraka zake. JUMAPILI NJEMA SANA PIA JIONI NJMEA. KAPULA/KADALA

Friday, June 26, 2015

MLO HUU NIMEUTAMANI SANASIKU YA LEO:- UGALI, SAMAKI WA KUKAANGA NA MLENDA/BAMIA

Ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa sita, Yaani hata siamini mwezi huu ulivyoisha haraka. Na katika siku hii ya leo ningependa sana kula mlo huu, Je? wewe ungependa kula nini siku hii ya leo au nawe kama Kapulya. IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)

Friday, July 25, 2014

MSIONE KUADIMIKA NIPO...PIA NIPO LIKIZO MUDA AMBAO NI MZURI KUWA NA FAMILIA...ILA NIPO!!!!

 Samahani kuadimika  ila nipo  kiaina ....
 ..Nipo likizo na nilikuwa nimejificha hapa na kublog ilikuwa ni kaziii kwelikweli. Nilikuwa na wakati mzuri sana na familia pia baadhi ya marafiki.  katika picha hapo unaona kitu fulani ni wanetu  wapo ziwani kuvua samaki...baada ya muda wakarudi na samaki...
...Na ndo ikawa kazi yangu kumtoa samaki magamba. Kwa vile nimekulia samaki hakuwa kazi kubwa na ngungu kwangu.:-)

Friday, June 20, 2014

CHAKULA KILICHONIKUZA MPAKA KUWA KAMA NILIVYO LEO....

Nimekitamani kweli chakula hili ..samaki, ugali na bamia..mmmhhh nausikilizia utamu wake.
JIONI NJEMA KWA WOTE

Tuesday, October 29, 2013

NIMETAMANI SANA CHAKULA HIKI MIHOGO KWA SAMAKI

Nimetumiwa picha hii na mdogo wangu Sarah Mgaya sasa hivi ni mihogo na samaki ni chakula ambacho nimekula sana nawaza kusema ndicho kilichonikuza. Kama si hivyo basi ugali wa muhogo na samaki...nimetamani mno...ahsante

Tuesday, October 8, 2013

HIVI NDIVYO MAPISHI YA NANGONYANI YALIVYOKUWA JANA JIONI SAMAKI WA KIHINDI!!!

 Hapa samaki anaandaliwa, ni samaki wa kihindi inaitwa KHARI MACHLEE  ulikuwa mlo wangu wa jana jioni unaweza kula na wali, ugali na mikate pia.
Na hapa ndo tayari ameiva na tayari kwa kuliwa ni mlo mzuri kwa kweli ...nilipitiwa kwa utamu nikasahau kupiga picha ilivyokuwa kwenye sahani yangu ilivyoonekana...:-) Kapulya

Monday, March 4, 2013

JUMATATU YA LEO TUIANZE KWA KUANGALIA VIPI JUMAPILI YA JANA ILIKUWA KWA KAPULYA...MLO WA JUMAPILI JIONI ULIKUWA KAMA IFUATAVYO:- WALI, SAMAKI AINA YA COD NA SLAMON, MCHUZI WA NAZI NA NJEGERE!!!

 Hapa mishikaki ipo tayariinasubiri kuchomwa ni mishikaki ya samaki ya aina mbili:- cod na salmon anayejua kwa kiswahili anisaidie tafadhali nimetafuta sijapata jibu.
 ---na hapa tayari mishkaki imeiva ..nimechoma kwenye oveni kwa vile huko nje bado kuna baridi na theruji nyingi sana ....
Na hapa mlo mzima ndivyo ulivyokuwa wali, njegere, salmon,cod na mchuzi ulioungwa kwa nazi  jioni ya jana ilikwisha safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana...
 
Na baada ya kula chakula kilibaki basi Kapulya akapata kutengeneza la kwa ajili ya kula leo jumatatu awapo kazini.Huwa sipendi kununua chakula kazini---kama unavyona hapo ndo mlo umekamilika nitakula leo jioni niwapo kazini ...JUMATATU NJEMA KWA WOTE.

Monday, October 1, 2012

NIMEUTAMANI KWELI MLO HUU UNGEKUWA MLO WANGU WA JIONI HII!!!

ila nitashindwa kwa vile kitu kikubwa zaidi ni kwamba sina unga ....mwisho nimebaki kumezea mate tu..hasa huyo samaki wewe acha tu...picha toka http://barakachibiriti.blogspot.se.
Nawatakieni kila la kheri au sijui jioni,mchana, asubuhi au usiku mwema.

Monday, July 23, 2012

Tuendelee na ile yetu …….HADITHI HADITHI…..HAPA NI HADITHI YA MVUVI NA SAMAKI WA DHAHABU!!!



Ilipoishia ”Usiwe na hofu, baba kizee enenda kwa amani sasa.” Baba Kizee alirejea kwa mkewe mzuri. Lo! Akaona nini? Jumba zuri na barazani mkewe amesimama , amevaa vazi la maridadi la nyoya jema. Na kichwani kavaa kilemba kilichotariziwa vilivyo na vito vyema vikimning´nia shingoni. Na pete za dhahabu zilipamba vidole vyake na viatu vyororo vyekundu vikimkubali miguuni….NA SASA INAENDELEA…………
Na mbele yake watumishi wakimhangaikia, huku akiwavuta nywele zao na kuwacharaza bakora. Baba kizee akamsaili mkewe mzuri “Je, waonaje sasa mke wangu sasa roho imeridhia kibibi? Mkewe akamjibu kwa jeuri , na kumpeleka mazizini kufanya kazi za suluba huko.
Wiki moja ilipita iklifuatwa na nyingine. Na mkewe mzuri akiwa haridhiki kupita siku zote. Akamwamuru baba kizee aende tena baharini. “Enenda tena baharini ukamkabili samaki mkuu mwambie sitaki kuwa mwanamke wa basaba bora bali malkia mwenye enzi!”
Baba kizee akaona vi mno akadahili kwa nguvu. ”Nini tena, ew mwanamke! La hasha umechanganyikiwa! Kumbuka ya kuwa wanena na kutenda. Kama mke wa mvuvi utaifanya milki nzima ilemewe na kicheko!”
Mke wa mvuvi akazidi kisirani akamvuta masikio mumewe na kusema ”unathubutuje kubishana . Ewe kisonoko na mimi mwanamke wa nasaba  bora? Elekea hivi sasa baharini nakuamuru! Kama hutaki, nitakuburura hadi huko!” Baba kizee alijizoazoa na kwenda tena baharini. Bahari ile ya maji ya mbingu ikawa nyeusi tii, tena inatisha.
Akapaza sauti yake, akaita na samaki wa dhahabu akaja akiogolea. ”Ni nini tena kinachokukera. Ewe baba kizee, hebu niambie!” Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee alijibu sawia ”ujaliwe neema Ewe Bwana wa Samaki! Mke wangu mzuri amecharuka tena safari hii ajipa wazo hatakuwa tena mwana wa nasaba bora. Yu ataka kuwa Malkia mwenye enzi.” Naye samaki wa dhahabu akajibu ”Usijali, ewe baba kizee rejea nyumbani kwa amani nawe utamkuta mkeo mzuri yu malkia!”
Baba kizee alirejea kwa mkewe mzuri na nini alikiona? Jumba lla kifalme, likimilikiwa na mwanamke wa hila akiwa ametamakani mezani. Wakuu na mabwana wakimngojelea, wakimnywesha mvinyo kwenye chombo cha dhahabu huku akividonadona vipande vinono vya nyama. Huku walinzi wenye macho makali wakimlinda pande zote wakiwa wamejihami kwa vishoka mikononi. Baba kizee akatupa jicho huku na huko. Jicho likamfeli, akagwaya! Alijiinamia hadhi ardhini mbele yake na kuweza kutoa maneno haya ”Heshima kwako na kicho Ewe malkia habe niambie sasa ikiwa moyo wako umeridhika?” Mkewe hakumthamini hata kwa mtupo wa jicho bali aliamuru watu wake kumuondolea mbali. Ndipo waungwana na wa nasaba bora wakamwelemea mbiombio wakamkwida shingoni. Na kumbeba hangahanga na mabawabu wa mlangoni wakamsindikiza nje kwa vishoka vyao.
Na halaiki yote kwa jumla yao wakajisheheni kwa kicheko. ”Hiyo ndiyo tosha yako ewe kizee mtovu wa busara! Na hilo liwe funzo lako kujijua wewe u nani siku za hapo baadaye! Na hivyo wiki ikayoyoma na nyingine ikafuata. Mama kizee akazidi utakavu, akatuma wajumbe wake kumkamata baba kizee. Walimpata, wakamleta mbele ya Malkia. Naye mke mzuri akanena kwa mumewe ”Enenda tena ukasujudu kwa samaki mkuu. Sitaki tena kuwa Malkia mwenye enzi, bali nataka kutamalaki maziwa yote na bahari na katika vina vya bahari. Nitaweka ngome yangu na huyo samaki wa dhabu atanitumikia mimi. Huku nikimtuma kotekote!” Baba kizee hakuthubutu kupinga kauli ya mkewe hivyo akaenda tena baharini na tazama! Tufani kuu ilitokea mawimbi makuu yaliinuka kumlaki, tetemeko tupu, muondoko wa ghasia, muungurumo mkuu hata hivyo baba alipaza sauti na kuita. Na samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”kulikonit ena baba kizee njoo unieleze!” Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee akajibu sawia ”Na ujaliwe neema Ewe Mkuu wa Samaki! Nimfanyeje huyu mwanamke? Huyu ajuza mjinga, hataki tena kuwa Malkia pia anataka kutawala maziwa na bahari. Anataka kuweka ngome zake katika vilindi vya bahari, na kukufanya wewe mwenyewe umtumikie. Na kukutuma wewe huk ona huko.” Samaki wa dhahabu alitulia tuli pasi na jibu na badala yake alipiga mkia wake majini akajerea kwenye maji makuu. Baba kizee alisimama ukingoni, akisubiri . Alisubiri kwa muda mrefu, lakini halikuja jibu. Hatimaye akarejea kwa mkewe mzuri, na tazama! Akamkuta amekaa mekoni kwenye kibanda kikongwe cha udongo na miti na mble yake kukiwa na kibeseni kilichoraruka hadi katikati. HADITHI IMEKWISHA..
Je Hadithi hii inatufunza nini? 

Monday, July 16, 2012

HADITHI HADITHI…..HAPA NI HADITHI YA MVUVI NA SAMAKI WA DHAHABU!!!

Nieipenda hadithi hii na nimeona nisiwe mchoyo ni hadithi nzuri hata kwa watoto wangu wamekisoma ....nimeisoma kwenye kitabu na mwandishi ni Alexander Pushkin. Haya karibuni.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hapo zamani za kale. Palikuwepo na mzee mmoja, aliyeishi na mke wake mzuri sana kandokando ya bahari yenye maji ya rangi ya mbingu na kina kirefu. Waliishi kwenye kibanda cha udongo na miti.
Walikuwa wameishi pale kwa miaka thelathini na siku thelathini. Baba Kizee akivua samaki na bibi mzuri akifuma nguo.
Siku moja baba kizee alitupa nyavu baharini, nyavu alizivuta juu zilikuwa zimejaa uchafu wa baharini. Alitupa tena nyavu baharini, nyavu alipozivuta juu zilijaa gugu-bahari.
Mara ya tatu, nyavu zikazamishwa tena majini nyavu alipozivuta juu :- Tazama! Alikuwemo samaki mmoja. Si samaki wa kawaida, bali ni samaki wa dhahabu.
Samaki wa shahabu, akaomba msamaha. Huku akisema kwa sauti ya binadamu ”Ewe baba kizee, nirejeshe baharini nitakulipa malipo mema, nitakupatia chochote utakacho.”
Baba kizee alipigwa na mghafala. Akaingiwa na woga. Alikuwa amevua maeneo haya kwa miaka mitatu na ushee lakini hata siku moja hakupata kumsikia samaki anayezungumza.
Akamwachia samaki uhuru wake huku akisema maneno ya huruma. ”Ewe samaki wa dhahabu enenda kwa salama katika njia zako huna haja ya kunilipa fadhila. Rejea kwenye kina cha bahari na kuogelea na kupiga mikambi utakayo.”
Baba kizee alirudi kwa mkewe mzuri akamwadithia kuhusu kioja.
”Leo nilimnasa samaki wa ajabu si wa kawaida, bali wa dhahabu samaki huyo alinena lugha yetu akanisihi nimrejeshe baharini na akaniahidi zawadi maridhawa kwa kunitaka nitaje nitakacho! Nami sikutaka ujira wake nikamrejesha baharini bila malipo.”
Mke akamwambia mumewe kwa karipio ”Kefule, mjinga kichwani we! Huwezi kupata pato la samaki ukashindwa hata kuomba kibeseni cha kuogea! Tazama kile cha kwetu kilivyoraruka katikati.
Baba kizee akaenda kwenye bahari ile ya maji ya mbingu tena yenye kina kikuu, akaona jinsi bahari ilivyochafuka akapaza sauti yake, akaita na mara samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”Kulikoni baba kizee nieleze nami nijue!”
Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee alijibu ”Ewe mwenye rehemu Ewe mkuu wa samaki! Mke wangu mzuri ana uchungu nami haniachii kwa kutaka utakalo ataka tuwe na beseni jipya la kuogea kwa kuwa la kwetu kongwe limeraruka hadi katikati”.
Samaki wa dhahabu naye akajibu sawia ”Usiwe na hofu kamwe ewe baba kizee na enenda sasa kwa amani huko uendeko. Utalikuta hilo beseni jipya!” Baba kizee alirejea kwa mkewe mzuri na kujionea mwenyewe baseni jipya liko pale. Lakini bibie ukali akazidisha Mjinga wahedi yaani hilo ndilo ombi lako kuu hilo beseni la kuogea! Kuna faida gani kamwe” Kuwa na beseni tu la kuogea? Hebu rudi himahima enenda kwa samaki mkuu. Uende umwinamie, umwombe kijumba kizuri. Baba kizee akashika njia kwenda kwenye ile bahari ya maji ya rangi ya mbingu. Sasa bahari ilikuwa nyeusi iliyoghafilika.
Baba kizee akapaaza sauti na kuita na samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”kulikoni baba kizee hebu uniambie hima!
Kwa mwinamo wa hadhi baba kizee akajibu ”Rehema iwe kwako Ewe mkuu wa samaki mke wangu mzuri amesawijika zaidi haniachii huru ila kuningángánia hatatulia bila kupata kijumba kizuri.” Samaki wa dhahabu akajibu sawia ” Usijali baba kizee enenda sasa kwa amani utapata takwa lako la hicho kijumba kizuri.”
Baba kizee akarejea kwenye kibanda chao kikongwe, hakuona dalili yoyote ya kibanda kikongwe. Badala yake akaona kijumba kipya, kizuri mno! Kimepakwa chokaa, kina mnara mzuri wa kupitishia moshi. Na milango ya mpingo , pia na dirisha la nakshi.
Na katika kiti cha bustanini aliketi mkewe mzuri, huku akiwa hajitambui kwa mahasira yaliyomzonga ”Kefule, pumbavu wewe usiye na kitu kichwani! Yaani hicho ndicho ulichoomba kijumba hicho cha ovyo! Rudi tena kwa samaki mkuu mwinamie na kumwambia mimi sitaki kuwa mke asiye na hadhi bali mwanamke wa nasaba bora!” Baba kizee alikwenda tena baharini. Nayo bahari ikachafuka zaidi na kusikitika. Baba kizee akapaaza sauti, akaita na samaki wa dhahabu akamjia akiogelea. ”Kulikoni ewe baba kizee, hebu niambie nami nijue!”
Kwa mwinamo wa heshima baba kizee akamjibu sawia. ”Usijali neema, ee Mkuu wa Samaki! Mke wangu, kwa roho isiyosikia kitu haniichii nikapata pumzi. Sasa ameamua hatakuwa mwanamke dhalili yeye ataka kuwa mwanamke wa nasaba bora!”
”Usiwe na hofu, baba kizee enenda kwa amani sasa.” Baba Kizee alirejea kwa mkewe mzuri. Lo! Akaona nini? Jumba zuri na barazani mkewe amesimama , amevaa vazi la maridadi la nyoya jema. Na kichwani kavaa kilemba kilichotariziwa vilivyo na vito vyema vikimning´nia shingoni. Na pete za dhahabu zilipamba vidole vyake na viatu vyororo vyekundu vikimkubali miguuni….ITAENDELEA……

Friday, June 15, 2012

VYAKULA VYA ASILI NI VITAMU/ HAPA MIMI NIMEFIA KABISA

Hakika ebu angalia hapa ugali tena bongo BONDO, samaki na mboga majani  na matunda/matikiti maji baada ya chakula. Halafu sasa fikiria hapo ugali umelima mahindi/mihogo, ulezi au sijui mtama, mboga umelima mwenyewe bustani, samaki umewavua mwenyewe au tu umetoka kuwanunu wakati tu wavuvi wamerudi. Matikiti maji nayo labda umeyalima mwenyewe ....ashilia mbali viungo. Yaani hakuna kitu kilichokaa kwenye kopo wala nini? Mmmmhhh!! Yamu yamu yamu  ngoja niache ...picha toka kwa kaka Mjengwa.

Tuesday, April 24, 2012

SWALI HILI LIMENIKERA SANA:- MAJINA YA SAMAKI YANATOKA WAPI???

HAPA NI SAMAKI AINA YA MAGEGE
Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kuhusu majina ya samaki. Juzijuzi nilikuwa nikiangalia habari/pragramu kuhusu ziwa Nyasa, ziwa Viktoria na Tanganyika. Nikakumbuka majina ya samaki kama vile :- Kambale, Mbofu, Mbelele/sengefu, Magege, Vitui, Vindogo, Mbasa nk. Nikawa najuiliza hivi ni maeneo ya ziwa nyasa tu tunawaita hawa samaki hivi au? Na kama ni hivi nani aliwapa samaki hawa haya majini? Sikupata jibu...nikaona niliweke hapa kibarazani  hili swali. Kama nisemavyo/nijuavyo palipo na wengi hapaharibiki kitu. Tuwe pamoja katika kamjadala haka

Tuesday, February 14, 2012

NIMEUTAMANI MLO HUU KWA KWELI!!!

Leo nimetamani kweli mlo huu ningependa kweli kula mchana wa leo Ugali wa muhogo na samaki. Yaani nimerudi nyuma enzi zileee Lundo/Nyasa kila siku ugali na samaki. Katika picha hii ni samaki aina ya Tilapia "TILAPIA FISH CURRY" picha toka blog ya kaka Isaack yaani nimeiona picha hii tangu juzi nimemezea mate weeeeeeee nimechoka nikafikiri naota ndoto.



Ugali huuuo wote mnakaribiswa ila inabidi mharikishe maana jinsi ninavyopenda chakula hiki hasa hiyo samaki mtakuta imekwisha...LOL.
WOTE MUWE NA SIKU NJEMA UKIZINGATIA NI SIKU YA WAPENDANAO..NAMI NASEMA WOTE MNAPENDWA !!

Friday, September 16, 2011

KARIBUNI KIKOMBE CHA CHAI...NINYIME VITU VYOTE LAKINI SIO CHAI!!!


You´re Just my Cup of Tea,

Our Love Warms my Heart.

Najua wote mnajua mie ni mpenzi sana wa chai tena ile isiyo na sukari(Chingambu) :-).

Kichwa cha habari hapo juu kinasema kuwa "NINYIME VITU VYOTE LAKINI SI CHAI" Duh ! naungama ni kwamba nimesema uongo kwani mimi ni mdhaifu/mpenzi sana wa smaki pia kama ilivyo kwenye chai......



Ngoja tusikilize wimbo huu wa Nuru ft Mr Chocolate Flavour - Muhogo Andazi!!!




NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA ....MUWE NA AFYA NJEMA , AMANI NA FURAHA ZITAWALE NYUMBANI MWENU/WAKO.......IJUMAA NJEMA!!!!