Showing posts with label mazoezi kukimbia. Show all posts
Showing posts with label mazoezi kukimbia. Show all posts

Tuesday, July 23, 2013

SWALI LILILONISUMBUA SIKU YA LEO...!!!!

Nimeamka asubuhi hii na nimemshukuru Mungu kwa kunilinda. Nikaona ngoja ninyooshe viungo:- Yaani nikaende nje kama kawaida yangu kukimbia, nimekimbia, nimekimbia mara nikakutana na mkimbaji mwingine naye kawaza kama mimi anakimbia. Sasa hapa kitu kilichonipa swali ni kwamba mdada huyu alikuwa akikimbia na mbwa wake ambaye amemfunga kamba shingoni. Swali likanijia huyu dada ana uhakika kama huyu mbwa/kambwa anataka kukimbia? Maana niliona kama mbwa mwenyewe hata hakufurahia. Nikataka kusimama na kumuuliza.....lakini nikaacha. Muda wote nilipokuwa nakimbia swali lilizidi kunisumbua hivi kweli yule mbwa alipenda kukimbia?  Na pia nikazidi kuwaza....Nikaona niwape na wenzangu haka kakisa....TUSITENGANE TUWA  TUNAKUMBUKANA. PAMOJA DAIMA SIKU NJEMA. KAPULYA!!

Tuesday, March 5, 2013

PICHA YA/ZA WIKI MAZOEZI NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE!!!!

 Mchaka mchaka chinja....aaah ebu tuchukue wimbo huu Idi amini akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....
Dada mkuu msaidizi naye hayuko nyuma kabisa ..Haya dada mkuu msaidizi msimu wa kuanza mazoezi unakaribia ,,wewe endelea  usitazame nyuma ..haya alisema, alisema, alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti tuanze mchakamchaka....mmmmhhh ngoja niwaachie na wengine waanzishe kuimba maaana mapumzi hapa  yanasumbua kweli....Sijui mnawafahau wadada hawa?:-) JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA KILA MMOJA!!!!!

Tuesday, August 7, 2012

HAYA TWENDEE, TWENDE,TWENDE USICHOKE...!!!!

 Huyoooo anakuja, huyooo anakuja..anakuja anakuja....
.....na hapa ndiyo nimefika  golini...hii ilikuwa leo asubuhi...nimepanga kupata dhahabu ya olimpiki ..LOL
mazoezi tu kwa ajili ya afya ..ngoja nikapalilie bustani yangu sasa...

Tuesday, October 4, 2011

PICHA YA WIKI...MAZOEZI NI MAHIMU KWA AFYA YAKO!!!

Picha hii imenikuna sana na pia nimejikuta natamani pia kukimba kwani nimekuwa mzembe sana. Ngoja nikurudi kutoka kazini nami nikimbie. Safi sana ..ila sasa usiache endelea hivyo hivyo :-)

Sunday, September 14, 2008

MAANDALIZI YA LONDONI 2012

...............

Tutaona nani ataweza huo mwaka. wote tupo katika mazoezi makali sana mtajiju. Au labda niseme karibuni kujiunga nasi.

Friday, August 22, 2008

AGOSTI 22,2008 ERIK NA YASINTA KATIKA MAZOEZI YA KUKIMBIA


Leo nimeamua kumchukua na kijana wangu kwenda kufanya mazoezi ya kukimbia tukiwa tumevalia T-shirt za kutoka TZ. Je? unafikiri nani alimshinda nani. Kuna zawadi inamsubiri atayejibu vizuri.