HONGERA KUTIMIZA MIAKA 14 ERIK
Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nguvu sisi wazazi/walezi kwa kuweza kumlea mtoto/kijana Erik na leo ametimiza miaka kumi na nne/14. Hakika miaka inaenda nikiwa kama mama naona kama ilikuwa juzi tu alizaliwa kijana huyu. Mwenyezi Mungu azidi kuwa naye katika masomo, na mengine yote afanyayo ili yawe mazuri. Ampe oyo wa upendo kwa walezi, ndugu jamaa na marafiki. Samahani nimeshindwa kupata picha yake yupo shule. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA ERIK!