Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUTEMBELEE WILAYANI NAMTUMBO.ELIMU NIMEIPATA HABARI HII Albano Midelo Haya KARIBUNI.
Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi
SelousWilayani Namtumbo wakiwa darasani.
WANAFUNZI wa
shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani
Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa
nyasi.
Uchunguzi
uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo
mjini Namtumbo umebaini kuwa katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi 296
wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa
nyasi.
.
Mwalimu wa
taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi
katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa
na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na
kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi
592.
Katika shule
ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma
kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma
kwa wanafunzi.
Mwalimu wa
taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka
2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati
ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea
kwenye vibanda vya nyasi .
Katika shule
ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi
Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi wanaosomea kwenye vibanda viwili
vya nyasi kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba
nane.
Mkuu wa
shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu
yanasomea katika chumba kimoja ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita
wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu .
“Unajua
wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye
vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine
kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu
ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’,alisema.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa Wilayani
Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao.
Mratibu
elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri
shule tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga,Mkapa na Selous
wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na
kusisitiza kuwa shule za Minazini,Kidagulo,Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa
nyasi.
“Shule
zangu tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu
mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha
jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na
serikali ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya
aibu’’,alisisitiza.
Makamu
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa
kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya
hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi .
“Mpango wa
uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule
nyingi hivyo baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa
vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa
vyumba vya madarasa’’,alisisitiza.
TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO KWA JINGINE LA ZAMANI!!





