Showing posts with label Afya na maisha. Show all posts
Showing posts with label Afya na maisha. Show all posts

Saturday, May 10, 2014

TAHADHARI :UGOMVI UNAATHIRI AFYA YAKO!!!


 
Wanaume wasio na ajira wako katika hatari ya kuathirika zaidi kutokana na ugomvi
 
Ugomvi wa mara kwa mara baina ya wapenzi, marafiki ama hata jamii unaongeza hatari ya kufa kwa watu wenye umri wa makamo. Haya ni kwa mujibu wa watafiti nchini Denmark.
Watafiti wamesema kuwa wanaume na wale ambao hawana kazi wako katika hatari Zaidi.
 
Utafiti huo katika jarida la 'Epidemiology and Community Health', unasema kuwa shughuli za kukidhi matakwa na mahitaji ya jamii pia zimehusishwa na idadi kubwa ya vifo vya mapema.
Pia kulingana na utafiti huo utu wa mtu na uwezo wa mtu binafsi kukabiliana na dhiki ilichangia katika matokeo ya utafiti huo.
Ingawa watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Copenhagen waliweza kupata uhusiano uliopo kati ya vifo vya mapema na kugombana, na kuwa ugomvi uliongeza hatari ya vifo vya mapema mara tatu, hawakuweza kuelezea kikamilifu sababu haswa ya hali hiyo.
Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa watu wenye wasiwasi mwingi na mahitaji mengi kutoka kwa wapenzi wao na watoto, pamoja na wale wanao gombana mara kwa mara na jamaa wao, wamo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua magonjwa ya moyo na kiharusi.
Tafiti za hapo awali pia zaonyesha kuwa utangamano mwema na watu pamoja na marafiki wengi ina athari chanya katika afya, huku utu kwa kiasi kikubwa ukiamua jinsi mtu hupokea na kuguswa na hali za kijamii pamoja na mahusiano.

Wapendanao hawapaswi kugombana

Kumsumbua mpenzi wako pia kunahatarisha afya
Katika utafiti huu, watafiti walisema kuwa athari za kisaikolojia zinazosababishwa na dhiki, kama vile shinikizo la damu na ongezeko la athari ya magonjwa ya moyo, ndizo hasa zinaweza kueleza athari ya ongezeko la vifo vya mapema.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanapokabiliwa na hali za dhiki kwa kuongeza homoni inayokabiliana na hali ya dhiki na wasiwasi, jambo ambalo linazidisha athari ya kiafya.
Utafiti huo ulihusisha watu 9,875 wake kwa waume wenye umri wa kati ya miaka 36 na 52 na ulitumiwa kuchunguza uhusiano uliopo baina ya hali ngumu ya uhusiano wa kijamii na vifo vya mapema.
Wote walikuwa wameshiriki katika Utafiti ‘Denmark Longitudinal’ kuhusu Ajira, ukosefu wa ajira na afya , kuanzia mwaka wa 2000.
Utafiti uligundua kuwa wasiwasi wa mara kwa mara au mahitaji yanayotokana na wapenzi na watoto ulihusishwa na ongezeko la kufikia 50%- 100% la vifo vya mapema.
Ukosefu wa ajira ulionekana kuongeza athari hasi za uhusiano mgumu wa kijamii. Wale ambao hawako kazini wameonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo kutokana na jambo lolote kinyume na wale walio na kazi.
wanaume pia wako katika hatari zaidi kutokana na mahitaji na wasiwasi unaotokana na wapenzi wao wa kike , huku wakiwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo zaidi ya ile ambayo kwa kawaida imehusishwa na kuwa mwanamume.
Dakta Rikke Lund, wa kitengo cha afya ya umma katika chuo kikuu cha Copenhagen amesema kuwa wasiwasi na ugomvi ni sehemu ya maisha. Lakini akaongeza kuwa watu ambao wanakuwa na migogoro mara kwa mara wako katika hatari zaidi lakini wanaweza wakasaidiwa.
CHANZO: BBC.

Tuesday, March 5, 2013

PICHA YA/ZA WIKI MAZOEZI NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE!!!!

 Mchaka mchaka chinja....aaah ebu tuchukue wimbo huu Idi amini akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....
Dada mkuu msaidizi naye hayuko nyuma kabisa ..Haya dada mkuu msaidizi msimu wa kuanza mazoezi unakaribia ,,wewe endelea  usitazame nyuma ..haya alisema, alisema, alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti tuanze mchakamchaka....mmmmhhh ngoja niwaachie na wengine waanzishe kuimba maaana mapumzi hapa  yanasumbua kweli....Sijui mnawafahau wadada hawa?:-) JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA KILA MMOJA!!!!!

Wednesday, January 25, 2012

Madaktari watangaza mgomo nchi nzima

MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali.
Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais.
Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao.
Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.
“Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango kinachostahili,” alisema Dk Ulimboka.
Alitaja madai mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye ‘Standard order’ ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.
Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike.
Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.
“Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo,” alisema.
Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao.
Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.
Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha.
“Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari,” alisema Dk Mkopi.
Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.....kupitia http://simulizi.blogspot.com/.

Friday, October 8, 2010

Ngoja Ijumaa ya leo tuache ugimbi na tule matunda!!


Kula matunda uwe na afya bora poa kujikinga na magonjwa!! IJUMAA NJEMA SANA KWA WOTE!!