Showing posts with label salamu. Show all posts
Showing posts with label salamu. Show all posts

Saturday, August 20, 2016

NAWATAKIENI JIONI HII YA JUMAMOSI YA LEO IWE NJEMA ...

Jumamosi njema kwa atakayepita hapa na msosi ndio huu hapa tena wa kutosha tu...JUMAMOSI NJEMA..WOTE MNAPENDWA!

Friday, November 28, 2014

ZILIPENDWA....IJUMAA NJEMA!!

NAPENDA KUWATAKIA WOTE IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE WENYE AMANI TELE!!

Sunday, December 29, 2013

TUMALIZA JUMAPILI YA MWAKA HUU 2013 NA MWIMBO HUU WA DADA BAHATI BUKUKU :- DUNIA HAINA HURUMA.


NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA MWISHO KWA MWAKA HUU 2013 IWE NJEMA SANA WAKATI TUKIUSUBIRI MWAKA 2014. JUMAPILI NJEMA SANA....KAPULYA

Tuesday, April 10, 2012

SALAMU NA SHUKRANI KUTOKA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO!!!

Kwanza kabisa napenda kuwasalimu wote. Pia napenda kuchukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila dakika anipayo. Halafu nashukuru nimeisherekea sikuku hii ya kufufuka kwa Bwana wetu Kristo vema. Kwa hiyo namalizia na salamu hizi:-
Tuni/mafuatano ya sauti ndogo inaweza kukufanya/kutufanya uanze/tuanze kuimba, pia kukumbatiwa kunaweza kukufanya ujisikie vizuri. Vitu vidogo vinaweza kukufanya/kutufanya uwe/tuwe na furaha. Ni matumaini yangu SALAMU yangu hii, imekufanya UTABASAMU.....SIKU NJEMA....Yasinta/Kapulya

Sunday, April 8, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUWATAKIENI WOTE PASAKA NJEMA SANA!!

Salamu za Pasaka ziwafikieni wote popote mlipo na baraka kwa wote wataopita hapa. Muwe na pasaka njema wote....MNAPENDWA SANA.


Friday, March 16, 2012

UNAJUA KISA CHA WANGONI KUAMKIANA MONILE??

Ni hivi:- Kulikuwa na mzungu pale Peramiho aliyejenga lile kanisa. Na aliishi miaka mingi pale Peramiho. Mzungu huyo alikuwa na tabia ya kuamka asubuhi na kupita kuwatembelea watu majumbani mwao. Yaani kwa nia ya kuwajulia hali wazee na vijana. Yeye alipenda sana kutembea kwa mguu, toka Peramiho Hospitali mpaka njia panda ya kwenda Mbinga. Kijiji kimoja kiitwacho Lipokela. Na baadaye kurudi.
Sasa yeye kwa kuwa alikuwa hajui kiswahili na alitaka kujifunza. Basi alikuwa ana wasalimia ile GOOD MORNING!
Kwa mkato yaani MORNING na wale wazee wakawa wanamuuliza tukujibuje? Naye aliwaaambia mujibu MORNING. Basi wale akina BAMBU wakawa sasa ni kila mtu wakimuona asubuhi wanasema MONILE.... wanajibishana MINILEEE...Kisha wanamalizia TUWAONE....jibu lake ..YEOO..Yaani tumemwona leo mzungu ndiyoo.
Basi toka miaka hiyo mpaka leo WANGONI wanasalimiana hivyo. Ikiwa Asubuhi MONILE...MONILE ..TUWAONE BAMBU ...YEOOO
SIKU NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!

Thursday, July 30, 2009

Salamu wanablog I

Nimelipenda shairi hili na nimepewa idhini toka kwa aliyeandika Kaka Fadhy Mtanga kuwa niliweka hapa kwangu.


Nashika kalamu yangu, salamu nazituma,
Kwenu marafiki zangu, natumai mu wazima,
Nawaombea kwa Mungu, mjaliwe yalo mema,
Salamu wanablog.

Simon Kitururu, huzamia MAWAZONI,
Fikra zake ni huru, pia zina burudani,
Nasi tunamshukuru, hachoki tangu zamani,
Salamu wanablog.

Yupo dadetu Yasinta, yeye hupenda MAISHA,
Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,
Sifa tele azipata, maana huelimisha,
Salamu wanablog.

Christian Bwaya yupo, hutaka tuJIELEWE,
Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,
Ukweli daima upo, muhimu ujadiliwe,
Salamu wanablog.

Mubelwa Bandio pia, MZEE WA CHANGAMOTO,
Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,
Muziki hutupatia, yenye midundo mizito,
Salamu wanablog.

Subi dada yetu sote, wa NUKTA SABA SABA,
Ili mengi tuyapate, blog yake yashiba,
Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,
Salamu wanablog.

Chib naye ni rafiki, hutumia HADUBINI,
Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,
Magharibi mashariki, hutujuza kulikoni,
Salamu wanablog.

MWANAMALENGA Kissima, hutuonesha MWANGAZA,
Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,
Kwa ushairi ni vema, tungo zake zapendeza,
Salamu wanablog.

Serina Serina huyo, ana UPANDE MWINGINE,
Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,
Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,
Salamu wanablog.

Koero Mkundi pia, hutuambia VUKANI,
Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,
Daima hukumbushia, tutoke usingizini,
Salamu wanablog.

Ndugu yetu Mumyhery, kabobea kwa MAVAZI,
Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,
Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,
Salamu wanablog.

Kamala tunamjua, wa nyegerage KIJIWENI,
Fikra apambanua, ili tutoke kizani,
Sote tukajitambua, tujijue kina nani,
Salamu wanablog.

Masangu wa Nzunzullima, CHAKULA chake KITAMU,
Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,
Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,
Salamu wanablog.

Markus Mpangala, KARIBUNI sana NYASA,
Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,
Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,
Salamu wanablog.

Lumadede mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,
Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,
Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,
Salamu wanablog.

Na MWANASOSHOLOJIA, siachi kumsifia,
Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,
Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,
Salamu wanablog.

Nami MWANANCHI MIMI, wa DIWANI YA FADHILI,
Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,
Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,
Salamu wanablog.

Ambao sijawataja, lipo shairi jingine,
Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,
Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,
Salamu wanablog.

Sunday, August 24, 2008

AGOSTI 24,2008 SALAMU KUTOKA KWA YASINTA NGONYANI

Did anyone ever tell you how important you make others feel. Somebody out there is smiling about love that is so realy.

Did anyone ever tell you just how much they like you? well, my dearest friend today Iam telling you.

I believe that without a friend you are missing out on a lot!!!

Have a nice day, and I`m glad we are friends!!!!

FRIENDSHIP IS CONTINUOUS HOPE YOU HAVE A GREAT DAY