Showing posts with label unyanyasaji. Show all posts
Showing posts with label unyanyasaji. Show all posts

Wednesday, June 10, 2009

UNYANYASAJI WA WANAWAKE UNAZIDI DUNIANI

Huu ni ujumbe wa leo ambao unaeleza mengi na mengi yanaonekana, haya karibuni msikie na muone.


Kama unataka kunywa pombe basi kunywa kwa starehe yako lakini sio unakunywa pombe na kuanza kupiga wengine au mke wako. Kwa nini kunyanyasana kama unaona ukinywa pombe akili inachafuka basi acha kunywa maji.

Tuesday, June 9, 2009

KWELI HII NI HAKI?

Haya na maoni ya msomaji kwa picha hizo hapo chini.

Hii niliwahi kusikia imetokea Uganda mabapo mzee mmoja, alikuwa akimlazimisha mke wake anyonyeshe watoto wa mbwa ambaye mama yao alifariki. Kwani kabla mama yao hajafariki alikuwa na ng'ombe ambao walikuwa akitoa maziwa kwa ajili ya hao mbwa. Na hao ng'ombe huyo mzee alitoa mahari ya huyo mama hivyo mbwa wakawa hawana sehemu ya kupata maziwa ndipo yule baba akawa anamlazimisha mke wake awanyonyeshe hao mbwa. Kwani yeye alikuwa ni muwindaji, na hao mbwa walikuwa wakimsaidia katika shughuli zake za uwindaji. Lakini watoto wa huyo mama mmoja alifariki kwa ugonjwa ambao unakisiwa ni kichaa cha mbwa, na yule mmoja aliebaki nae alianza kukuhoa kama mbwa, na mama chuchu zake zilikuwa na madonda kwa ajili ya kung'atwa na mbwa wakati akiwanyonyesha, lakini kwa india ni mambo ya kawaida. Ikiwa ni pamoja na kuuza viungo vya mwili na kupandikizwa mimba za watu wengine kwa ujira.

Hapa bado sijaelewa yeye huyo mzee alijisikia raha gani. Na pia kweli alimpenda mke wake na watoto au aliwapenda zaidi mbwa. Kumsaidia kuwinda, labda wenzangu mnisaidie hapa. Kwali kumlazimisha mkw wako knyonyesha mbwa hivi wanaume wanakiri wao ni akina nani kuwatesa wanawake kiasi hiki?

Tuesday, April 21, 2009

MASUALA YA UBAKAJI NA KUPIGA WANAWAKE LINAZIDI KUWA KUBWA

Dunia imeharibika watu wanazidi kupotoka, angalieni haya mambo yanavyozidi kuenea. Mambo kama vile unyanyasaji, kuna ukatili mwingi sana hapa duniani ambao zaidi ni juu ya wanawake na watoto. Hao ndio wanaopata shida zaidi. Ukatili ni kinyume na haki za binadamu na uko ukatili wa aina mbalimbali. Kuna vipigo, matusi, kulazimishwa kufanya mapenzi, kuna baadhi ya mila potofu kama vila ndoa za lazima, kuolewa ukiwa na umri mdogo, kurithi wajane nk.

Bado sijaelewa ni kitu gani kinawafanya wanaume wengine wawapige wanawake. Kwanini umpegi mwenzi wako? Je usipompiga uanaume wako utapotea? Na kuna raha gani kumpiga mwenzako kama mnyama? Na hata mnyama hairuhusiwi kumpiga. Hili suala la kubaka utasikia raha gani wakati mwenzako anapata maumivu yasiyo kifani. Na pia hajapenda.

Je? Mnafikiri hii inaweza kutokana na wengi wanaume wanafikiri wao ndio waamuzi wa kila kitu ndani ya nyumba? Na kwa nini watu wawili waliooana wasikaa chini na kujadiliana na kuona kosa liko wapi. Je? Ingekuwa kinyume ingakuwa sawa?

Au labda wengi wanafuata maandishi haya:- Mwanzo 3:16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako, kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumea, naye atakutawala.

Ndugu wasomaji/wanablog naomba mnisaidie kunipa jibu.

Friday, April 3, 2009

Video documentary : Taifa linalojengwa na wafanyakazi wa majumbani

Nimeichukua kwa Da Subi kwani najua kuwa wote tuna nia moja.





Nikiwa kama mzazi nimeguswa sana na maelezo katika vido hii kwa kweli ni dhurumana pia naweza kusema unyama kabisa. Soma na sikilizeni wenyewe na semeni mnawanza nini na je huu ni uungwana?

Ni imani yangu kuwa hakuna ubishi ya kuwa elimu ya darasani yenye malengo maridhawa ndiyo msingi mahsusi wa maarifa na maendeleo kwa jamii yoyote ile. Mtizamo huu ndiyo unaonisababisha nisikubaliane na kitendo cha watoto kufanyishwa kazi majumbani kwa kisingizio tu cha kuwa mzigo kwa kushindwa kuendelea na masomo ama ya sekondari au ufundi.

Kazi si adhabu wala dhambi, lakini kazi yenyewe inapofanyika bila kuzingatia mustakabali wa maisha ya wafanyakazi wenyewe, hasara inayopatikana kwa muda uliopotea na kudumaa mawazo ni kubwa kwa wahusika pamoja na Taifa lao. Nchi inakosa kuwa na raia walioelimika kwa kiwango cha kutosha kuchangia katika uchumi wa Taifa lenyewe.

Nadhani, nchi inayojengwa kwa vibarua na ufanyakazi wa huduma za nyumbani haiwezi kuwa na misingi imara katika mipango ya maendeleo. Mtapanga vipi mipango ya maendeleo ikiwa unaopanga nao wanafahamu shughuli za nyumbani tu? Ikiwa uamuzi wetu ni kusema habari ya maendeleo lakini hatuna nia ya kuendelea, basi hakuna sababu ya kuzungumzia mipango ya maendeleo, tuendelee kuishi hivi hivi tu. Lengo letu likiwa ni kuendelea, basi ni dhahiri kuwa inatubidi kubadilisha mifumo yetu na kuachana na kuendelea kufanya shughuli zile zile hasa zisizo za ushindani wa kimataifa huku tukitaraji kuona mabadiliko ya kutufikisha kwenye kilele cha maendeleo.

Kwa kweli tumebakia kuwa Taifa la wapokeaji na watendaji wa mazoea badala ya kuwa Taifa lenye wajuzi na wafikiriaji wa mambo mbadala. Hii haifai.
Film documentary hii inaonesha na kuelezea maisha ya watoto wanaofanya vibarua majumbani.