Showing posts with label ndugu. Show all posts
Showing posts with label ndugu. Show all posts
Wednesday, September 24, 2014
Saturday, January 25, 2014
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA KWA KIPANDE HILI:- NASONGA MBELE....
JUMAMOSI NJEMA SANA....NA TUKUMBUKE YA KWAMBA SISI SOTE NI NDUGU NA WATOTO WA BABA MMOJA!!!!!
Wednesday, April 10, 2013
KUNA ANAYEJUA HABARI ZA MWALIMU MATONDO MASANGU NZULILIMA????
Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza mwalimu Matondo yupo wapi na halafu juzi tu nimeulöizwa na mkereketwa mwingiau niseme mwal. Mhango kama najua habari na ndugu yetu huyu. Kwa kweli sijui kabisa na sasa naona kichwa kimetawala mno..Je? kuna anayejua habari/kitu chochote kuhusu ndugu yetu huyo? Maana ukiangalia hapa inaoshesha ni muda sana aliweka kitu...
Friday, March 1, 2013
CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KATIKA KUUANZA MWEZI HUU WA MACHI/TATU NA IJUMAA YA KWANZA YA MWEZI HUU NI:- WIMBO HUU WA DADA RAY-C UPO WAPI...
Tuanza mwezi huu kwa kujiulizani lini nimewasiliana na baba, mama, babu, bibi, shangazi, mjomba, kaka, dada, mama mdogo, baba mdogo, mtoto, rafiki, mpenzi wangu au hata jirani yako. Kwa hiyo chukua nafasi na mtafute yule mliopoteana na mpeana mawili matatu....NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA WIKI...
Saturday, December 1, 2012
SIKU YA LEO NIMEKUMBUKA LUNDO MBAMBA BAY 2007
Hapa kutoka kushoto ni kaka yangu wa mwisho Philoteo, katikati ni mjomba wangu mwl. John Bosco Ngonyani anajulikana zaidi kwa jina la JB na mwisho ni mwenyewe Kapulya. Siku hii ilikuwa siku ya furaha sana katika maisha yangu kwani nilikuwa sijaonana na mjomba wangu mpendwa karibu mika ishirini ...Muwe na WAKATI MZURI PIA JUMAMOSI NJEMA YA MWEZI HUU WA KUMI NA MBILI AMBAYO NI YA KWANZA NA KESHO NDO TUNAANZA KUSUBIRI ULE UJIO /KUZALIWA WA/KWA BWANA YESU KRISTU.
Sunday, July 22, 2012
NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI WOTE!!
Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda, kuniongoza, kunifanya nipate chakula, na kuniepesha na yasiyo mema. Nakutumaini wewe Mungu wangu , eh Mungu, wewe ni mwamba imara katika maisha yangu ...... Pia napenda kuwaombea familia, ndugu, wazazi/walezi, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzangu pia hata madui zangu. Mwenyezi Mungu na atushushie wote baraka na upendo pia amani ...AMINA. . NA UJUMBE WA LEO NI:- SISI SOTE NI NDUGU,WATOTO WA BABA MMOJA.
Labda tumalizie jumapili na mwimbo huu wa Bony Mwaitege SISI SOTE..
JUMAPILI NJEMA SANA!!!!!
Labda tumalizie jumapili na mwimbo huu wa Bony Mwaitege SISI SOTE..
JUMAPILI NJEMA SANA!!!!!
Thursday, March 15, 2012
KUNA ANAYEJUA NI NINI KUNAMSIBU DADA SUBI?
Wednesday, December 21, 2011
SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!
Habari zenu jamani!!Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2011 na kuingia katika mwaka mpya 2012. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tunaoonyeshana. Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2012 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA LISILOWEZEKANA/KISICHOWEZEKANA. NAONA TUTAENDELEA MWAKANI NA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO YA MADA, MATUKIO MBALIMBALI PIA PICHA.. bila ninyi kipengele hiki hakingeweza kuwa. MBARIKIWE WOTE MTAKAOPITA KATIKA BLOG HII NA NYINGINE ZOTE. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!
Wednesday, September 28, 2011
HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU SHABAN KALUSE!!!
Napenda kuchukua nafasi na KUMPONGEZA KAKA YANGU WA HIARI SHABAN KALUSE kwa siku yake ya kuzaliwa. Shaban Kaluse ni kaka mmoja ambaye ni mshauri mzuri sana , msikilizaji, sio mbinafsi. nk. Nikuambieni kitu kimoja? Ni hivi mimi au pia watu wengine wanafikiri kaka, dada au ndugu ni yule uliyezaliwa naye tumbo moja yaani mama mmoja na baba mmoja. LA HASHA. Kaka huyu amekuwa KAKA kweli na amekuwa mwema sana katika familia ya akina NGONYANI. HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 40 NI MIAKA MINGI MWENYEZI MUNGU AKULINDE NA AKUJALIE AFYA NJEMA!!!
Tuesday, August 30, 2011
NILIPOKUTANA NA MWANABLOG MARKUS MPANGALA
Baada ya kukutana na kaka S hapa Ruaha safari ikaendelea kufika Dar es Salaamau, ikawa bahati tena nika/tukakutana na mwanablog mwingine pia ni mjomba na rafiki wa karibu sana. Si mwingine tena ni Mzee wa Lundu Nyasa.
Alijitahidi na akaja hapa Silver Sands kutusalimia hapa ni yeye Mzee Lundu Nyasa/Markus Mpangala, Yasinta na Kijana Erik.
Na hapa ni Markus na wajomba zake Erik na Dada Camilla.... Ilikuwa ni furaha kukutana na yeye. Kwani kama kawaida huwa furaha sana kuonana tulibadilisha maneno mawili matatu na muda ukawa ni mdogo ....
Friday, August 19, 2011
NAMTAFUTA MDOGO WANGU KWA MAMA MWINGINE "HIARI" KOERO MKUNDI:- JE? KUNA ANAYEJUA WAPO ALIPO?
Ni muda sasa umepita tangu 24/6, mdogo wangu huyu sijamsikia wala kuona katika vibaraza vingine akitoa mchango wake.Si mwingine tena ni Koero Mkundi. Ninakumiss sana UPO WAPI? Je? kuna anayejua alipo. Koero, natumaini na naamini kwamba uko salama; na ukibahatika kusoma ujumbe huu tujulishe uliko koeromkundi.blogspot.com.
Wednesday, June 8, 2011
MSAADA: RENATHA BENEDICTO ANATAFUTWA NA FAMILIA YA MUBELWA BANDIO!!!
Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.
Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu. Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html)
Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio. Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.
Email yangu ni changamoto@gmail.com
NATANGULIZA SHUKRANI
http://www.changamotoyetu.blogspot.com/
http://www.youtube.com/user/mutwiba
Tuesday, December 28, 2010
SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!
Habari zenu jamani!!Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2010 na kuingia katika mwaka mpya 2011. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2011 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA KISICHOWEZEKANA. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!
Thursday, October 28, 2010
WANABLOGGERS KUKUTANA JANA MJI WA TAMPERE
Malkiory Matiya na Mtakatifu Simon Kitururu
wakutana uso kwa uso!!!
Wanablogger hawa walikutana jana katika mji wa Tampare. kujua nini kilitokea huko bonyeza
Mtakatifu Simon na pia Malkiory Matiya. Ila jamani ugimbi huo mmmmhhh!!!
Wednesday, March 3, 2010
AHSANTE MUNGU KWA KUITENDEA FAMILIA YA MZEE NGONYANI MIUJIZA
Tukio hilo lilimtokea mchezaji wa Kimataifa aitwae Nnwanko Kanu. Huyu alikuwa ni mchezaji wa Timu ya taifa ya Nigeria, ambaye alikuwa akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi.
Ni baada ya Kuiwezesha nchi yake kutwaa kombe la Olympic, hapo mnamo mwaka 1996, ndipo alipopanda kilele cha mafanikio na kununuliwa na timu maarufu ya kule Italia inayoshiriki ligi ngumu ya almaarufu kama Serial A.
Mchezaji huyu alinunuliwa na timu ya Inter Milan na ni wakati alipokuwa akifanyiwa vipimo vya afya,(Medical Check Up) ndipo matokeo ya vipimo hivyo vilipoushangaza ulimwengu. Nnwanko Kanu aligundulika kuwa na matatizo ya moyo na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana ili kunusuru afya yake.
Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa akishiriki ligi za kimataifa, akichezea timu ya Ajax ya Uholanzi pamoja na kuchezea timu yake ya Taifa ya Nigeria na kuiwezesha kutwa kombe la Olympic, lakini katika kipindi chote hicho haikuwahi kugundulika kuwa na tatizo hilo. Hata hivyo kulikuwa na kupingana kwingi kitaalamu kati ya madaktari wagunduzi wa tatizo hilo na wale wa Uholanzi, lakini hatimaye alifanyiwa upasuaji na kurejea katika anga za michezo na kupata mafanikio makubwa.
Nimelikumbuka tukio hili kutokana na kile kilichomtokea mdogo wangu Asifiwe, huyu ni mdogo wetu wa mwisho kuzaliwa. Tukiwa tumezaliwa wanaume watano na wanawake wawili, yaani kati ya watoto saba wa Mzee Ngonyani na mama Ngonyani tuko watoto wakike wawili tu, yaani mimi na huyu mdogo wangu Asifiwe.
Akiwa darasa la sita ndipo alipoanza kuugua, ghafla, na tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ilikuwa ni tatizo la kukosa nguvu ghafla na kubanwa na kifua, lilikuwa ni tatizo ambalo kule Songea katika Hospitali ya Peramiho hawakuweza kugundua kuwa ni tatizo gani lakini kwa juhudi za madaktari aliweza kupewa tiba ambayo hata hivyo ilimletea nafuu badala ya kumponyesha.
Ni mwaka jana mwezi wa pili nilipokuwa nyumbani Tanzania ndipo nilipokata shauri tumpeleke katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi. Ni hapo ndipo tulipo shangawa na matokeo ya vipimo kuwa mdogo wetu Asifiwe anayo matatizo ya Moyo na anatakiwa kufanyiwa Upasuaji nchini India.
Naamini hata wewe unayesoma hapa unaweza kuhisi ni kwa kiasi gani nilikuwa naumia kwa kile kilichomtokea mdogo wetu.
Hata hivyo baada ya kushauriana na madakatari alipangiwa kuwa awe anakuja pale Muhimbili kwa ajili ya matibabu yaani kliniki huku mchakato wa kufanyiwa upasuaji nchini India ukiendelea.
Kwa hiyo akawa anakuja Muhimbili na kurudi Songea (Ruhuwiko). Lakini mara hii ya mwisho yaani mwezi wa kwanza mwaka huu alipofika Kliniki aliandikiwa kufanyiwa upasuaji hapa hapa nchini na hivyo kulazwa pale Muhimbilli akisubiri kufanyiwa upasuaji.
Ni katika kipindi hicho sala na maombi vilifanyika kumuomba mungu afanikishe upasuaji huo ili mdogo wetu apone na kurejea shule kuendelea na masomo.
Mnamo tarehe 16/02/2010 mdogo wetu Asifiwe alifanyiwa upasuaji wa moyo na kwa uwezo wa Mwenye Enzi Mungu upasuaji ulikwenda vizuri na ijumaa tarehe 27/02/2010 ametolewa nyuzi zake na tarehe 01/03/2010 jumatatu ameruhusiwa.
Leo napenda kumshukuru Mwenye Enzi Mungu, Madaktari, Manesi na watu wote kwa Juhudi zao katika kumuhudumia mdogo wetu Asifiwe, sisi tunasema kwamba kwa uwezo wake ameweza kuisimamia kazi hiyo ya madaktari na kufanikisha upasuaji huo.Pia shukrani nyingi sana kwa daktari Mrs. Mushi wa kule Peramiho yeye ndiye aliyetupa ushauri wa kumpeleka Asifiwe, Kwanza katika kliniki moja hapa Dar ya Dr. Johnson M. Lwakatare. na ndipo tukapata rufaa ya kwenda Muhimbili .
Sisi tunaamini ni mungu pekee kwa kupitia mikono ya madaktari wale pamoja na manesi ameweza kufanikisha upasuaji huo. Nakumbuka siku tatu kabla ya kufanyiwa upasuaji huo nilizungumza na mdogo wangu, na kwa huzuni alinijulisha kuwa watoto wawili wa kike ambao walitangulia kufanyiwa upasuaji kabla yake wamepoteza maisha, ni watoto ambao walikuwa wana umri wa chini ya miaka 10, na walihitaji bado kuishi lakini Mwenye Enzi Mungu aliwapenda zaidi, na hivyo kuwatwaa. Ila namsifu Asifiwe, yeye hakuwa mwoga isipokuwa hakupenda kama ingetokea bahati mbaya kutuacha sisi nduguze.
Tulifanya maombi kwenye simu na nilimpa moyo mdogo wetu kuwa yote tumuachie Mungu kwani tunaamini atatenda miujiza. Lakini hata hivyo upasuaji uliahirisha tena kutokana na ziara ya ghafla ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alipotembela hapo hospitali ya Muhimbili kuzungumza na madaktari.
Leo hii kwa niaba ya familia ya mzee Ngonyani napenda kuchukua nafasi hii kusema Ahsante Mungu kwa kuitendea familia ya Mzee Ngonyani Muujiza, Pia ningependa kuwashukuru wote mliokuwa nasi katika sala, katika kutupa moyo wakati tulipokuwa na mawazo. Na shukrani nyingi zimfikie kaka yetu Ngonyani na mkewe wa pale Kinondoni Kinondoni Mkwajuni kwa kuwa karibu nasi wakimhudumia mdogo wetu katika kipindi chote alipokuwa akija kliniki na hata wakati wa kufanyiwa upasuaji. Ninawashukuru kwa kuwa walitumia muda wao mwingi kwenda na kurudi Muhimbili ili kuhakikisha mdogo wetu Asifiwe hajisikii mpweke.
Na pia napenda kumpongeza yeye mwenyewe Asifiwe kwa kutoonyesha uoga.
Ningependa kuzisindikiza shukrani hizi kwa wimbo wa Upendo Nkone uitwao Hapa nilipo.
Thursday, November 26, 2009
NAPENDA KUMPONGEZA MDOGO WANGU PEKEE, KWA KUTIMIZA MIAKA LEO... HONGERA SANA MDOGO WANGU!!

Ni mdogo wangu wa mwisho.
Leo ni siku maalum na ya pekee kwa mdogo wangu. Ilikuwa si muda mrefu nilikubeba na ukanikojolea mkojo mgongoni. Kweli sasa naamini miaka inazidi kwenda tena inakimbia kwa haraka sana. Sisi wote hapa nyumbani tunapenda kukupa HONGERA sana kwa kutimiza miaka. Na tunakuombea uwe na maisha mazuri, pia nakuombea kwa sala hii, Mungu akubariki, akuongoze, akufariji na akusaidie katika mambo yako. HONGERA SANA MDOGO WANGU MPENDWA KWA KUTIMIZA MIAKA . HONGERA MAMA MDOGO, SHEMEJI , RAFIKI NK. NAAMINI UNA WAKATI MZURI!!!!!
Tuesday, November 10, 2009
UJUMBE KUTOKA SWEDEN KWA KAKA LAURENT KINUNDA
Katika ukuaji wangu/akili yangu nilikuwa nafikiri ya kwamba ndugu ni yule mliyezaliwa mama mmoja na baba mmoja. Lakini kumbe nilikuwa na mawazo finyu. Ndugu ni mtu yeyote yule sio TU yule mliozaliwa tumbo moja.
Ilikuwa mwaka 1993 nilipokutana kwa mara ya kwanza na kaka LAURENT KINUNDA. Kaka Laurent, napenda kukushukuru kwa moyo ulio nao, wema wako na upendo wako. Umekuwa karibu sana nasi. Umekuwa huna kinyongo na familia yangu mara kunapotokea shida pia kunapokuwa na raha unakuwa nasi.
Nakumbuka kila tujapo TZ, hakuna mwingine anayekuja kutulaki uwanja wa ndege, isipokuwa ni wewe kaka Kinunda. Kwa hili napenda kutoa shukrani zangu/zetu za dhati. Umekuwa nasi katika matukio mbalimbali na umetusaidia na unatusaidia mambo mengi ambayo siwezi kuyahesabu hapa. Ninachoweza kusema. NAOMBA MWENYEZI MUNGU AKULINDE WEWE NA FAMILIA YAKO MUWE NA AFYA NJEMA NA MAISHA MEMA. TUNAWAPENDA WOTE. UPENDO DAIMA.

Tuesday, September 8, 2009
UZOEFU WANGU KATIKA MAISHA AMBAO SITAUSAHAU
Kuna mambo mengi katika maisha ambayo kama wanaadamu tunakuwa tumeyapitia, hayo yote ndio huyafanya maisha haya tunayoishi yawe na maana. Miongoni mwa mambo au masaibu tuliyokutana nayo yapo ya kufurahisha na ya kuhuzunisha na mengine yenye kukera na kutia kinyaa, lakini yote ni maisha na yalikuwa ni lazima yatokee ili kujifunza jambo fulani.
Lakini hata hivyo si rahisi kusahau kila jambo ulilokumbana nalo katika maisha hasa kama lilikuwa ni la kuumiza kihisia, lakini kuna wengine wanasahau upesi na wengine si rahisi kusahau. Kwa mfano kwa upande wangu mimi kuna jambo moja, ambalo mimi SITALISAHAU. Nakumbuka nilikuwa na miaka 10 wakati huo. Baba na mama walikwenda hospital Litembo iliyoko katika wilaya ya Mbinga, mkoani Songea. Mimi na kaka zangu tulibaki kwa baba mkubwa.
Huyu baba mkubwa alikuwa na watoto wa kike 6 na mwanae mkubwa wa kike aliitwa Maria. Siku moja jumapili Nilimwomba dada Maria kanga kwani mimi nilikuwa sina, lakini hakunipa ALININYIMA na kuniuliza kwa nini baba yangu ambaye ni mwalimu asininnunulie. Kwani wakati ule nilikuwa mtoto wa kike peke yangu. Nayeye katika hali ya kinisimanga aliniambia "wewe uko peke yako mtoto wa kike inakuwaje wazazi wako wanashindwa hata kukununulia kanga" .(Mwana mdala nga veve vishindwa kukugulila nyula). Aliongea kwa Kingoni. Siku ile nililia sana, mpaka sasa nalikumbuka vizuri tukio lile na mpaka leo roho inaniuma sana kila nikikumbuka maneno yale.
Sikujua kama binadamu wanaweza kuwa wakatili kiasi hiki, na hasa ukizingatia yeye alikuwa dada yangu. Naomba nikiri kuwa tangu tangu siku ile sijawahi kuwasiliana naye, ingawa sina ukakika kama atakuwa analikumbuka tukio hilo. Kwani waswahili wanasema mtendaji hakumbuki ila mtendewa ndiye anayekumbuka.
Mimi kama walivyo binadamu wengine ninao udhaifu wangu, na udhaifu huo si mwingine bali ni kutomudu kufanya kazi ngumu tangu utototni mwangu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kule kingoli maisha yalikuwa magumu sana kwangu, kwani kulima mpunga na pia karanga na mihogo ilikuwa ni shughuli ambayo ilikuwa inanipa shida sana, ilikuwa kila tukienda shambani, mimi nilikuwa wa mwisho kumaliza ngwe yangu kule shambani.
Mazao ambayo tulikuwa tunalima sana ni karanga na mpunga tangu asubuhi mpaka mchana. Halafu kule kingoli tulikuwa tunakula sana ugali wa muhogo na kwa kuwa sisi tulihamia kule, tulikuwa hatuna shamba la mihogo. Kwa maana hiyo ilibidi tununue, ndugu yangu huko tulikokuwa tukinunulia hiyo mihogo kulikuwa ni mbali, yaani tunatembea mpaka miguu inauma. Tulikuwa tunachimba, kumenya kabisa ili uzito upungue.
Baada ya hapo tunarudi na mzigo kichwani na jua linawakia utosini. tukifika nyumbani na kutua mzigo, kuna kazi ya kuandaa chakula cha mchana. Tukishamaliza kula tunapumzika kidogo kisha tunaanza kazi ya kuchotelea maji ya kulowekea ile mihogo. Kwani kulikuwa hakuna maji ya bomba, tulikuwa tunachota kisimani. Jamani kweli maisha ni safari ndefu.
Kusema kweli kila nikikumbuka maisha niliyopitia kule kijijini kwetu, kuna wakati ninalia na kuna wakati huwa ninacheka sana. Kwa simulizi hii sio kwamba nilikuwa namlaumu dada yangu mkubwa kwa kitendo chake cha kunisimangia kanga yake, kwani ilikuwa ni hiyari yake kunipa au kutonipa, kilichoniuma ni yale masimango, hata hivyo simlaumu kwani kuna jambo nilijifunza, kutokana na kitendo chake kile.
Kama kuna mtu yeyote ambaye ataumizwa na simulizi hii basi anisamehe, kwani sio nia yangu kumuumiza mtu bali nilitaka kusimulia uzoefu wangu juu ya maisha haya tunayoishi, kwamba, kumfanyia mtu wema ni sawa na kuweka akiba ambayo inakufaa kesho..

Sunday, July 12, 2009
NAPENDA KUMPA HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU
Subscribe to:
Posts (Atom)