Monday, October 28, 2019

AINA MBALIMBALI YA VIFAA VINAVYOTENGENEZWA NA UDONGO WA MFINYANZI



Soko la vyungu vya asili vinavyotokana na udongo wa mfinyanzi. Si rahisi hasa kwa vijana wetu waliokulia mjini kufahamu umuhimu wa vyungu hivi. Kwani vijana wa zamani tunakumbuka jinsi mama zetu, shaangazi zetu na bibi wazaa mama au baba jinsi walivyotumia vyungu hivi kupikia na jinsi chakula kilichotoka humo kilivyokuwa na ladha na utamu wa aina yake. Lakini pi tunakumbuka jinsi ambavyo vyungu hivi vilitumika kama jokofu. Kwa kuweka chungu kilichojaa maji juu ya mafiga matatu, na kuweka mchanga chini ya chungu na kunyunyizia maji mchanga huo, maji yalikua yakipoa na kuwa ya baridi kana kwamba yametoka kwenye jokofu.

Sunday, October 13, 2019

VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA...SAMAKI NA VYOTE VYA ASILI HASA VYA KUPIKIA KWENYE VYUNGU

 Ni aina ya samaki kama hujaonja jaribu
Na hapa ni vyakula mbalimbali  vya asili viöivyopikwa kwenye vyungu utamu wake ni ngumu kuelezea  bora uonje mwenyewe.

Tuesday, October 1, 2019

LEO NILIKWENDA MSTUNIKUCHUMA UYOGA ...

Msimu ni ule majira ya kupukutika kwa majani. Kwa hiyo ni msimu wa uyoga pia kwa hiyo wapenzi wa uyoga tunafurahia sana kwenda mstuni na kuchuma/kutafuta uyoga. Kumbuka uwapo msituni sio unachuma uchoga tu ...La hasha ni mazoezi makubwa sana na pia  kama ulikuwa na msongo wa mawazo basi msitu ni sehemu nzuri sana na kuwa.
Nawatakieni kila la kheri  tuonane tena panapo majaliwa.....kapulya wenu!