Showing posts with label mboga. Show all posts
Showing posts with label mboga. Show all posts

Saturday, April 25, 2015

KARIBU:- KUNA USHIBE!!

Naanza bila mpango, Kwa tenzi pia na tungo,
Niyafumbue mafumbo, Ugali na mbogamboga.
Wanadharau mapishi, Wanayabeza mapishi,
Mapishi ya Waswahili, Ugali na mbogamboga.
Umeyasifu matango, Mazuri sana kwa macho,
Huleta ngozi nyororo, Ugali na mbogamboga.
Na uyoga asilia, Kushiba bila ya kula,
Nashiba na kutazama, Ugali na mbogamboga.
Ugali huo wa sembe, Sembe nyeupe pepepe,
Na dona usiutupe,Ugali na mbogamboga.
CHANZO : KWA MJENGWABLOG

Saturday, July 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELE...

 Ni mboga ya maboga na mahindi, ila hasa mboga maboga. Hii imekubali sana na nimeanza kula lakini mchicha na figiri mwaka huu vimekataa kabisa. Hata sijui kwa nini...
 Na hapa ni viazi mviringo na mahidi ...Mahindi nilijaribu tu  yanakaribia kuchanua ila sijui kama nitavuna muhindi. Ila viazi karibu nitavuna kwani sasa vinachanua kwa hiyo mwezi ujao tutakula.
Mwaka huu tutakula na ZABIBU  kama mnavyoona hapa:-)
JUMAMOSI NJEMA BINAFSI NIPO LIKIZO KWA HIVYO MKIONA SIPATIKANI  MJUE  MAJUKUMU. ILA SITAPOTEA SANA MAANA SISI NI NDUGU LAZIMA KUTAKIANA HALI.

Friday, April 11, 2014

MAMBO YA BUSTANI YANANUKIA NUKIA :-) TUMALIZE JIONI HII YA LEO KIHIVI UKULIMA!!!

Hii ni ile BUSTANI yetu, nilikuwa kimyaaaa, nilikuwa natifuatifua. Karibuni tu kutakuwa na zile mbogamboga na viungo. Hivyo vionekanavyo hapo ni vitunguu saumu. Nilipata ushauri kuwa ukipata mwezi wa kumi mapema mwanzoni mwa mwaka au kama baridi imepungua huchipua kwa haraka:-) Nimekwisha atika atika baadhi ya mbegu ndani kwenye makopo kama kawaida:-) ZAIDI MAENDELEO YA BUSTANI YATAKUJA....JIONI NJEMA NDUGU ZANGU!!

Friday, November 15, 2013

HAYA NI MAPISHI YA IJUMAA YA LEO KUKU.....KARIBUNI

Ijumaa ya leo itakuwa kuku ambayo ni:- kuku mzima, viazi, karoti, kitunguu, kitunguu saumu, tangawizi, nyanya kopo, binzari, mafuta, chumvi na maji..... Picha zaidi zinakuja baada ya muda tu....Kwa hiyo mnakaribishwa kujumuika nasi.

Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.

Thursday, May 16, 2013

MAANDALIZI YA BUSTANI ZA MBOGA NA MAUA YAMEANZA...ANGALIEANI WENYEWE...KARIBUNI TUJUMUIKE!!!!

 Hapa ni baadhi ya matu ya bustani yangu ...maandalizi yameanza..leo mnaona udongo tu hapa baada ya wiki mtaona mimea....
 Katika maisha inabidi uwe mtundu hapa nilikwisha andaa baadhi ya miche kama vile NYANYA na Miche ya mboga ZA MABOGA,,ujanja eeeehhh
Mdada/kapulya hapendi shughuli za bustani za mboga tu ni mpenzi sana wa bustani sana wa bustani za maua kama mnavyoona hapa na mawe pia....kwa hiyo msione nipo kimya nipo ...daima pamoja...anayejisikia kuja kusaidia anakaribishwa..majembe yapo mengi tu:-)

Saturday, May 11, 2013

PICHA YA WIKI..MAMA NISHUCHE NATAKA KUCHEZA...

Inaonekana mtoto hataki kubebwa au sijui kaona kitu fulani anataka akachukua??? Au wenzangu mwasemaje? ...mmmmhhh nimetamani mchicha na chaina hiyo ngoja nami nianze kulima bustani yangu...JUMAMOSI NJEMA..

Wednesday, December 5, 2012

MCHANA WA LEO NINGEPATA MLO KAMA HUU NINGEFURAHI SANA LAKINI SASA ITANIBIDI NILE KWA MACHO....

Ni ugali kwa mlenda uliochanganywa kwawa majani ya maboga na ambayo bamia. Halafu  bakuli la (ma)tembele la kuchemshwa kwa nyanya na kitunguu. Bila kusahau pilipili shamba.
Hakika hapa ni utamu, na tena ule wa asili kabisa ,yamu yamu yamu....NAWATAKIENI WOTE SIKU /JUMATANO NJEMA SANA.