Kutokana na maoni ya msomaji mmoja katika mada ya WANAWAKE UGHAIBUNI (SWEDEN). Nimeona ni vizuri mkijua ya kwamba:-
Maisha ya ndoa ya Afrika na hapa Sweden kila ninapojaribu kuwaelezea watu kuwa. Sisi waAfrika tunapokaribia umri wa kuoa kitu cha kwanza ni kutafuta mchumba na ukishampata zinaanza shughuli za kupanga mahari (posa). Lakini wao wanashangaa sana hata hawaelewi kabisa kwa nini tunatoa MAHARI(POSA). Wao wanadai ya kwamba tunauzwa, kama kuku. Yaani mzazi wa msichana anamuuza binti yake. Wanasema kama tunatoa mahari (posa) kwa kuwashukuru wazazi wa upande wa kike je? kwa nini na wazazi wa upande wa kiume wasipongezwe kwa kazi nzuri ya kumtunza kijana wao. Hata kama ukiwaambia ni njia ya kuonysha respect pia hawaelewi kabisa.
Hapo zamani hapa Sweden ilikuwa hivi , msichana akiolewa yaani anapoenda kuanza maisha kama mke. Alikuwa anachukua vitu toka kwao kama vile shuka, vyombo nk. Ni kama nyumbani TZ
Lakini siku hizi hiyo haipo hapa wanaoana/ishi tu hivihivi. Hakuna kutoa mahari ( posa) .
Naomba niseme hivi inaonekana kama watu wengi wanafikiri ukitoa MAHARI (POSA) basi ndio utakuwa mtawala. Yaani wanaume wengine wanakuwa na kasumba, wanajiona wakubwa wa nyumba, na mke anakuwa hana sauti. Anasema mi nimetoa MAHARI (POSA) kwa ajili yako.
Ndugu wasomaji kusema kweli sisi wanadamu tunaishi katika mila na desturi tofauti kabisa. Kwani hapa wao hili jambo la ndoa halihusishwi kabisa kwa wazazi. Ni baina ya kijana na msichana. wanaelewana wao wawili tu kama kufunga ndoa au kuishi hivihivi Naweza nikasema hii ni moja ya sababu ndoa zao hapa hazidumu muda mrefu. Haya wasomaji je kuna maelezo zaidi ya kuwaeleza watu hawa. Naomba MCHANGO basi.