Ni juzi tu nilikuwa dukani kapata mahitaji kama kawaida binadamu lazima ale/tule..Nikafika kwenye matunda nikakutana na matunda ya kila aina mojawapo lilikuwa tunda la EMBE, nikapata hamu LAKINI KUJA KUANGALIA BEI NIKANYWEA...EMBE MOJA NI Tsh. 4868...mmmhhh nikakumbuka nyumbani jinsi miti ya miembe ilivyozunguka nyumba nikaacha.....nikaendelea na matunda mengine.......
Nikakutana na karakara (Passion) nikaangalia weee nikapumua kwa hiyo bei tena ...Tsh. 1696 kwa karakara (passion) moja nikaanza kukumbuka.....
Kazi ya mikono yangu...mikarakara yangu(mapassion)
........karakara (passion) zangu nilizonayo nyumbani Ruhuwiko-Songea. Ambazo ni freshi kabisa yaani kutoka tu nje na kuchuma. Nakwambia nusu nilie:-( Ebu angalia hapa...basi nikaamua kufanya ubahili. Yaani sikununua nimepata hasira ya kuanza kuongeza kupanda miche ya mikarakara (mipassio/mipasheni) zaidi... Nguja niache niwaachie na wengine wasema...
panapo majaliwa wapendwa.